Arusha - Nalaani vikali kauli zilizotolewa na viongozi wa CUF

mwitaz

JF-Expert Member
Feb 19, 2012
315
93
Naendelea Kulaani vikali kauli zilizotolewa na Viongozi wa CUF kwanyakati tofauti kwenye mkutano wao wa ndani.......... . sorry mkutano wao wa wazizi hivi majuzi hapa Arusha eti Vijana na nguvu kazi ya Arusha inatumiwa vibaya na wanasiasa na eti tunaongwa Viroba ya pombe ili tufanye fujo! kwakweli kauli hizi zimejeruhi nafsi yangu na vijana wapenda mabadiliko wa Arusha kwa sababu

1) Vijana wa Arusha hatuja wahi kufanya fujo yeyote ya kisiasa zaidi ya kuunganisha sauti zetu na kukataa dhuluma na ufisadi
unaofanywa na chama Tawala kwa wananchi wa Tanzania

2) Pili hatuja wahi kuongwa viroba na kiongozi yeyote yule wakisiasa ili tukafanye fujo na wala hatupo tayari kuhongwa viroba ili
tufanye fujo yeyote.

3) Tatu hakuna kijana yeyote mkoani Arusha anatumika au kutumiwa kisiasa Vijana wa Arusha tunajielewa na tunataka ukombozi wa kweli wa kifikra, uhuru,na uchumi.

4) Nne harakati za kutafuta ukombozi hapa Arusha si kazi ya vijana peke yake, kuna Wazee, Umri wa kati, Vijana na watoto. baada ya kutabanaisha haya Natoa Rai kwa uongozi wa CUF popote pale walipo: Kwana wafute kauli na matamshi yao waliyo yatoa
hadharani Pili uongozi wa CUF uwaombe radhi Vijana wa Arusha na wapenda maendeleo kwa ujumla kwa kudhalilishwa na kwa
nafsi zao zilizo jeruliwa kwa kauli hizo.

Nawasilisha.
 
Aim sorry to say this but vijana wa arusha wanatumika vibaya na wanasiasa .. maneno ya cuf Yamaha ukweli ndani yake
 
Huu msamiati wa kutumika kisiasa binafsi huwa unanishangaza. Wanatumikaje wakati wao wenyewe ndo wameamua kushiriki siasa wakiwa na akili zao timamu??? Nini maana ya kutumika kisiasa??? Kama wanatumika kisiasa na chama kimoja, kwa nini vyama vingine navyo visiwatumie kisiasa??? Au ndo chama kinapozidiwa kiushindani kinaamua kutafuta misamiati tata na kuifanya ndo sehemu ya sera zao??? Ni upuuzi kwa mwana siasa kulalamikia mbinu za mwenzio anazotumia wakati havunji sheria, na wewe buni za kwako mpambane kwenye ulingo wa siasa tuone nani anaibuka mshindi.
 
Aim sorry to say this but vijana wa arusha wanatumika vibaya na wanasiasa .. maneno ya cuf Yamaha ukweli ndani yake

Umezoea kuwatumikia mabwana wako mafisadi nna hivyo unafikiri kuwa hata vijana wa Arusha wako kama wewe.
 
mkuu mwitaz hawa cuf wanafanya kazi waliyotumwa na mabwana zao ccm watatukana sana lakini vijana wa arusha wanajua kuchambua mchele na pumba
 
Naaapa kwa jina la mwenyezi mungu hakuna wakati nimewahi kumdharau mtu katika maisha yangu kama nilivyo mdharau profesa lipumba kwa maneno yake arusha juzi
yaani yeye kuolewa na ccm tu basi akili yake ya uprofeseri kwishney
 
ndugu yangu mwitaz wala usiumize kichwa, cuf wanatekeleza matakwa ya mwandani wao ccm.
ukweli uko wazi kwamba hii technic ya kuwanywesha vijana viroba imekuwa ikitumiwa na ccm muda mrefu sana lakini sasa vijana wamestuka na kuamua kuunganisha nguvu kwa kusupport chama kinachopigania haki za watanzania wote-Chadema hivyo mtu na mke wake wanaweweseka.

Kila mahali wanapokwenda ccm wakakosa watu wa kuhudhuria mikutano yao ama wakiongea utumbo wakazomewa na wananchi wanaishia kulalamikia viroba. ccm na cuf ni wataalamu wa kugawa viroba kama walivyo wataalamu wa kusomba watu kwa mafuso kuhudhuria mikutano yao. Lakini kwa Chadema unajua hali ni tofauti, watu wanakwenda wenyewe kwa nauli zao.
 
Last edited by a moderator:
Aim sorry to say this but vijana wa arusha wanatumika vibaya na wanasiasa .. maneno ya cuf Yamaha ukweli ndani yake
Kwahiyo hapa unamaanisha yale mauwaji ya Janualy 2001 na moja kule Zanzibar CUF na hasa huyu Maalim Seif alikuwa anawatumia Wapemba kufanikisha Political Agenda na sasa amefanikiwa anakula mpaka amevimbiwa ndio anakuja na style ya nyani halioni kundule?

Hivi kuwasafirisha vijana kutoka Buguruni mpaka Arusha huku kama siyo kuwatumia tuwaitaje? CUF wanapaswa kuwaomba radhi vijana wa Arusha otherwise sintoshangaa next time nikisikia wamechezea mkong'oto kama alivyofanywa Mtikila kule Tarime.
 
Kafu wanatekeleza maagizo ya mme wao,si wamepewa pesa za kuzunguka nchi zima??wewe unadhani watafanya nini,lazima watekeleze.
 
Naaapa kwa jina la mwenyezi mungu hakuna wakati nimewahi kumdharau mtu katika maisha yangu kama nilivyo mdharau profesa lipumba kwa maneno yake arusha juzi
yaani yeye kuolewa na ccm tu basi akili yake ya uprofeseri kwishney

Mkuu anachokipata kwa mumewe anakijua mwenyewe, so yuko tayari hata kujivunjia heshima yake kwa ajili ya kumtumikia mumewe
 
Maswali safi kwa wakati muafaka!
Hakika ndug njiwa hatoweza kujibu bali atakimbia hoja au ata toka nje ya hoja!
Big up lets wait for Answers from Mh Njiwa!

Kwahiyo hapa unamaanisha yale mauwaji ya Janualy 2001 na moja kule Zanzibar CUF na hasa huyu Maalim Seif alikuwa anawatumia Wapemba kufanikisha Political Agenda na sasa amefanikiwa anakula mpaka amevimbiwa ndio anakuja na style ya nyani halioni kundule?

Hivi kuwasafirisha vijana kutoka Buguruni mpaka Arusha huku kama siyo kuwatumia tuwaitaje? CUF wanapaswa kuwaomba radhi vijana wa Arusha otherwise sintoshangaa next time nikisikia wamechezea mkong'oto kama alivyofanywa Mtikila kule Tarime.
 
Hakika Cuf ni wakusamehe na washangaa kwa nini wanapambana na cdm!
 
Na huo ndiyo ukweli, nawaunga mkono CUF kwa kusema ukweli, mnatumiwa vibaya na wanasiasa mnasahau haki na wajibu wenu kuendeleza nchi
 
Huu msamiati wa kutumika kisiasa binafsi huwa unanishangaza. Wanatumikaje wakati wao wenyewe ndo wameamua kushiriki siasa wakiwa na akili zao timamu??? Nini maana ya kutumika kisiasa??? Kama wanatumika kisiasa na chama kimoja, kwa nini vyama vingine navyo visiwatumie kisiasa??? Au ndo chama kinapozidiwa kiushindani kinaamua kutafuta misamiati tata na kuifanya ndo sehemu ya sera zao??? Ni upuuzi kwa mwana siasa kulalamikia mbinu za mwenzio anazotumia wakati havunji sheria, na wewe buni za kwako mpambane kwenye ulingo wa siasa tuone nani anaibuka mshindi.

Nahuyu pia anayesema sii pia anawataka watumie kisiasa au kwa hiyo ngoma drooo
 
Back
Top Bottom