Ziara za mawaziri mikoani balaa
2007-10-08 09:27:14
Na Waandishi Wetu
Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Bw. Henry Daffa Shekifu, amelazimika kuingilia kati na kuwasihi wananchi wa wilaya ya Hanang wasimzomee Waziri wa Mipango Uchumi na Uwezeshaji, Dk. Juma Ngasongwa, anaripoti Zillipa Joseph wa PST kutoka Hanang.
Bw. Shekifu aliwataka wananchi waliohudhuria katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya soko mjini Katesh kutoa nafasi kwa viongozi kujieleza badala ya kuzomea.
Hali hiyo ilijitokeza baada ya Dk. Ngasongwa kujibu maswali ya baadhi ya wananchi waliohudhuria katika mkutano huo.
`Tufautishe mikutano. Mkutano huu sio wa kampeni ni wa serikali, tutoe nafasi kwa viongozi, tusitunishiane misuli tukapoteza amani, na amani ikivunjika kuirudisha ni kazi. Kama kuna mwananchi anataka kubadilisha mkutano huu uwe wa kampeni nitamdhibiti kwa nguvu za serikali,` alionya Bw. Shekifu.
Baadhi ya maswali yaliyoulizwa na wananchi hao ni kutaka kufahamu ni kwa sababu� gani serikali inawasambaza mawaziri na manaibu wao mikoani kuelezea bajeti, na kudai kuwa huo ni ubadhirifu wa fedha za walipa kodi, wakati wananchi wanataabika na bei za bidhaa kupanda.
Swali lingine lilihoji uhalali wa kumsimamisha mbunge wa Jimbo la Kigoma Kaskazini Bw. Zitto Kabwe, kuhudhuria vikao vya Bunge huku wananchi hao wakidai kuwa ziara hiyo ni sehemu ya kukipigia debe Chama Cha Mapinduzi(CCM).
Akijibu maswali hayo, Dk. Ngasongwa alisema Bw. Zitto, anajitafutia umaarufu na kuongeza kuwa alitoa lugha ya matusi bungeni ndio sababu ya kusimamishwa kuhudhuria vikao.
`Wabunge wenyewe ndio waliomhukumu kwa sababu alikiuka utaratibu,` alisema.
Kuhusu mfumuko wa bei,� alisema hali hiyo inasababishwa na majanga ambayo Tanzania iliyopata kama ukame na mafuriko.
Alisema hali hiyo iliilazimu serikali kutenga fedha za dharura kutumika na kuifanya nchi katika hali ngumu.
Kuhusu mawaziri kufanya ziara kuelezea bajeti, alisema inawalazimu kufanya hivyo ili kujibu shutuma zinazotolewa na vyama vya upinzani kuhusu bajeti hiyo.
Aliongeza kuwa serikali haitumii fedha vibaya bali wapinzani ndio wanatumia kodi za wananchi kwa kukodi helikopta na kufafanua kuwa vyama vya upinzani vyenye wabunge vinapata ruzuku kutoka serikalini.
`Kati ya mimi niliyefika hapa kwa gari na hao wanaokuja kwa helikopta nani mfujaji?` aliuliza Dk. Ngasongwa.
Mara baada ya kusema hivyo, wananchi hao walilipuka na kukataa majibu hayo huku wengine wakianza kuzomea hali iliyomfanya Mkuu wa Mkoa wa Manyara, kushika kipaza sauti na kuanza kuongea na wananchi na kusema anasikitishwa na tabia hiyo ya aibu ya kutomheshimu kiongozi mkubwa kama huyo.
Awali akihutubia wananchi hao, Dk. Ngasongwa alisema serikali imetenga shilingi trilioni sita na kutaja vipaumbele vya utekelezaji wa bajeti hiyo kuwa ni kuboresha sekta za elimu, miundombinu, afya, kilimo na maji ili kumwezesha mwananchi kujiinua kiuchumi.
Alisema katika sekta ya elimu wametenga Sh. trilioni moja, miundombinu bilioni 777, afya bilioni 590, kilimo bilioni 379 na maji 309.
Aidha waziri huyo aliwataka wananchi kuhakikisha wanafuatilia maendeleo ya watoto wao shuleni kwa kushirikiana na walimu ili kupata wanafunzi wa vyuo vikuu miaka ijayo.
Katika ziara hiyo Dk. Ngasongwa anatembelea wilaya za Mbulu, Hanang, Babati Mjini na Babati Vijijini.
Wakati huo huo, Bigambo Jeje wa PST anaripoti kutoka Musoma kuwa Naibu Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk. Deodatus Kamala, mwishoni mwa wiki alipata wakati mgumu baada ya kuzomewa na wananchi katika mkutano wa hadhara na kulazimika kulikimbia jukwaa.
Alikumbana na mkasa huo katika mkutano uliofanyika katika kata ya Nyasho Manispaa ya Musoma mkoani Mara na baada ya kuona anazidi kuzomewa aliteremka haraka jukwaani na kuondoka.
Dk. Kamala alianza kuzomewa na wananchi hao baada ya kutetea tuhuma zilizoelekezwa kwa Waziri wa Miundombinu Bw. Andrew Chenge na viongozi wengine waliotajwa kuhusika katika kashfa ya ufisadi iliyotolewa siku za hivi karibuni na kambi ya vyama vya upinzani.
Wananchi hao waliamua kumzomea Naibu waziri huyo mara tu alipoanza kumtetea waziri mwenzake huku akibeza kauli za kambi ya upinzani kuhusiana na kashfa ya rushwa.
Dk. Kamala alisema tuhuma dhidi ya vigogo hao akiwemo Waziri Chenge hazina msingi kwa kuwa wapinzani hawana ushahidi wowote.
Alisema serikali ya CCM itaendelea kutawala tu hata kama wapinzani watazidi kuwashambulia viongozi wa serikali.
Alisema wamechaguliwa na wananchi kwa zaidi ya asilimia 80 huku akiwabeza wapinzani kwamba kama na wao wanataka kutawala basi waombe ridhaa kutoka kwa wananchi.
`Tutaendelea tu kutawala hata kama wapinzani watazidi kutushambulia na kutupaka matope, ukiona wapinzani wanatusifu mjue kuwa CCM na serikali yake inaelekea kubaya lakini mkiona wanatupaka matope ni dalili ya kwamba kazi yetu kwa wananchi ni nzuri,` alisema licha ya mayowe ya kuzomea ya muda wote kutoka kwa wananchi.
Hali ya kuzomeazomea ilizimwa na mjumbe wa Halmashauri Kuu ya (CCM) Taifa, Bw. Vedastus Mathayo, ambaye pia ni Mbunge wa Musoma mjini.
Aliposimama alijibu baadhi ya maswali yaliyokuwa yameulizwa na wananchi katika mkutano huo, majibu ambayo yalionekana dhahiri kuwaridhisha na hivyo kushusha jazba waliyokuwa nayo hapo awali.
Kwa upande wake, Waziri wa Miundo mbinu, Bw. Andrew Chenge alisema hawezi kujibu tuhuma hizo kwa kuwa hata kama atajieleza vipi wananchi hawawezi kuridhika na majibu yake.
Alisema angependa kuongelea mambo mengine ya maendeleo kuliko kuchukua muda mwingi kujibu tuhuma kama hizo.
Wakati huo huo, Wazee wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilayani Geita, mkoani Mwanza wameeleza chanzo cha mbunge wa jimbo la Geita, Bw. Ernest Mabina kuzomezwa mbele ya Waziri Mkuu hivi karibuni kuwa ni mbunge huyo kutowajibika kwa wapiga kura wake.
Baadhi ya wazee hao walidai kuwa walitaka kumkabidhi mbunge huyo kwa Waziri Mkuu Bw. Edward Lowassa, aondoke naye siku hiyo kwa madai kuwa yeye ni mbunge wa Dar es Salaam na siyo Geita anaandika Renatus Masuguliko wa PST, Geita�.
Walisema mbunge huyo haonekani jimboni mpaka wakati wa ziara za viongozi.
Walisema wapiga kura wake wamekuwa kama yatima kwa sababu tangu achaguliwe hajakutana nao.
Tuhuma hizo zilitolewa na baadhi ya wazee wa CCM katika kikao chao kilichofanyika kwenye jengo la CCM wilayani siku ya Jumatano wiki hii.
Kikao hicho kiliwashirikisha wazee zaidi 70 wakiwemo viongozi wa mashina.
Kikao hicho�kiliitishwa na Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Geita, Bw. John Chenge Luhemeja kwa lengo la kutafuta kiini cha kuzomewa kwa mbunge wa Geita mbele ya Waziri Lowassa katika mkutano wa hadhara uliofanyika mjini hapa mwezi uliopita.
Habari zaidi kutoka ndani ya kikao hicho, zimedai kuwa baadhi ya wazee walidai mbunge huyo anawabagua wanachama wakiwemo wazee na vijana katika makundi na wengine kuonekana bora na kwamba bila wao hakuna CCM.
`Tunashangaa baadhi ya wazee wamekuwa wakibaguliwa na wengine wachache kupewa kipaumbele�kwa maslahi binafsi,�bila kujali matokeo yake na wengi wetu tumekuwa tunabaguliwa kutokana na kuwa na msimamo wa kusema ukweli,` alidai mzee Michael Makongoro.
Mwezi uliopita mamia ya wananchi walimzomea mbunge huyo, Mabina, mbele ya Waziri Lowassa pale alipotambulishwa na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi,� Bi. Margaret Sitta, kwenye mkutano wa hadhara wakati wa ziara ya Bw. Lowassa.
Jitihada za kumpata Bw. Mabina kuzungumzia suala hilo hazikuzaa matunda kwa kuwa simu yake ya kiganjani ilikuwa imezimwa.
* SOURCE: Nipashe