Arusha: Mzee Iddi Maganga abomoa nyumba zake mbili(200M) baada ya wanawe kuacha kufanya kazi na kusubiri urithi

Replica

JF-Expert Member
Aug 28, 2017
1,444
7,808
Mkazi wa Ngarenaro, Mzee Iddi Maganga amebomoa nyumba zake mbili zenye thamani ya milioni 200 akiwatuhumu watoto wake kumfanyia ndivyo sivyo.

Akiongea kwa uchungu, Mzee Maganga amesema mmoja wa watoto wake anayeitwa Abdallah alimfungia kwenye chumba chenye giza wiki nzima bila chakula mpaka kufikia kula kinyesi chake. Mzee Maganga amesema aliokolewa na mtoto wake wa kike baada ya kutomuona muda mrefu.

Mzee Maganga amebomoa nyumba zake na kuwataka watoto wake wakafanye kazi badala ya kukaa wakimendea urithi.

 
Unamfungia Baba yako ndani kwenye chumba cha giza wiki nzima bila chakula ili afe urithi Nyumba!

Watu wanatafuta ili walee wazazi wao, wengine wanataka kuua wazazi wao ili warithi Nyumba ya mzazi wao!

Mzee Idd ametumia maamuzi ya haraka sana, kwanza angefungua kesi ya watoto wake kujaribu kumuua kwa kumfungia ndani wiki nzima bila chakula, halafu angeweka sawa mambo yake ya mirathi, watoto kuanza kugombea mali za mzazi huku akiwa hai ni dalili ya kujikatia tamaa mapema kutafuta vyao.
 
Mzee anatunzwa na mtoto wake wa kike, ambaye mume wake ni askari Polisi alimshawishi wakamuibe mzee nyumbani kwake awe anamtunza, akaanza kupanda mbegu ya tuuze nyumba tukununulie shamba tukujengee huko, mzee akakubali, nyumba imeuzwa kwa 160 mil aliyevunja ni aliyenunua eneo na sio mzee.
(Hii ndio habari kamili toka kwa walio karibu na huyo mzee)
 
Back
Top Bottom