Kirchhoff
JF-Expert Member
- Nov 4, 2010
- 5,365
- 7,606
Siku ya Jumamosi wiki iliyopita majira ya saa 10:30 jioni uligunduliwa mwili wa kijana Agel katika kiwanja cha bwana mmoja mtaani hapa ambapo uchunguzi wa awali ilibaini kuwa kifo chake kilitokea mida ya saa saba baada ya kipigo tukuka toka kwa walinzi wa mtaa.
Inasemekana kuwa Mwenyekiti huyo aliwakamata vijana hao baada ya kupata habari ya wizi uliofanyika kwa mama mmoja (jina linahifadhiwa). Mama huyo aliibiwa kuku na deki.
Inatonywa zaidi kuwa mwenyekiti alipowaona vijana wawili Agel na mwenzake (bado sijapata jina lake) na kwakuwa vijana hao wanajulikana kwa tabia yao ya wizi, aliwakamata na kuanza kuwachapa kisha kuwakabidhi kwa vijana wawili ambao hulipwa na serikali ya mtaa kwa ajili ya doria usiku. Vijana hao wanadaiwa kumpiga kijana Agel hadi kupelekea mauti yake.
Mjomba wa kijana Agel ambaye pia amewahi kuwa DC huko Rombo ndo amechukua jukumu la kufuatilia kifo cha mpwa wake hali iliyosababisha mwenyekiti huyo wa mtaa wa Suye kupitia CHADEMA kuwa katika wakati mgumu.
Kisa na Mkasa.
Mwananchi wa Suye Oloirien Arusha