Arusha: Mwenyekiti wa Mtaa wa Suye Kata ya Oloirien Mbaroni kwa kuhusika na mauaji ya mtuhumiwa wa wizi

Kirchhoff

JF-Expert Member
Nov 4, 2010
5,340
7,557
Siku ya Jumamosi wiki iliyopita majira ya saa 10:30 jioni uligunduliwa mwili wa kijana Agel katika kiwanja cha bwana mmoja mtaani hapa ambapo uchunguzi wa awali ilibaini kuwa kifo chake kilitokea mida ya saa saba baada ya kipigo tukuka toka kwa walinzi wa mtaa.

Inasemekana kuwa Mwenyekiti huyo aliwakamata vijana hao baada ya kupata habari ya wizi uliofanyika kwa mama mmoja (jina linahifadhiwa). Mama huyo aliibiwa kuku na deki.

Inatonywa zaidi kuwa mwenyekiti alipowaona vijana wawili Agel na mwenzake (bado sijapata jina lake) na kwakuwa vijana hao wanajulikana kwa tabia yao ya wizi, aliwakamata na kuanza kuwachapa kisha kuwakabidhi kwa vijana wawili ambao hulipwa na serikali ya mtaa kwa ajili ya doria usiku. Vijana hao wanadaiwa kumpiga kijana Agel hadi kupelekea mauti yake.

Mjomba wa kijana Agel ambaye pia amewahi kuwa DC huko Rombo ndo amechukua jukumu la kufuatilia kifo cha mpwa wake hali iliyosababisha mwenyekiti huyo wa mtaa wa Suye kupitia CHADEMA kuwa katika wakati mgumu.

Kisa na Mkasa.
Mwananchi wa Suye Oloirien Arusha
 
Hakuna jinsi kama huyo agel aliamua kuwa kibaka lazima mwisho wake ulikuwa mbaya tu,Sema pia kujichukulia sheria mkononi si vizuri.
 
Makarai hayaonekani kwenye uzi huu...Mwenyekiti hajui utawala wa Sheria??
Hii ndio gharama ya kuchagua wahuni na kuwapa vyeo.
 
Makarai hayaonekani kwenye uzi huu...Mwenyekiti hajui utawala wa Sheria??
Hii ndio gharama ya kuchagua wahuni na kuwapa vyeo.
Yaani we nae kweli ni jinga lao ccm msha uwa wangap? Kaa kmya kilakitu siasa sizani ata kama unadini wewe.
 
Yaani we nae kweli ni jinga lao ccm msha uwa wangap? Kaa kmya kilakitu siasa sizani ata kama unadini wewe.
Kwa hiyo kama CCM imeua na nyie lazima muue?
Hayo mawazo yako ni ya dini gani?
 
Makarai hayaonekani kwenye uzi huu...Mwenyekiti hajui utawala wa Sheria??
Hii ndio gharama ya kuchagua wahuni na kuwapa vyeo.
wee ngojea tu uliwe timing baada ya kukabidhiwa buku 7 wakushushie mkongoto wa nguvu wakunyofoe ulimi Na kupooza mikono yako.
 
wee ngojea tu uliwe timing baada ya kukabidhiwa buku 7 wakushushie mkongoto wa nguvu wakunyofoe ulimi Na kupooza mikono yako.
Vibaka nishakutana nao sana Ila approach ya mwenyekiti sio sahihi...sheria zipo wazi na ziliwekwa kwa ajili ya hawa hawa vibaka.
Kama mwenyekiti anatakiwa kusimamia sheria mtaani kwake na sio kuzivunja
 
Hiki chama kina watu wa ajabu sana nakumbuka kipindi kile walivyojilipua pale arusha.
 
kifo cha uyo kijana kimesababishwa...Ccm na serikali yake ...maana...ugumu wa maisha ndo umenfanya aibe...kwaiyo ...mwenyekit hana kosa.
 
Vibaka nishakutana nao sana Ila approach ya mwenyekiti sio sahihi...sheria zipo wazi na ziliwekwa kwa ajili ya hawa hawa vibaka.
Kama mwenyekiti anatakiwa kusimamia sheria mtaani kwake na sio kuzivunja
Tulia wewee
 
Back
Top Bottom