ARUSHA: Mtoto akutwa amekufa kando ya nyumba akiwa kanyofolewa sehemu za siri, miguu na mikono

Jembe Jembe

JF-Expert Member
Jun 9, 2016
749
1,797
Mtoto mwenye umri unaokadiriwa kuwa na miezi mitatu amekutwa amekufa kando ya nyumba kwenye migomba huku sehemu ya viungo vyake zikiwemo sehemu za siri vikiwa vimenyofolewa.

Tukio hilo la kusikitisha limetokea mapema leo katika mtaa wa Lolovoni kata ya Sokoni 1,jijini Arusha baada ya mwili huo ambao jinsia yake halikufanyika mara moja kukutwa majira ya saa mbili asubuhi katika nyumba ya mkazi mmoja wa eneo Hilo.

Mwenyekiti wa mtaa huo,Orgeness Lema amethibitisha tukio hilo na kueleza kuwa tukio hilo ni mwendelezo wa matukio ya ukatili kwa watoto yanayofanywa na watu wasio na hofu ya Mungu.

"Nilipigiwa simu nikiwa Kanisani na kufika eneo la tukio nimeshuhudia mwili wa mtoto ukiwa kwenye migomba kando ya nyumba ya mkazi wa eneo hili ukiwa hauna miguu yote na mikono na sehemu za Siri pia zikiwa hazipo nilitoa taarifa polisi ambao walifika na kuuchukua mwili huo "alisema Mwenyekiti

Aidha amesema kuwa Serikali ya mtaa kwa kushirikiana na wananchi imeanza msako wa nyumba kwa nyumba ili kubaini nani amejifungua mtoto hivi karibuni na kwa sasa hana mtoto .

Naye balozi wa nyumba kumi katika mtaa huo,Omari Shedafa alisema kuwa alishuhudia mwili wa mtoto huyo akiwa uchi wa mnyama huku mikono na miguu pamoja na sehemu zake za Siri zikiwa zimenyofolewa .

Naye Bibi mwenye nyumba ambayo mwili wa mtoto huyo umekutwa kando ya nyumba yake , Magdalena Shaushi Mkazi wa mtaa wa Lolovono alipata taarifa kwa watoto waliokuwa wakocheza kwenye migomba yake na alipofika alishuhudia mwili wa mtoto huyo na kutoa taarifa kwa balozi.

"Mimi nimeambiwa na watoto waliokuwa wakocheza kuwa Kuna mtoto ametupwa na nilipofika nimekuta mwili wa huyu mtoto akiwa Hana miguu na mikono Sasa sijui ni Nani amemtupa hapa kwenye nyumba yangu"alisema Bibi huyo.

Baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo akiwemo mjumbe wa serikali ya mtaa huo ,John Mchasu amewataka wananchi kushirikiana kubaini aliyehusika na unyama huu ili aweze kuchukulia hatua kwani kitendo hiki hakikubaliki.

"Ninachowaomba wananchi washirikiane na viongozi wa mtaa huu ili kufanya msako wa kuwez kubaini aliyehusika na kitendo hiki "alisema Mchasu

Mwili huo imehifadhiwa katika hospitali ya Mkoa Mount Meru kusubiri taratibu zingine za kiuchunguzi

12.jpg

Ends..
 
Changamoto za maisha zinawafanya watu kuwa WEHu ,sasa sehemu za siri za mtoto mdogo ndio zitakupa UTAJIRI?
 
Ujinga unaopelekea umasikini na kukosa elimu.

Mbona USA au UK na Australia hakuna mambo kama haya?

Ona sasa!
 
Back
Top Bottom