Arusha: Mtekaji wa watoto afariki dunia kwa kupigwa risasi wakati akijaribu kutoroka

Nimejiuliza maswali mengi yenye maumivu makali moyoni, huyu kijana bado ni mdogo alianzaje kuteka watoto, alifikiria nini, ninii hasa cha kuchukua vitu visivyo na hatia na kuvidumbukiza kwenye shimo la choo ni machungu gani waliyoyapata hao watoto kwa kukosa msaada mpaka kufa, waliliaje, yeye nini kilichomfanya afanye hayo kweli hii ni dunia pole kwa wazazi wa hivyo viumbe mungu awatie nguvu
 



View attachment 583247
Mtuhumiwa Samson Petro ambaye ndie mtekaji na muuji wa watoto wawili Maureen na Ikram amefariki dunia kwa kupigwa na risasi wakati akitaka kutoroka mikononi mwa Polisi jijini Arusha.

Mtuhumiwa alipigwa risasi mbili za miguu wakati akijaribu kutoroka na ndipo alipofariki dunia akiwa hospital ya Mount Meru.

Hapo awali Usiku wa tarehe 2 Septemba kijana mwenye umri wa miaka 18, Samson Petro alishikiliwa na polisi kwa tuhuma za kuteka watoto katika mkoa wa Arusha na Geita.

Kamanda wa Polisi mkoani Geita, Mponjoli Mwabulambo alithibitisha taarifa hizo za kukamatwa kwa mtekaji huyo.

Mwabulambo alisema kuwa kijana huyo alikamatwa katika nyumba ya kulala wageni ya Shitungului iliyopo mji mdogo wa Katoro akiwa na mtoto mdogo nmwenye miaka miwili.

Alisema mtuhumiwa alimficha mtoto huyo katika chumba namba 11 cha kulala wageni iitwayo Shitungulu wakati akisubiri mpango wake wa kutaka alipwe shilingi milioni nne na wazazi wa mtoto huyo Omben Mshana na Elizabeth Ombeni.

Habari zaidi soma;.

Kukithiri kwa vitendo vya Utekaji wa watoto/kidnapping katika Jiji la Arusha

ARUSHA: Watoto wawili kati ya wanne waliokuwa wametekwa wapatikana wakiwa wamekufa

Askari wa FFU akamatwa sakata la utekaji watoto

GEITA: Mtekaji wa watoto Arusha, Geita anaswa na Polisi

Mtekaji akiri kuua watoto 2, kuwatumbukiza shimoni

Huyu hakukimbia ila aliingizwa chaka na msoja kwamba SEPA UNASUBIRI NINI
mwanya ukapatikana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapana aisee...
What if ana mtandao...?
Utajulikana vipi kama shaidi namba moja ndio marehemu tena...
Sitaki kuingilia kazi ya polisi lakini mmmmnnnnhhhhh....

Ametuachia maswali kwa kifo chake ambayo ni yeye tu angeweza kuyajibu...
What if majibu yashapatikana?
 
Hapana aisee...
What if ana mtandao...?
Utajulikana vipi kama shaidi namba moja ndio marehemu tena...
Sitaki kuingilia kazi ya polisi lakini mmmmnnnnhhhhh....

Ametuachia maswali kwa kifo chake ambayo ni yeye tu angeweza kuyajibu...
mpaka wanamtoa roho tayari washamhoji zaidi ya ujuavyo
 
Back
Top Bottom