Gerad2008
JF-Expert Member
- Jun 9, 2009
- 583
- 287
Msaidizi wa mwenyekiti wa mtaa wa Moshono Kaskazini katika kata ya Moivaro iliyopo jijini Arusha siku ya jumamosi saa nne asubuhi alishambuliwa kwa fimbo na kijana ajulikanaye kama Riziki Lotha Mollel. M/mwenye kiti huyo ajulikanaye kama Prudence Muki alikwenda nyumbani kwa Riziki Mollel kumtambulisha karani wa mahakama katika zoeoi la kumkabidhi hati za mashataka mengine yaliyokuwa yanamkabili.
Ghafla Riziki baada ya kumwona mwenyekiti huyo aliingia ndani na kutoka na fimbo na kuanza kumshambulia mwenyekiti na kusababisha karani huyo kukimbia kuokoa maisha yake had majirani walipojitokeza na kumsaidia mwenyekiti asiendelee kupata kipigo. Mwenyekiti alipata majeraha mikononi ,kichwani na aliweza kufika hospitali na kupatiwa matibabu .
Polisi walipewa taarifa lakini hadi Jumapili jioni riziki alikuwa hajakamatwa bado.
Tunaomba jeshi la polisi limtafute huyu kijana hatari kwani ametangaza lazima aue mtu na majirani haswa wasio na uhusiano mzuri naye hawana amani.