G Sam
JF-Expert Member
- Apr 20, 2013
- 11,555
- 35,880
Mgombea urais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chadema ndugu Edward Lowassa anayeungwa mkono na vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA ) kesho anatarajiwa kulisimamisha jiji la Arusha, imethibitishwa.
Mashabiki wa Edward Lowassa, Chadema na UKAWA kwa jumla wanatarajiwa kusababisha shughuli muhimu ndani ya jiji hilo kusimama kwa takribani saa nane huku shamrashamra kubwa na hamasa zikiwa zimetanda kila kona ya mji huu leo jioni.
Aidha baada ya mkutano huo, mgombea huyo wa urais anayetoa wasiwasi mkubwa ndani ya kambi ya CCM anatarajiwa kuutikisa mji wa Moshi siku ya ijumaa ambapo ataivunja rekodi iliyowekwa na Willbrod Slaa mwaka 2010 wakati akiwa Moshi mjini uwanja wa mashujaa ambapo rekodi hiyo haijawahi kuvunjwa hadi anapoingia mgombea huyo wa Chadema anayeungwa mkono na wananchi walio wengi ambao wanataka mabadiliko.