Arusha, Moshi kutikisika. Ujio wa Lowassa kuleta kitimtim

G Sam

JF-Expert Member
Apr 20, 2013
11,555
35,880
Mgombea urais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chadema ndugu Edward Lowassa anayeungwa mkono na vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA ) kesho anatarajiwa kulisimamisha jiji la Arusha, imethibitishwa.

Mashabiki wa Edward Lowassa, Chadema na UKAWA kwa jumla wanatarajiwa kusababisha shughuli muhimu ndani ya jiji hilo kusimama kwa takribani saa nane huku shamrashamra kubwa na hamasa zikiwa zimetanda kila kona ya mji huu leo jioni.

Aidha baada ya mkutano huo, mgombea huyo wa urais anayetoa wasiwasi mkubwa ndani ya kambi ya CCM anatarajiwa kuutikisa mji wa Moshi siku ya ijumaa ambapo ataivunja rekodi iliyowekwa na Willbrod Slaa mwaka 2010 wakati akiwa Moshi mjini uwanja wa mashujaa ambapo rekodi hiyo haijawahi kuvunjwa hadi anapoingia mgombea huyo wa Chadema anayeungwa mkono na wananchi walio wengi ambao wanataka mabadiliko.
 
Magufuli kwa kweli ana wakati mgumu sana. Akisha maliza senema zake Mzee wa kazi anaingia kuweka sera za maana. Subiri Kesho Usikie muziki wake.!!
 
Magufuli kwa kweli ana wakati mgumu sana. Akisha maliza senema zake Mzee wa kazi anaingia kuweka sera za maana. Subiri Kesho Usikie muziki wake.!!
WAKIWA leo naona mkutano wa Magufuli umewaumiza kwelikweli
 
Sina shaka na hili.........Lowasa hakamatiki, kulw Chato pamoja na kuwa Magufuli anatokea huko na mji ulisimama, hiyo kesho nasubiri nini kitafuata.
 
sisiem wanachukia sana ukitumia neno delete-kinana akiwa mwanza kaomba msamaha wananchi kaahidi ccm itabadilika
 
Tunamsubiri kwa hamu! Hapatatosha hakuna kusomba watu wala nini! Watu wanajichanga wenyewe
 
Hata pale lumumba wanajua kuwa mwaka huu kwa mara ya kwanza hata wakiiba hazitatosha wamejiandaa kuwa chama cha upinzani
 
Kazi ya tingatinga si inajulkana ni kusafsha njia na kufunika mabonde!! Ili mzee mwenye mji apite mahali Safi...sasa kazi hyo ishafanywa rais ndio atapita sasa..mafsiem yote yatapagawa!!!
 
Kesho Arusha itasimama bila magari ya mizigo kwenda stand rais anayesubiriwa kuapishwa akiutubia taifa na wakazi Wa Arusha
 
haa haa kazi ipo. chondechonde viongozi wa UKAWA hakikisheni mkutano wa ukawa wa kesho uonyeshwe LIVE ni muhimu kwelikweli. hasa kipindu hiki cha kuelekea mwisho wa kampeni.msituangushe sisi wengine tuliopo mbali na arusha...
 
ngosha! ngosha! mwanaume n mtu ambae anajiamn muda wote na aNAWEZA KUSIMAMA PEKE AKE BILA KUSAIDIWA KWENYE MAMBO MUHM xaxa kama kampen 2 mpaka usaidiwe na wasanii
 
Back
Top Bottom