ARUSHA: Mmiliki wa shule awaburuza Kortini wazazi wasiolipa ada, akamata mali zao

Waziri2025

Senior Member
Sep 2, 2019
148
379
Wazazi wanaosomesha watoto wao katika shule binafsi ya msingi ya Geen Pasture iliyopo katika halmashauri ya Arusha, wilaya ya Arumeru ,mkoani hapa,wamemlalamikia mmiliki wa shule hiyo kwa kukamata samani za ndani baada ya kushindwa kulipa ada za watoto wao.

Wazazi hao wameiomba serikali kuingilia kati kutokana na vitendo vya udhalilishaji vinavyifanywa na mmiliki wa shule hiyo .

Mmoja ya wazazi hao,Nembrisi Mollel, Mkazi wa Sekei ,alisema kuwa mmiliki wa shule hiyo aliyemtaja kwa jina la Julius Mathew, amefikia hatua ya kuwanyang'anya zamani za ndani kwa kisingizio kuwa ni amri ya mahakama ili kufidia deni lake jambo ambalo ni kinyume cha sheria.

Kwa mujibu wa maelezo ya Nembrisi, alikiri kudaiwa kiasi cha sh,630,000 ambayo ni ada ya mtoto wake aliyekuwa akisoma katika shule hiyo kati ya mwaka 2020/21.

"Mimi ninachoshangaa ni kufuatwa na askari polisi wenye silaha wakitaka kuchukua vyombo vya ndani bila kufuata taratibu za kisheria ikiwemo kuonana na uongozi wa kijiji au balozi ,kubandika matangazo yenye kusudio la kuchukua mali za mdaiwa "alisema

Aliongeza kuwa mmiliki wa shule hiyo amekuwa akitumia fedha nyingi kuwarubuni polisi ili kuwadhalilisha wazazi wanaodaiwa kwa kuwafuata majumbani wakitumia gari la polisi wilayani humo bila hata kuwa na notisi ya mahakama wakitishia kuchukua vyombo vya ndani.

"Jana lilikuja gari la polisi aina ya Land rover limejaa askari wenye silaha wakinitaka niondoke wachukue vyombo au nilipe fedha niliamua kuondoka na kuwachia nyumba kilichoendelea hapo nyumbani sikujua ila walikaa kwa muda wakishauriana na baadaye waliondoka"alisema.

Alisema watu hao walimshinikiza alipe deni la shule na usumbufu kiasi cha sh,milioni 1.3 jambo ambalo alishindwa kukubaliana nao kwa kuwa deni analotambua ni sh,630,000 tu.

Akiongelea tuhuma hizo mmiliki wa shule hiyo,Julius Mathew alisema kuwa uongozi qa shule hiyo uliamua kuwapeleke mahakamani wazazi 18 baada ya kushindwa kuwalipia ada watoto wao wakati wanasoma shule ya msingi na wengine walimaliza masomo na kuondoka.

Alisema uongozi wa shule hiyo unadai kiasi cha zaidi ya sh, milioni 14 zilizotokana na malimbikizo ya ada ambayo baadhi ya wazazi wameshindwa kulipa.

"Mimi niliamua kuwafikisha katika mahakama ya mwanzo ya Enaboishu baada ya jitihada mbalimbali za awali ikiwemo kutumia mabalozi,ofisi ya mtendaji wa kijiji kushindikana.

Aliwatuhumu baadhi ya wazazi kwa ujeuri na kukaidi kulipa licha ya mahakama hiyo kuamuru watoe walau kidogo kidogo lakini baadhi yao hata hicho kidogo wameshindwa kulipa jambo ambalo linakwamisha ushtawi wa shule hiyo.

"Mimi nipo tayari wanilipe hata kidogo kidogo ila mahakama iliniamuru nikamate mali zao ikiwemo vyombo lakini nimekosa msaada wa viongozi wa kijiji hicho ndio maana zoezi hili linakwama"alisema.

Alipoulizwa iwapo mahakama ya mwanzo inauwezo wa kutoa kibali cha mtu kukamatiwa mali zake ,alisema haina uwezo ila inaweza kuiomba mahakama ya wilaya ikatoa kibali jambo ambalo alishindwa kufafanua kama mahakama ya wilaya imempatia kibali za kukamata mali za mdaiwa ikiwemo kuweka matangazo kama sheria inavyosema.

Ends..
 
Wazazi wanaosomesha watoto wao katika shule binafsi ya msingi ya Geen Pasture iliyopo katika halmashauri ya Arusha, wilaya ya Arumeru ,mkoani hapa,wamemlalamikia mmiliki wa shule hiyo kwa kukamata samani za ndani baada ya kushindwa kulipa ada za watoto wao.
Kwa hiyo mnataka shule itoe elimu kwa mkopo? Shule za bure mnazijua, mnalazimisha kusomesha msikokuweza! Somesha mtoto kwa urefu wa kamba yako!
 
Tatizo ni baadhi ya watu kupenda mambo makubwa ambayo hawana uwezo nayo, wajitahidi kulipa hiyo kidogo kidogo mpaka wamalize madeni yao.
 
Tatizo la kufosi kujikuna mkono usipofika ndiyo huko😂😂..pole zao aisee
 
Wazazi wanaosomesha watoto wao katika shule binafsi ya msingi ya Geen Pasture iliyopo katika halmashauri ya Arusha, wilaya ya Arumeru ,mkoani hapa,wamemlalamikia mmiliki wa shule hiyo kwa kukamata samani za ndani baada ya kushindwa kulipa ada za watoto wao.
Wajinga sana hso wazazi unapeleka watoto shuleni halafu hutaki kulipa.
Unategemea nini?
Hapana kucheka na nyani
!
 
Mabilionea wa Arusha hao 😀😀😀 ubabe ubabe tu

Ada inafuatiliwa kama marejesho 😆 hii ni mupyaaa
 
Wazazi wanaosomesha watoto wao katika shule binafsi ya msingi ya Geen Pasture iliyopo katika halmashauri ya Arusha, wilaya ya Arumeru ,mkoani hapa,wamemlalamikia mmiliki wa shule hiyo kwa kukamata samani za ndani baada ya kushindwa kulipa ada za watoto wao.
Si Arusha huwa wanajifanya ni mji wa matajiri, imekuwaje MTU anakosa shg 630,000/= mpaka anaukimbia mji ! Poleni sana akina Molleli.
 
TATIZO ni Ile tabia ya kumuiga flani, au kushindana na flani kusomesha Mtoto shule hizo, Bila kufahamu hasa chanzo Cha MAPATO Cha unayemuiga!
Matokeo yake kuingia kwenye madeni nk.
Angalizo:sisemi tusisomeshe watoto, ila tusomeshe Kwa uwezo sio kufuata mkumbo
 
SAFI.

ningekua mkuu wa hiyo shule ningeandaa party wakati shule zimefunguliwa nika iita

OPENING SCHOOL PARTY WITH PARENTS

Siku ya sherehe najua kila mzazi atakuja na mwanae na magari yao ya kifahari,wakiingia Getini muda wa kutoka ukifika wanatoka kwa kuonyesha risiti ya ADA usie na risiti ya ADA gari inabaki ndani ya shule ukatafute ADA.

Watu wanahangaika usajili wa shule,wanahangaika kukopa wafungue shule nzuri leo hii mnaleta watoto wenu mnakuta shule inavutia halafu ADA kutoa mpaka muanze tekenywa tekenywa,

Nimemkubali sana huyo mkuu wa shule.
 
Wazo zuri. Sema unakuta mzazi hata pkpk tu hana. Uingie hasara ya kuandaa party na pesa usipate.
 
Back
Top Bottom