Arusha: Mkurugenzi wa Kampuni ya OBC ashindwa kufika Mahakamani akihojiwa na TAKUKURU

Jembe Jembe

JF-Expert Member
Jun 9, 2016
749
1,797
MKURUGENZI wa kampuni ya Uwindaji ya Oterlo Businness Coperation (OBC), Isack Lesian Mollel (59) jana ameshindwa kufika Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha katika kesi yake ya kuajiri raia wa kigeni, sababu ya kuhojiwa na Taasisi
ya kuzuia na kupambana na Rushwa(TAKUKURU), kwa kile kinachodaiwa ni matumizi mabaya ya Madaraka.

Mbele ya Hakimu Niku Mwakatobe wa Mahakama hiyo, Wakili wa Sserikali Maritenus Marandu alidai mshitakiwa huyo hajafika Mahakamani hapo
sababu yupo chini ya ulinzi wa TAKUKURU akihojiwa

Mapema wiki mbili zilizopita, Mollel alikamatwa na kusomewa makosa kumi Makamani hapo, likiwemo la kuajiri raia wa kigeni kinyume cha sheria za kazi nchini, katika kesi ya jinai namba 1/2019.

Mshtakiwa huyo aliyekuwa akitetewa na mawakili watatu ambao ni Daud Haraka akisaidiana na Goodluck Peter pamoja na Method Kimomogoro alikana mashataka yote 10 na kupata dhamana.

Kabla ya mshitakiwa huyo kufikishwa Mahakamani hapo siku mbili kabla, Waziri wa Mambo ya ndani ya nchi,Kangi Lugola akiwa mkoani hapa, alimwagiza Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani hapa, Longinus Tibushumbwamu, kuhakikisha anamsaka popote alipo baada ya kutopatikana kwa muda mrefu, ili amfikishe kwenye vyombo vya sheria na kujibu makosa yanayomkabili.

IMG-20190215-WA0008.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Aisee siwezi kuandika hapa. Huu mgogoro umeanza tangu Ndolanga wa TFF akiwa maliasili. Watu wamekufa kwa ajili ya huu mgogoro wakiwemo waandishi wa habari. Nakushauri ukapekue makrasha usome. Siwezi mm kuandika kila kitu hapa.
OK. But kutoa shuhuda juu ya jambo kwa maneno ya kusikia ni hatari sana. Ni vizuri kufanya utafiti wako mwenyewe.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom