Arusha: Mke wa Mtu auawa na mchepuko wake baada ya kutoa mimba ya mchepuko

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,500
9,279
622d0291c01bc3e7f561d6ff12538bc2

MWILI wa mwanamke aliyetambulika kwa jina la Teddy Mallya mkazi wa Ilboru Kisiwani, Arumeru mkoani Arusha umekutwa umetupwa kwenye shamba la migomba akiwa mtupu na baadhi ya majeraha mwilini ikiwemo ya kung’atwa na meno huku akidaiwa kuuawa na hawara yake (mchepuko).

Mwili huo ulipatikana jana majira ya saa 2:30 asubuhi baada ya wapita njia kuuona na kutoa taarifa. Taarifa za wakazi wa eneo hilo wanadai kuwa marehemu alikua na uhusiano wa siri na mwanaume nje ya ndoa ambaye anadaiwa kutekeleza mauaji hayo kutokana na kumtuhumu marehemu kuwa alitoa ujauzito wake.

Mume wa marehemu, Richard Lanyuni alisema mkewe alikuwa mfanyabiashara wa pombe za kienyeji aina ya mbege, hakuonekana kurejea nyumbani muda wa kawaida na ilipotimu majira ya saa saba usiku niliamua kulala ndipo kesho yake alipata taarifa za kuuawa.

“Kuhusu mke wangu kuwa na uhusiano na mwanaume huyo siwezi kujua ila hakuwa na ujauzito. Naomba vipimo vya kitaalamu vifanyike kujua kama kweli alikuwa na ujauzito maana ana shughuli zake mimi siwezi kumchunguza sana,” alisema Richard.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Justin Masejo alisema jeshi linamshikilia mwanaume mmoja kwa tuhuma za kumuua mwanamke huyo, na kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na mwenyekiti wamtaa wa Ilkiroriki, Emmanuel Lazaro, mtuhumiwa anadaiwa kuwa na mahusiano ya kimapenzi na marehemu na alikamatwa kutokana na baadhi ya nguo zake na viatu kukutwa eneo la tukio.
 
Ila hata hayo maelezo ya Mume yanatia mashaka. Kwamba alimsubiri mpaka saa 7 akaona hajarudi akaamua kulala?

Kwamba hakujishughulisha kumchunguza kwa kuwa mke ana shughuli zake?

Afu Mtuhumiwa amekamatwa kwa sababu Vitu vyake vimekutwa eneo la tukio?

Anyway, RIP Teddy Mallya..
 
TUKIO HILI LINGEFANYWA NA MUME, WATETEZI WA HAKI ZA MWANAMKE NA USAWA HIVI SASA WANGEISHA TOA MATAMKO HUKU MISHIPA YOTE IMEWASIMAMA.
SASA TUKIO HILI KAFANYA MCHEPUKO WATETEZI MCHONGO WAKO KIMYAAAAA
 
Aisee daah imenihuzunisha sana. Huyo mshenzi ahasiwe. Yaani uibe mali ya mtu na bado ulete wivu ukamuua kabisa. Shenzi sana wakamfirimbe.
Mkuu tisilaumu sana asilimia 80 tunaishi na wanawake ammbao sio our real rib.
Mwanamke yeyote hata kama hakupendi we tangaza tu ndoa yani yuko tayari muda huohuo.

Matatizo ya ndoa huanzia hapo hasa akikutana na mwenye huo ubavu.

Hataangalia ndoa tena.
 
622d0291c01bc3e7f561d6ff12538bc2

MWILI wa mwanamke aliyetambulika kwa jina la Teddy Mallya mkazi wa Ilboru Kisiwani, Arumeru mkoani Arusha umekutwa umetupwa kwenye shamba la migomba akiwa mtupu na baadhi ya majeraha mwilini ikiwemo ya kung’atwa na meno huku akidaiwa kuuawa na hawara yake (mchepuko).

Mwili huo ulipatikana jana majira ya saa 2:30 asubuhi baada ya wapita njia kuuona na kutoa taarifa. Taarifa za wakazi wa eneo hilo wanadai kuwa marehemu alikua na uhusiano wa siri na mwanaume nje ya ndoa ambaye anadaiwa kutekeleza mauaji hayo kutokana na kumtuhumu marehemu kuwa alitoa ujauzito wake.

Mume wa marehemu, Richard Lanyuni alisema mkewe alikuwa mfanyabiashara wa pombe za kienyeji aina ya mbege, hakuonekana kurejea nyumbani muda wa kawaida na ilipotimu majira ya saa saba usiku niliamua kulala ndipo kesho yake alipata taarifa za kuuawa.

“Kuhusu mke wangu kuwa na uhusiano na mwanaume huyo siwezi kujua ila hakuwa na ujauzito. Naomba vipimo vya kitaalamu vifanyike kujua kama kweli alikuwa na ujauzito maana ana shughuli zake mimi siwezi kumchunguza sana,” alisema Richard.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Justin Masejo alisema jeshi linamshikilia mwanaume mmoja kwa tuhuma za kumuua mwanamke huyo, na kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na mwenyekiti wamtaa wa Ilkiroriki, Emmanuel Lazaro, mtuhumiwa anadaiwa kuwa na mahusiano ya kimapenzi na marehemu na alikamatwa kutokana na baadhi ya nguo zake na viatu kukutwa eneo la tukio.
Maajabu haya na dharau juu..
Mwizi/mgoni kujimilikisha mali za watu🙄
Ukiwa na mke mlevi hesabu maumivu tu. Akishalewa anageuka cha-wote !!!
 
Back
Top Bottom