Arusha- Mji wa kitalii - mji uliojaa kinyesi

Crashwise

JF-Expert Member
Oct 23, 2007
22,227
8,735
katika hali isiyo vumilika mji wa Arusha umekuwa ikubwa na upasukaji/kuziba kwa mabomba ya maji machafu( mavi) na kusababisha kero kubwa kwa wakazi wa Arusha na mbaya zaidi kila linapotokea tatizo hili huchukua siku si chini ya siku tatu kutatuliwa na maeneo sugu kabisa ni kuzunguka uwanja wa Sheikh Amri Abeid, makongoro Road na barabara ya uhuru lakini ya leo imenikera kuliko siku zote kwani ukipita barabara ya uhuru utakuta mavi siyo maji ya mavi barabarani na ukipandisha hii barabara ya sokoni karibu na Pallson Hotel napo mambo ni hovyo kabisa sasa najiuliza huu ni mji wa kitalii au mji wa mavi...
Photo-0070.jpg
hii ni mizinga ya kinyesi kama inavyoonekana karibu kabisa na soko kuu la Arusha....
 
View attachment 37097
hii ni mizinga ya kinyesi kama inavyoonekana karibu kabisa na soko kuu la Arusha....

Uliyoyasema yana ukweli, lakini ungetumia lugha ya kistaarabu.......... Wewe umeona Arusha tu Je jiji lenu la Dar umeliona?
 
Mkuu! Yani hii ni kero full,hebu zunguka na hii barabara ya kupandia stendi ya mkoani upande wa kushoto wakati unatokea hapo Jogoo House na hata mtaa wa pili wa majengo yani ni upande wa pili pale stendi yani ni full kero mtu wangu yani mabomba yanavuja na hata karibu kbs na ofisi ya maji safi na maji taka ni kero kwa wenye ofisi mtaa huo. Kwa kweli Mkuu hili siyo kitu cha kusema polepole.
 
Kwa ujumla watanzania bado hatuna elimu elekezi inayohusiana na mazingira! Utakutana na mtu ananunua ndizi anatembea huku anakula halafu baada yakumaliza anatupa maganda barabarani! mwisho wa maarifa yote nenda mkoa wa kilimanjaro pale Moshi mjini ukitupa tu hata ganda la BigGee
ukishikwa unatiwa adabu kwakupigwa faini ya sh 50'000.
 
Uliyoyasema yana ukweli, lakini ungetumia lugha ya kistaarabu.......... Wewe umeona Arusha tu Je jiji lenu la Dar umeliona?
Mimi ni mtu wa Arusha ndiyo maana nimekereka sana mbaya zaidi baada ya kuwaambia wahusika nikambulia matusi kidogo tupigane...
 
Dar je? nenda msasani m.vi yametapakaa
Tunasubiri msaada kutoka ugaibuni kutatua kero hizi....au ni hakuna uamzi wa dhati wa kushughulikia kero hizi...jiji la Arusha linapata pesa nyingi sana linashindwaje kushughulikia kero hizi
 
Ndio maana twataka katiba mpya.

Kwani katiba ndio italeta usafi wa miji yetu,...mimi nafikiri miji yetu ijifunze kuwajibika kwa wananchi,...hii ikiwa ni pamoja na sisi wananchi kwani arusha kila mahali mate yametapakaa,....na dar ndio usiseme mabomba yote hovyo_yanapasuka kila mara
 
Kwa ujumla watanzania bado hatuna elimu elekezi inayohusiana na mazingira! Utakutana na mtu ananunua ndizi anatembea huku anakula halafu baada yakumaliza anatupa maganda barabarani! mwisho wa maarifa yote nenda mkoa wa kilimanjaro pale Moshi mjini ukitupa tu hata ganda la BigGee
ukishikwa unatiwa adabu kwakupigwa faini ya sh 50'000.
Natambua umakini uliko moshi kwani mimi ni moja ya mtu nilie athirika na sheria za moshi lakini sikujuta na ilinikuta baada ya kutupa vocha...
 
Kwani katiba ndio italeta usafi wa miji yetu,...mimi nafikiri miji yetu ijifunze kuwajibika kwa wananchi,...hii ikiwa ni pamoja na sisi wananchi kwani arusha kila mahali mate yametapakaa,....na dar ndio usiseme mabomba yote hovyo_yanapasuka kila mara
Kweli kabisa mkuu sheria za miji ninavyo jua mimi hutungwa na halimashauri husika bona moshi wameweza kwanini siyo Arusha na kimapatao Arusha iko juu ya Moshi....
 
tumeshasema hatumtambui meya,hata akituwekea vinyesi milangoni kwetu tunasema njia iliyotumika kumpata si sahihi.
ndo maana tunasisitiza serikali za majimbo.hawa magamba wanachukua rasilimali za arusha wanajendea vitambi.
mi nina hasira na mtu yeyote anaevaa nguo za kijani hata yanga naanza kuichukia sasa ila siendi simba.
 
plz, plz! naomba nitofautiane nawe jamani! uchafu unachangiwa na tabia binafsi ya mtu banaa! na hao watendaji kila mtu ana hulka yake kabla ya proffessionalism! arusha miundombinu haijalemewa kiasi hicho.

Na ikitokea tatizo shurti litatuliwe. siasa interms of investment at large kwenye miundombinu. na hiyo picha it is nt flowing sewage,inaonekana kulikuwa na tatizo na likatatuliwa.ila cleanup haijafanyika (sorry,im doing a risk analysis here,lol)

wakuu hii yote inachangiwa pia na siasa....
 
Mamlaka yenye dhamana ya kukussanya kodi na kuweka mji katika hali inayostahil kwa maisha ya binadamu ni manispaa/halmashauri ya jiji la arusha.
Hawa ndio wanaotakiwa kuratibu mambo yote yahusuyo miundombinu. Kama mitaro na chambers zinavuja hovyo, kamkamateni mkurugenzi, mumuulize fedha za kodi anapeleka wapi? Na idara zake zinafanya nini?
 
tumeshasema hatumtambui meya,hata akituwekea vinyesi milangoni kwetu tunasema njia iliyotumika kumpata si sahihi.
ndo maana tunasisitiza serikali za majimbo.hawa magamba wanachukua rasilimali za arusha wanajendea vitambi.
mi nina hasira na mtu yeyote anaevaa nguo za kijani hata yanga naanza kuichukia sasa ila siendi simba.
Wewe mshitakiwa hujaenda mahakamani leo kesi yako inasomwa....
 
plz, plz! naomba nitofautiane nawe jamani! uchafu unachangiwa na tabia binafsi ya mtu banaa! na hao watendaji kila mtu ana hulka yake kabla ya proffessionalism! arusha miundombinu haijalemewa kiasi hicho. na ikitokea tatizo shurti litatuliwe. siasa interms of investment at large kwenye miundombinu. na hiyo picha it is nt flowing sewage,inaonekana kulikuwa na tatizo na likatatuliwa.ila cleanup haijafanyika (sorry,im doing a risk analysis here,lol)
<br />
<br />
Mkuu mimi huwasiongee vitu vya kubahatisha kama uko Arusha nenda uhuru road utasikilizia na tatizo hili hajaanza leo tangu jana nikategemea watalitatua badala yake leo ni mavi tu barabarani mbaya zaidi ni karibu na soko kuu...
 
Mamlaka yenye dhamana ya kukussanya kodi na kuweka mji katika hali inayostahil kwa maisha ya binadamu ni manispaa/halmashauri ya jiji la arusha.
Hawa ndio wanaotakiwa kuratibu mambo yote yahusuyo miundombinu. Kama mitaro na chambers zinavuja hovyo, kamkamateni mkurugenzi, mumuulize fedha za kodi anapeleka wapi? Na idara zake zinafanya nini?
Niliongea na wasaidizi wake wakani jibu hayani husu na matusi kibao...
 
Back
Top Bottom