Arusha: Mgombea udiwani CUF aomba kura kwa kulia

Crashwise

JF-Expert Member
Oct 23, 2007
22,227
8,735
Baada ya kuhudhuriwa na watu wasiozidi 50 mkutano wa Makamu wa Raisi kumnadi John Bayo aliefukuzwa na CHADEMA mgombea huyo(John Bayo) ameagua kilia akiwaomba wananchi wajitokeze kuja kumskiliza na tarehe 16.6 wamfute machozi kwani CHADEMA walimuonea hakuchukua rushwa kama walivyodai CHADEMA, baada ya kulia kwa muda Makamu wa rais alisimama na kuanza kumbembeleza...

cuf.JPG
Mkutano wa CUF ukiendelea
cuf2.JPG
Makamu wa rais Zanzibar akishuudia aibu.
bayo.JPG
John Bayo akilia jukwaani
MGOMBEA udiwani kata ya Elerai Jijini Arusha kwa tiketi ya Chama cha Wananchi (CUF) John Bayo, juzi aliangua kilio jukwaani wakati akijinadi na kuomba kura kwa wapiga kura wa kata hiyo.

Bayo, ambaye awali alikuwa Diwani wa kata hiyo kabla ya kufukuzwa uanachama na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),alijikuta katika hali hiyo mbele ya Katibu Mkuu wa chama hicho, Maalim Seif Sharif Hamad.

Bayo huku akitokwa na machozi, aliapa mbele ya wananchi hao kuwa hakuwahi kupokea kiasi chochote cha fedha kwa ajili ya kupatikana kwa muafaka wa Meya wa Jiji la Arusha kama ambavyo amekuwa akituhumiwa na Chadema.

"Sijala hata senti moja kuwasaliti watu wangu kwani najua kwa kufanya hivyo ni kukiuka maadili na kuwasaliti nyie mliokuwa mmenichagua. Nina imani nyie ndiyo mtanifuta machozi kwa kunipa kura zenu tena ili nikaweze kuwatetea katika halmashauri," alisema mgombea huyo.

Bayo aliwaeleza wananchi hao kuwa iwapo watampa ridhaa ya kuendelea kuwaongoza atahakikisha anashirikiana nao katika kutatua changamoto ambazo zimekuwa zikiwakabili, ikiwa ni pamoja na tatizo la michango ya madawati kwa wanafunzi wa shule ya sekondari ya Elerai.

Mgombea huyo aliwataka wapiga kura kuachana na siasa za kishabiki na badala yake kuchagua mtu atakayeweza kuwawakilisha na kuangalia maslahi ya wananchi kwanza.

Wakati huo huo, Katibu Mkuu wa chama hicho, Maalim Seif awali akimnadi mgombea huyo aliwaomba wananchi kumchagua Bayo kutokana na kuwa CUF ni chama ambacho kimekuwa kikisisitiza juu ya amani na kuwataka wapiga kura hao kuzingatia mambo mawili katika uchaguzi na siyo kukurupuka kuchagua viongozi.

HabariLeo
CHADEMA wakikamua jukwaani huku CUF wakilia jukwaani
chadema.JPG
 
Attachments

  • chadema1.JPG
    chadema1.JPG
    121 KB · Views: 522
Hapo hata kama ni mimi lazima nilie,wewe mpaka Mzee sawasawa anakuja kukupigia debe na watu hawataki kuja kusikiliza? Uwepo wa Maalim tuu pekee ilikuwa sababu za kuleta mvuto maana huyo ni Makamu wa Rais 'mkoani' Zanzibar lakini watu wa Arusha walivyo wagumu wamepotezea. Na kama viongozi wenzangu wasiponiunga mkono kwa kilio najitoa.
 
Maalim amesema Lpmba nae atakja saasijui atakuja kuwaambia nini wana elerai juu ya udini wake na kikwete

Walivyo wachovu wa kufikiri hadi sasa hawajatoa tamko lolote la maana kuweka mambo sawa!....wanaona sawa tu..
Mtu mwenye akili kati ya Lipumba au Wa Msoga angesimama hadharadi na kuelezea umma nini hasa ilikuwa dhamira ya Lipumba kukiri msikitini kuwa walimhujumu DR Slaa kwa kigezo cha udini!
 
MGOMBEA udiwani kata ya Elerai Jijini Arusha kwa tiketi ya Chama cha Wananchi (CUF) John Bayo, juzi aliangua kilio jukwaani wakati akijinadi na kuomba kura kwa wapiga kura wa kata hiyo.

Bayo, ambaye awali alikuwa Diwani wa kata hiyo kabla ya kufukuzwa uanachama na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),alijikuta katika hali hiyo mbele ya Katibu Mkuu wa chama hicho, Maalim Seif Sharif Hamad.

Bayo huku akitokwa na machozi, aliapa mbele ya wananchi hao kuwa hakuwahi kupokea kiasi chochote cha fedha kwa ajili ya kupatikana kwa muafaka wa Meya wa Jiji la Arusha kama ambavyo amekuwa akituhumiwa na CHADEMA.

"Sijala hata senti moja kuwasaliti watu wangu kwani najua kwa kufanya hivyo ni kukiuka maadili na kuwasaliti nyie mliokuwa mmenichagua. Nina imani nyie ndiyo mtanifuta machozi kwa kunipa kura zenu tena ili nikaweze kuwatetea katika halmashauri," alisema mgombea huyo.

Bayo aliwaeleza wananchi hao kuwa iwapo watampa ridhaa ya kuendelea kuwaongoza atahakikisha anashirikiana nao katika kutatua changamoto ambazo zimekuwa zikiwakabili, ikiwa ni pamoja na tatizo la michango ya madawati kwa wanafunzi wa shule ya sekondari ya Elerai.

Mgombea huyo aliwataka wapiga kura kuachana na siasa za kishabiki na badala yake kuchagua mtu atakayeweza kuwawakilisha na kuangalia maslahi ya wananchi kwanza.

Wakati huo huo, Katibu Mkuu wa chama hicho, Maalim Seif awali akimnadi mgombea huyo aliwaomba wananchi kumchagua Bayo kutokana na kuwa CUF ni chama ambacho kimekuwa kikisisitiza juu ya amani na kuwataka wapiga kura hao kuzingatia mambo mawili katika uchaguzi na siyo kukurupuka kuchagua viongozi.

HabariLeo
 
Walivyo wachovu wa kufikiri hadi sasa hawajatoa tamko lolote la maana kuweka mambo sawa!....wanaona sawa tu..
Mtu mwenye akili kati ya Lipumba au Wa Msoga angesimama hadharadi na kuelezea umma nini hasa ilikuwa dhamira ya Lipumba kukiri msikitini kuwa walimhujumu DR Slaa kwa kigezo cha udini!
Mkuu kitendo cha Prof. Lipumba au Kikwete na CCM yake kujibu video hiyo itaibua nyingine tena ambayo ipo kwenye ushahidi wa mbunge wa Arusha (Mhe. Godbless Lema) ambayo masheikh wanathibitisha hilo siku ikifika tutaiweka ingawa ni inatia hasira sana kwa dini nyingine na vyama vingine ambavyo havikuwepo kwenye mpngo huo haramu...
 
Bora muiweke mapema, ukweli ni ukweli tu ata kama unauma, hapa hatumjengi mtu tunajenga Tanzania yetu ya sasa na ijayo kwahiyo kama ni kweli kiongozi wa nchi alifanya kitu cha aibu alafu anakuja kujifanya kukemea udini, huyo ni mnafki namba wani. na si mbaya sana kwsababu karibia anaachia madaraka, iwekeni hiyo tuelewa unafki wa hawa watu
 
Bayo, you can fool same people sometimes, but you cannot fool all people all the time.
Kama hukuvuta mshiko, na ulikuwa na nia ya kutikkia wananchi wako kama ni kweli, mbona ulionyesha kiburi pale uliposhauriwa na viongozi wako?
Una habari kuna watu walikufa kupinga utaratibu ulio tumika kmpata meya?
Ulipo pingana na chama chako na kukbilia manispaa kwa tamaa zako, ni nani angekuwa meya wako????
 
Bayo bado hajalia vizuri, atalia inavyostahili baada ya kupata kura zenye idadi ya number ya yeboyebo.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Back
Top Bottom