Crashwise
JF-Expert Member
- Oct 23, 2007
- 22,227
- 8,735
Baada ya kuhudhuriwa na watu wasiozidi 50 mkutano wa Makamu wa Raisi kumnadi John Bayo aliefukuzwa na CHADEMA mgombea huyo(John Bayo) ameagua kilia akiwaomba wananchi wajitokeze kuja kumskiliza na tarehe 16.6 wamfute machozi kwani CHADEMA walimuonea hakuchukua rushwa kama walivyodai CHADEMA, baada ya kulia kwa muda Makamu wa rais alisimama na kuanza kumbembeleza...
Mkutano wa CUF ukiendelea
Makamu wa rais Zanzibar akishuudia aibu.
John Bayo akilia jukwaani
Mkutano wa CUF ukiendelea
Makamu wa rais Zanzibar akishuudia aibu.
John Bayo akilia jukwaani
CHADEMA wakikamua jukwaani huku CUF wakilia jukwaaniMGOMBEA udiwani kata ya Elerai Jijini Arusha kwa tiketi ya Chama cha Wananchi (CUF) John Bayo, juzi aliangua kilio jukwaani wakati akijinadi na kuomba kura kwa wapiga kura wa kata hiyo.
Bayo, ambaye awali alikuwa Diwani wa kata hiyo kabla ya kufukuzwa uanachama na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),alijikuta katika hali hiyo mbele ya Katibu Mkuu wa chama hicho, Maalim Seif Sharif Hamad.
Bayo huku akitokwa na machozi, aliapa mbele ya wananchi hao kuwa hakuwahi kupokea kiasi chochote cha fedha kwa ajili ya kupatikana kwa muafaka wa Meya wa Jiji la Arusha kama ambavyo amekuwa akituhumiwa na Chadema.
"Sijala hata senti moja kuwasaliti watu wangu kwani najua kwa kufanya hivyo ni kukiuka maadili na kuwasaliti nyie mliokuwa mmenichagua. Nina imani nyie ndiyo mtanifuta machozi kwa kunipa kura zenu tena ili nikaweze kuwatetea katika halmashauri," alisema mgombea huyo.
Bayo aliwaeleza wananchi hao kuwa iwapo watampa ridhaa ya kuendelea kuwaongoza atahakikisha anashirikiana nao katika kutatua changamoto ambazo zimekuwa zikiwakabili, ikiwa ni pamoja na tatizo la michango ya madawati kwa wanafunzi wa shule ya sekondari ya Elerai.
Mgombea huyo aliwataka wapiga kura kuachana na siasa za kishabiki na badala yake kuchagua mtu atakayeweza kuwawakilisha na kuangalia maslahi ya wananchi kwanza.
Wakati huo huo, Katibu Mkuu wa chama hicho, Maalim Seif awali akimnadi mgombea huyo aliwaomba wananchi kumchagua Bayo kutokana na kuwa CUF ni chama ambacho kimekuwa kikisisitiza juu ya amani na kuwataka wapiga kura hao kuzingatia mambo mawili katika uchaguzi na siyo kukurupuka kuchagua viongozi.
HabariLeo