Arusha. Mbunge Godbless Lema leo Jan 18 amepelekwa tena Mahakamani

Francis12

JF-Expert Member
Sep 30, 2016
7,533
22,278
Mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema na mke wake Neema Lema wamesomewa maelezo ya awali ya kusambaza ujumbe wa kuudhi kwa mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo ambapo Wakili wa serikali Alice Mtenga Ameieleza mahakama kwamba wameaandaa mashahidi watano na watakuwa na vielelezo ikiwemo simu ya Mshtakiwa.

August 20 mwaka 2016 washtakiwa wote kwa kutumia simu ya mkononi waliandika ujumbe mfupi na kuutuma kwa mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo na msg yenyewe ilikua inasema ‘Karibu tutakudhibiti kama Arabuni wanavyodhibiti Mashoga‘

Mshtakiwa ambaye ni Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema amekana tarehe ya kukamatwa na kumtumia ujumbe huo wa kuudhi mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo ambapo Wakili wa Lema, John Malya amesema wameweka pingamizi la maandishi kutokana na kuwepo kwa upungufu katika hati ya mashtaka

Hakimu anayesikiliza kesi hiyo John Baro amehairisha kesi hadi February 3 ambapo pingamilizi hilo litasikilizwa lakini pia Mbunge wa Arusha mjini Godbles Lema amesomewa shtaka la kuhamasisha watu kufanya kusanyiko lisilokuwa na kibali kupitia mtandao wa kijamii

Hakimu anayesikiliza kesi hiyo Bernard Nganga amepanga kutolea uamuzi mdogo kuhusu hoja iliyoletwa na upande wa mshtakiwa kuhusu kesi hiyo kuhamishiwa katika mahakama ya kikatiba yenye majaji watatu.
IMG-20170118-WA0019.jpg
 
Madhara ya kuteuliwa kwa lundo la Majaji wenye Sifa za kutoweza kuwa majaji sasa yanajionyesha wazi.
Katika dunia yenye Majaji (Binadam wajuzi wa Falsafa na Hekima Ya kutosha) haya yanayoendelea yasingekuwepo. Bahati mbaya sana kwa Afrika hasa Tanzania ni ukweli kuwa Baada ya Kusataafu kwa Majaji wa Kweli waliokuwa wanateuliwa na watu wenye Sifa na weredi wa kutambua wanaostahili kuteuliwa majaji kumebakwa na wateuzi ambao hawana weredi matokeo yake tutaendeelea kusoma hekima za Kijaji kutoka kwa Majirani zetu hadi pale ambapo tutapata kizazi cha wateuzi wa majaji wenye hekima na weredi.
Mahakama kwa sasa sio pahala pa kupatikana haki na wala weredi wa Mawakili hauwezi kukuhakikishia haki Mbele ya Jaji asiye na weredi wowote zaidi ya kuwa na Elimu ya sheria na kufurahisha mamlaka kuwa ndio msingi wa uteyzu wake naye hatakuwa tayari kutoautiana na mamlaka iliyofanikisha Kumfikisha pale ambapo hajawahi kuwa na ndoto wala maoni ya kupafikia.
Amani amani itawale hadi taifa litapokuja kupata viongoxi wa kweli
 
Huyu mkuu wa mkoa kajitengenezea maadui mwenyewe...siasa sio uadui alitakiwa apambane kwa hoja
 
Vumilia kamanda ipo siku coz mungu siyo magufuli kama aliwatoa wana waisiraeli toka misiri hata ww atakutoa gerezani kwa maombi ya wana arusha na wana chadema wote
 
Hilo dua lako liondoe, litamsotesha sana mwenzio.
Hili dua kwa kulinganisha hadithi ya Mungu na wana wa Israeli ni dua kimeo. Sababu hadi kupata neema na kuikanyaga nchi ya ahadi walisoteshwa jangwani kwa miaka arobaini na waliokanyaga nchi ya ahadi ni kizazi cha pili na kuendelea.
Miaka arobaini kwa kutembea umbali mfupi wa kijiografia kama kutoka Arusha kwenda Moshi. Yaani umbali huo usotee miaka 40 ndiyo ufike! Tena siyo ufike wewe! Wafike wajukuu zako na vitukuu!
"Sterling" wa hiyo hadithi (Mussa) hakuikanyaga nchi ya ahadi. Kwa majaaliwa ya M/ Mungu alioneshwa kwa njozi, kwamba ni palee nchi ya ahadi,lkn hakufika akafa.
Sasa kama ndiyo Lema unamsalia kwa kumlinganishia na hiyo hadithi ya Mussa, nashauri iondoe umemuua, maana hiyo sala ikiswihi atasota miaka nenda rudi bila kufika safari yake, ni kizazi chake ndiyo kitakachofika kwenye safari aliyoanzisha.
Chonde chonde iondoe sala hiyo, itamsotesha sana Lema.
Vumilia kamanda ipo siku coz mungu siyo magufuli kama aliwatoa wana waisiraeli toka misiri hata ww atakutoa gerezani kwa maombi ya wana arusha na wana chadema wote
 
Back
Top Bottom