Arusha: Mashahidi 9 kumkaanga Mfanyabiashara Maarufu wa Oryx na Polisi

Jembe Jembe

JF-Expert Member
Jun 9, 2016
749
1,797
Mashahidi wapatao 9 wanatarajiwa kutoa Ushahidi katika kesi ya Rushwa ya shilingi milioni 10 inayomkabili mfanyabiashara maarufu Jijini Arusha,Shabiby Virjee{34} na wenzake wawili akiwemo askari polisi.

Mbali ya mashahidi hao kutarajiwa kutoa Ushahidi huo pia Mwendesha Mashitaka wa Taasisi ya Kuzuia na Kupamba na Rushwa{TAKUKURU} Hamidu Simbano alisema kuwa vielelezo 10 vinatarajiwa kutolea katika kesi hiyo.

Kabla ya kueleza hayo,Simbano aliwasomea mashitaka watuhumiwa wote na walikana mashitaka yao mbele ya Hakimu Mkuu Mfawidhi,Martha Mahumbuga na sasa shahidi wa kwanza katika kesi hiyo anatarajiwa kutoa Ushahidi wake aprill 24 mwaka huu.

Simbano alidai mahakamani hapo kuwa Virjee , Askari polisi Pc 8683 ,Paulo Erasmo{37} na mfanyakazi wa kampuni hiyo ya mafuta ya Oryx,Nkenzi Pazi{38} desemba 18 mwaka jana wote walimshawishi Staff Sajenti Meshack Laizer kuchupokea Rushwa ya shilingi miloni 10 katika kesi anayoipeleleza inayomhusu Mkurugenzi wao Virjee.

Alisema wafanyakazi hao kwa pamoja walimtafuta pc Erasmo na kumpatia kiasi cha shilingi milioni 10 ili aweze kumkabidhi Staff Sajenti Laizer ili aweze kumwachia huru mtoto wa mfanyabiashara huyo aliyetambuliwa kwa jina la Ilphran Virjee.

Simbano alisema wafanyakazi hao walikamatwa na kikosi polisi kikiongozwa na Sajenti Laizer wakiuza mafuta nje ya Jiji la Arusha kinyume na sheria.

Mfanyabiashara huyo na wenzake wanaotetewa na mawakili maarufu Jijini Arusha Godluck Maico na Sambo Gwakisa.
 
Back
Top Bottom