Arusha: Mahakama yatupilia mbali rufaa ya mawakili wa serikali kwenye kesi ya Lema

Hawa mawakili wa Sizonje nasikia wanataka kwenda The Hague kukata rufaa tena!!

Kiukweli hii nchi imekosa dira.Hivi viongozi wetu wastaafu wanaoheshimika wako wapi kukemea huu upuuzi unaoendelea? Yaani kesi inayopaswa kukaliwa na kuamuliwa na mahakama ya mwanzo pale LUNGUYA, tena ndani ya wiki moja,inakwenda mpaka mahakama ya mwisho kiutawala? (Naamini pia iwapo kungekuwa na mwendelezo wa korti zingine hata mia huko juu hawa Jamaa wangefika,lengo ni kumfurahisha Mr Sizonje).

We have to say "NO" for this kind of stupidity.Tuna kesi za mauaji kibao zinahitaji maamuzi ya mahakama kuu na Rufaa.Zimeshindwa kuamuliwa kwa sababu ya pesa hakuna na watu wanazidi kutumikishwa kama wafungwa na mahabusu magerezani wakisubiri maamuzi ya mashauri yao.Leo majaji wa mahakama ya rufaa wanakaa kuamua suala LA dhamana ya kesi eti ya kumtukana mtu,badala ya kesi nzitonzito kama murder,ufisadi n.k?


Aliyeturoga kweli Kafa na najuta kuzaliwa Tanzania!!
 
Mawakili wa serikali wamejidhalilisha wenyewe. Kazi kutumika tu kijinga!
 
KUTOKA KWA WAKILI MSOMI KIBATALA

Mahakama ya Rufani ya Tanzania (Luanda, Kipenka, Mugasha, JJA) iliyokaa Arusha leo 27th February 2017 imetupa Rufaa zote mbili zilizofunguliwa na Serikali dhidi ya maamuzi ya Mahakama Kuu Kanda ya Arusha kuhusiana na dhamana ya Lema. Serikali ilikubali yenyewe kwamba Rufaa zote mbili hazina mashiko kisheria; kama tulivyokuwa tunasema siku zote tangu wakate Rufaa hizo.

Files sasa zitapelekwa Mahakama Kuu ili kuendelea na mambo yanayohusiana na dhamana.

Mahakama pia imezungumzia kwa masikitiko makubwa namna ambavyo Serikali imekuwa ikitumia case hii kama mbinu ya kutesa na kusumbua watu na imeshangazwa namna ofisi ya DPP ilivyoji-conduct. Imeshangazwa namna wanasheria wanavyoweza tia najisi fani kwa mbinu za ajabu ajabu mahakamani.

Imemkaripia sana DPP; in open court, too.

Kwetu sisi ni vindication kwamba we were always right. Always.

Soon safari hii itaisha.

Motto; if U know U are right, persevere and let all temporary things pass. U will eventually be vindicated.
Mods tafadhali pandisha hii kitu juu
 
Msijitie kujua sana wakati mwenzenu anaemia jela
Cha maana mshaurini afunge mdomo wake na anene mambo ya msingi ya kisiasa.
Kakaa selo miezi karibia minne kwa domo lake na kutaka kushindana na dola.

Mtahangaika sana.Sasa hivi mnatusaidia hata kufanya kampeni za TLS,hatutapoteza muda wa kufanya kampeni
 
MUNGU yupi? huyu aliyetufundisha na kutuasa kuwa na kauli njema? Na kutokuwa na kauli za kuudhi
Yule aliyemteua Musa kuwatoa Waisraeli Misri wakati alikuwa ameua mtu. Aliyempenda Mfalme Daudi wakati aliiba mke wa mtu... Mungu ni pendo kaka. Hutoa msamaha bure na sio kama binadamu anavyoangalia na kuhukumu hukumu. Hakika neema yake ni toshelevu kila wakati
Leo kesi ya mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini Godbless Jonathan Lema inaanza kusikilizwa katika mahakama ya Rufani kuhusu dhamana .
Ntajitihidi kuwaletea yanayojiri kutoka mahakamani.

Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini Godbless Jonathan Lema akiwa anawasili eneo la mahakama
View attachment 474947
Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Mhe. Freeman Mbowe akiwa ameongozana na Mbunge wa Kibamba wakiwasili katika Mahakama Kuu Mkoa wa Arusha Leo Jumatatu 27/02/2017 ikiwa leo linasikilizwa shauri la Mbunge wa Arusha mjini, Mhe. Godbless Lema.

Viongozi wengine waliofika mahakamani leo ni Katibu Mkuu wa CHADEMA Taifa, Dkt. Vincent Mashinji, Mjumbe wa Kamati Kuu,Prof. Mwesiga Baregu, Waziri Mkuu Mstaafu, Mhe. Frederick Sumaye, Meya wa jiji la Arusha,Mhe. Calist Lazaro, Katibu wa CHADEMA Arusha, Mhe. Aman Golugwa na viongozi mbalimbali wa CHADEMA.
View attachment 474945
================
Taarifa ambazo tumezipata Mbunge Godbless Jonathan Lema atapandishwa kizimbani muda mfupi ujao.
Uamuzi unaanza kutolewa.
Mahakama ya Rufani kanda ya Arusha imetoa maelekezo ya kesi irudi kwenye mahakama zenye dhamana ya kutoa dhamana kwa Mh. Lema, kwani hakuna hoja ya msingi kwa rufaa iliyokatwa na mawakili wa serikali.

Majaji wamesema wamesoma mapingamizi ya mawakili wa serikali bila kuona tija yeyote ya kisheria kwaiyo inatoa oda kwa Mahakama kuu kulishughulikia swala la Godbless Jonathan Lema haraka sana.

MUNGU yupi? huyu aliyetufundisha na kutuasa kuwa na kauli njema? Na kutokuwa na kauli za kuudhi
 
Back
Top Bottom