Jembe Jembe
JF-Expert Member
- Jun 9, 2016
- 749
- 1,797
Mahakama ya wilaya ya Mkoa wa Arusha imemwachia huru mfanyabiashara Maarufu wa madini ya Tanzanite jiiini Arusha Lucas Mdeme(46) na mwenzake Nelson Lyimo(58) waliokuwa wakikabiliwa na mashtaka sita likiwemo la uhujumu uchumi baada ya upande wa mashtaka kudai haina Nia ya kuendelea nao katika shauri hilo.
Mdeme na Lyimo walikuwa ni miongoni mwa washtakiwa nane wakiwemo Askari Polisi watatu katika kesi ya uhujumu uchumi ,utakatishaji fedha haramu na kupanga njama za kujipatia rushwa ya fedha ya awali shilingi milioni 10 kati ya milioni 30 walizohitaji kutoka kwa Mfanyabiashara maarufu Jijini ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama Cha Wauzaji Madini Wakubwa ndani ya nchi na nje {TAMIDA} Sammy Mollel.
Waendesha mashtaka wa serikali Adelaide Kassalay na Agnes Hyera walimweleza Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya wilaya ya Arusha,Rose Ngoka kwamba upande wa jamhuri haina nia ya kuendelea nao katika shauri hilo na hivyo wanaiomba mahakama iweze kuwaachia huru bila masharti yoyote.
‘’Mheshimiwa Hakimu upande wa jamhuri hatuna Nia ya kuendelea na mshtakiwa namba sita na Saba katika shauri hilo hivyo tunaiomba mahakama iwaachie huru bila masharti yoyote’’alisema Kassalay.
Kufuatia maelezo hayo Hakimu Ngoka aliamuru kuachiwa kwa mshtakiwa namba Saba ,Lucas Mdeme na mshtakiwa namba sita Nelson Lyimo na alihairisha kesi hiyo hadi mai 4 mwaka huu kwa washtakiwa wengine waliobakia wakiwemo Askari Polisi.
Askari waliopandishwa kizimbani baada ya kufukuzwa kazi ni pamoja na askari mwenye namba G. 5134 DC Heavenlight Mushi aliyekuwa Askari kitengo Cha Intelijensia Mkoa wa Kipolisi Kinondoni jijini Dar es Salaam,H.125 PC Gasper Paul kitengo Cha Intelijensia Makao Makuu Dodoma na H.1021 PC Bryton Murumbe aliyekuwa Askari wa kawaida Mkoani Dodoma.
Wengine wanaoshikiliwa mahabusu katika kesi hiyo ni pamoja na Joseph Chacha{43} maarufu kwa jina la ‘’baba Ngodo’’ mkazi wa Ilboru, Leonila Joseph{46} mkazi wa Ilboru, na Omary Alphonce{43} maarufu kwa jina la Matelephone mkazi wa Olasiva Jijini Arusha.
Ends...