Arusha: Mahakama yakubali pingamizi utetezi kesi ya Sabaya

Waziri2025

Senior Member
Sep 2, 2019
148
379
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Arusha, imeridhia pingamizi lililowekwa na mawakili wa upande wa utetezi wakipinga shahidi wa 13 wa Jamhuri Ramadhani Juma(39), kuzitolea ufafanuzi video za CCTV wakidai kwamba siyo mtaalamu na hana uwezo wa kuzizungumzia.

Akitoa uamuzi mdogo mahakamani huko jana, Hakimu wa mahakama hiyo, Patricia Kisinda, kwa kuzingatia sheria ya ushahidi kifungu cha 47 na uamuzi wa mahakama za juu shahidi sio mtaalamu na hana uwezo wa kuitolea ufafanuzi video za CCTV .

Alisema kwa kuwa shahidi huyo alikuwa ni mchunguzi katika shauri hilo na alitumia taarifa kutoka maabara ya uchunguzi wa kielekroniki lakini siyo mtaalamu na hana uwezo wa kuzitolea video hihiz

=====

Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha imekubali pingamizi la mawakili wa utetezi katika kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya na wenzake sita.
Desemba 17 mwaka jana, mawakili wa utetezi waliwasilisha hoja ya pingamizi wakipinga shahidi wa 13 wa Jamhuri ambaye ni Ofisa Uchunguzi kutoka Takukuru, Ramadhan Juma asitolee ufafanuzi ikiwemo kuwatambua watu kupitia picha za CCTV Kamera zilizopo kwenye ripoti ambayo hajaiandaa yeye.

Akitoa uamuzi huo mdogo leo Januari 3,2022 Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo, Patricia Kisinda amesema uamuzi wake umezingatia sheria ya ushahidi pamoja na uamuzi uliotolewa na mahakama za juu, ambapo amekubaliana na pingamizi na upande wa mashitaka uendelee kumuongoza shahidi kwa kumuuliza maswali mengine.

"Mahakama imeangalia sheria ya ushahidi na kurejea maamuzi ya mahakama za juu na kuona shahidi siyo mtaalamu wa maabara ya kiuchunguzi na hana uwezo wa kujibu swali kuhusiana na CCTV kamera," amesema Hakimu

Awali akiwasilisha hoja ya pingamizi hilo Wakili wa utetezi Mossea Mahuna aliieleza mahakama kuwa shahidi huyo hana uwezo wa kutambua watu kupitia ripoti hiyo ambayo hajaiandaa yeye na wala siyo mtaalamu kutoka maabara ya kiuchunguzi.
Alisema kuwa shahidi wa nane, Johnson Kisaka (Ofisa uchunguzi kutoka maabara ya kiuchunguzi ya Takukuru) aliieleza mahakama kuwa hawezi kumtambua mtu kupitia ripoti hiyo.

Alieleza kuwa iwapo Juma atawatambua watu hao wakati hajashiriki wala kuandaa ripoti hiyo atakuwa anatoa maoni yake hivyo kuomba mahakama isimruhusu kutambua watu kwenye ripoti ambayo hajaandaa yeye.

Kwa upande wao mawakili wa Serikali waliomba mahakama hiyo kutupilia mbali pingamizi hilo kwani halina misingi ya kisheria wala mashiko na kuwa shahidi huyo alikuwa anataka kuionyesha mahakama kile alichokuwa ameeleza kukibaini kwenye ripoti hiyo iliyopo kwenye flash.

Awali uamuzi huo ulipangwa kutolewa Desemba 29 mwaka jana ila ilishindikana baada ya mawakili wa utetezi kushindwa kufika mahakamani ambapo leo utetezi uliwakilishwa na Mawakili Mosses Mahuna, Fauzia Mustafa na Wlliams Alexander.

Jamhuri iliwakilishwa na Mawakili wa Serikali Waandamizi Janeth Sekule, Felix Kwetukia, Tarsila Gervas na Wakili wa Serikali Neema Mbwana huku Takukuru ikiwakilishwa na Wakili Jacob Piyo.

Baada ya uamuzi huo shahidi huyo ameendelea kutoa ushahidi wake pasipo kuwekwa kwa video hizo zilizopo katika flash ambapo aliieleza mahakama kufuatia uchunguzi wake alibaini Sabaya alikuwa akiratibu genge la uhalifu na vijana wake ambao walikuwa wakitekeleza maelekezo yake.

Shahidi huyo alidai washitakiwa wengine Enock Mnkeni, Watson Mwahomange, John Aweyo, Sylvester Nyegu, Jackson Macha na Nathan Msuya walitekeleza jukumu la kuchukua rushwa ya Sh90 milioni kutoka kwa mfanyabiashara Francis Mrosso, ambayo yalikuwa maagizo toka kwa Sabaya.

Shahidi huyo ameeleza mahakama kuwa watuhumiwa wawili Msuya na Macha walikimbilia wilayani Rombo Mkoa wa Kilimanjaro ambapo baada ya wenzao kufikishwa mahakamani Juni 15 usiku walikamatwa baada ya kurejea katika makazi yao wilayani Moshi.

Akiongozwa na Wakili, Kwetukia alidai baada ya kufanya mahojiano ya awali na Msuya alikiri kuwa miongoni mwa vijana wanaounda genge la Sabaya na huwa anatumika kama dereva na Januari 22,2021 alikiri kwenda kwa Mrosso na wenzake kuchukua rushwa ya Sh90 na kukiri kupata mgao wa laki tano.

"Macha alikiri kuwa miongoni mwa vijana wa Sabaya na alijiunga baada ya kushawishiwa na Msuya na kwa kuwa alikuwa na taaluma ya fedha alipewa jukumu la kuwa Ofisa TRA walipofika kwa Mrosso, alikiri kwenda benki ya CRDB kwa Mromboo na kupata mgao wa Sh1.4 milioni"

Juma alidai kuwa Sabaya hakuwa na biashara aliyokuwa anafanya wala mkopo na kuwa gari alilonunua ilikuwa ni zao la rushwa aliyoiomba na kupokea Januari 22 toka kwa Mrosso.

"Gari lile nilithibitisha kuwa ni zao la rushwa kwani alinunua siku 10 baada ya kuchukua rushwa hiyo na nilienda taasisi za kifedha kama Sabaya ana mkopo na hakuwa na mkopo,"alisema na kuongeza
"Nilienda benki ya CRDB ambapo Sabaya alikuwa na akaunti na mshahara ulikuwa unapitia huko, NMB, Exim, Barclays, Akiba benki na nikabaini hakuna taasisi ya kifedha aliyikopa Sabaya iliyomuwezesha kununua gari,"

Kesi hiyo imeahirishwa hadi kesho Januari 4, 2022 atakapoanza kuhojiwa na mawakili wa utetezi.

Chanzo: Mwananchi
 
Gaidi atatoa macho kama amebanwa na mlango ila kwa ujumla kesi ya Sabaya ni siasa tupu wala hajafanya kosa lolote.
Punguza roho mbaya mada inamzungumzia Sabaya wewe unamshambulia mwingine. Tatizo mnashabikia na kuabudu vyama mpaka ubinadamu unawatoka. Tofautisha vyama na ubinadamu
 
Tunaomba kesi ya gaidi iyanze mara moja,kesi nzito na yenye ushahidibulionyooka inapakwa pakwa rangi..wanatulete kesi ya Sabaya iliyojaa siasa tupu.


Huyu gaidi afungwe chapu waache kuisumbua mahakama
 
Anaonewa na wamachame wa Hai
Wanachama wa hai ndiyo waliomtuma aajiri majangili na kutengeneza genge la uhalifu?
Wamachame ndo waliomfanya ampore mrombo pesa zake ml 90 na kwenda kununua gari ya ml 60 na kulala na mabaya wa kidimbwi?
Wamachame ndiyo wanaotoa ushahidi mahakamani?
( sikiliza nondo zilizotolewa na mpelelezi mkuu wa Pccb leo) au na yeye ni wa hai?
 
Back
Top Bottom