Arusha: Mahakama yaamuru mfanyabiashara Philemon Mollel kunyang'anywa eneo la hekari 7 alilowekeza kituo cha mafuta

jembejembe

JF-Expert Member
Jun 9, 2016
632
1,000
Mahakama Kuu Kanda ya Arusha imempokonya mfanyabiashara maarufu jijini Arusha Philemon Mollel(Monaban) ,eneo lenye ukubwa wa ekari Saba alilowekeza kituo Cha mafuta lililopo Ngulelo ,jijini Arusha, Mara baada ya mahakama hiyo kujiridhisha kwamba alikuwa anamiliki kinyume Cha Sheria.

Kesi hiyo ya madai namba 1 /2017 ilikuwa ikisikilizwa na Jaji Mosses Mzuna wa mahakama hiyo ambaye aliridhika pasipo shaka kwamba eneo hilo ni Mali halali ya William Taitus Mollel Mkazi wa Ngulelo jijini Arusha.

Katika uamuzi wa jaji Mzuna alioutoa Mei 11 mwaka huu alizingatia ushahidi uliotolewa na pande zote mbili ikiwemo vielelezo vya umiliki,ndipo alipobaini kwamba mollel hakuwa Mmiliki halali bali alivamia pasipo kufuata Sheria za umiliki.

Jaji Mzuna alipomtaja Mollel kama mvamizi wa eneo hilo ambaye hakuwahi kutambulika kama Mmiliki halali wa eneo hilo ambalo aliliendeleza kwa kuwekeza kituo Cha Mafuta pamoja na biashara zingine.

Kesi hiyo iliyodumu kwa zaidi ya miaka mitano ilichukua sura mpya hapo jana mara baada ya walinzi kutoka kampuni binafsi ya ulinzi kuvamia eneo la kituo cha Mafuta na kuzua taharuki kwa kuwatimua wafanyakazi hao na kisha kulizungumzia utepe eneo hilo.

Hata hivyo upande wa Mollel ulijaribu kujibu mapigo kwa kuleta walinzi wake ili kuokoa kituo hicho cha Mafuta lakini polisi wenye silaha za Moto waliingilia Kati na kufika eneo la tukio baada ya kuarifiwa kuwepo kwa dariri za uvunjifu wa Amani na kufanikisha kuwasambaratisha watu waliojaribu kuleta vurugu.

Akizungumzia hatua hiyo Taitas amesema kwamba anaishukuru mahakama hiyo kwani imetenda haki na kuwashauri watu wengine waliodhulumiwa maeneo yao na watu wenye fedha kudai haki yao mahakamani.

Kwa upande wake Philemon Mollel alidai kutoridhika na maamuzi ya mahakama hiyo na tayari amekata rufaa kupinga uamuzi huo .

Mollel alisema kuwa kilichofanyika ni uhuni kwa sababu mahakama hiyo haikuelekeza apokonywe eneo hilo kibabe na kumfungia biashara zake.

Alisema kuwa eneo hilo lenye viwanja vinne aliinunua kisheria mwaka 2009 kutoka kwa Jimmy Taitas Mollel kwa makubaliano ya shilingi milioni 95 kwa kila kiwanja kimoja na kufanya uwekezaji wa Kituo Cha Mafuta na sehemu ya kuoshea magari .

Alisema mwaka 2017 familia ya Taitas walifanya mabadiliko ya msimamizi wa mirathi kwa kumteua Mdogo wao William Taitas Mollel ambaye mwaka 2017 alifungua shauri mahakamani alidai eneo hilo.

Alisema baada ya kutoka hukumu na wao kushindwa waliamua kukata rufaa kupinga hukumu hiyo na ameshangaa kuona Taitas akivamia kutuo cha Mafuta na kusitisha shughuli zote za biashara yake.

Mollel amelalamika kutopata msaada wowote kutoka Jeshi la polisi kutokana na kitendo Cha uvamizi kilichofanywa na William Taitas Mollel kwa kufungia biashara zake.

Ends...

IMG_20210515_184020_174.jpg
 
Nkanini

JF-Expert Member
Jun 6, 2017
2,239
2,000
Mkuu hiki kichwa cha habari ya hoja yako umekiandika kama mwandishi wa magazeti ya musiba!haki imetendeka mahakamani na asiyeridhika amepewa haki ya ku appeal sasa wapi ameporwa mchana kweupe?
 
macho_mdiliko

JF-Expert Member
Mar 10, 2008
14,284
2,000
Na amezowea maana hata NMC kule Unga Ltd alisema ni mali yake. Kabla serikali haija muweka kando.
Wafanyabiashara wengi matapeli wanapenda sana kuitumia CCM kujificha. Infact ni watu wengi matapeli hupenda kujificha kwenye chaka la ukada ili kuendeleza hujuma zao.
 
UmkhontoweSizwe

JF-Expert Member
Dec 19, 2008
4,989
2,000
Wafanyabiashara wengi matapeli wanapenda sana kuitumia CCM kujificha. Infact ni watu wengi matapeli hupenda kujificha kwenye chaka la ukada ili kuendeleza hujuma zao.
Mambo hayo yalishamiri sana wakati wa utawala wa JK, wafanyabiashara majizi, matapeli, wanyang'anyi, zulumati, madawa ya kulevya, vyote vilikuwa halali as far as wewe ni kada wa chama.
 
Benny Haraba

JF-Expert Member
Dec 7, 2012
6,743
2,000
Mahakama Kuu Kanda ya Arusha imempokonya mfanyabiashara maarufu jijini Arusha Philemon Mollel(Monaban) ,eneo lenye ukubwa wa ekari Saba alilowekeza kituo Cha mafuta lililopo Ngulelo ,jijini Arusha, Mara baada ya mahakama hiyo kujiridhisha kwamba alikuwa anamiliki kinyume Cha Sheria.

Kesi hiyo ya madai namba 1 /2017 ilikuwa ikisikilizwa na Jaji Mosses Mzuna wa mahakama hiyo ambaye aliridhika pasipo shaka kwamba eneo hilo ni Mali halali ya William Taitus Mollel Mkazi wa Ngulelo jijini Arusha.

Katika uamuzi wa jaji Mzuna alioutoa Mei 11 mwaka huu alizingatia ushahidi uliotolewa na pande zote mbili ikiwemo vielelezo vya umiliki,ndipo alipobaini kwamba mollel hakuwa Mmiliki halali bali alivamia pasipo kufuata Sheria za umiliki.

Jaji Mzuna alipomtaja Mollel kama mvamizi wa eneo hilo ambaye hakuwahi kutambulika kama Mmiliki halali wa eneo hilo ambalo aliliendeleza kwa kuwekeza kituo Cha Mafuta pamoja na biashara zingine.

Kesi hiyo iliyodumu kwa zaidi ya miaka mitano ilichukua sura mpya hapo jana mara baada ya walinzi kutoka kampuni binafsi ya ulinzi kuvamia eneo la kituo cha Mafuta na kuzua taharuki kwa kuwatimua wafanyakazi hao na kisha kulizungumzia utepe eneo hilo.

Hata hivyo upande wa Mollel ulijaribu kujibu mapigo kwa kuleta walinzi wake ili kuokoa kituo hicho cha Mafuta lakini polisi wenye silaha za Moto waliingilia Kati na kufika eneo la tukio baada ya kuarifiwa kuwepo kwa dariri za uvunjifu wa Amani na kufanikisha kuwasambaratisha watu waliojaribu kuleta vurugu.

Akizungumzia hatua hiyo Taitas amesema kwamba anaishukuru mahakama hiyo kwani imetenda haki na kuwashauri watu wengine waliodhulumiwa maeneo yao na watu wenye fedha kudai haki yao mahakamani.

Kwa upande wake Philemon Mollel alidai kutoridhika na maamuzi ya mahakama hiyo na tayari amekata rufaa kupinga uamuzi huo .

Mollel alisema kuwa kilichofanyika ni uhuni kwa sababu mahakama hiyo haikuelekeza apokonywe eneo hilo kibabe na kumfungia biashara zake.

Alisema kuwa eneo hilo lenye viwanja vinne aliinunua kisheria mwaka 2009 kutoka kwa Jimmy Taitas Mollel kwa makubaliano ya shilingi milioni 95 kwa kila kiwanja kimoja na kufanya uwekezaji wa Kituo Cha Mafuta na sehemu ya kuoshea magari .

Alisema mwaka 2017 familia ya Taitas walifanya mabadiliko ya msimamizi wa mirathi kwa kumteua Mdogo wao William Taitas Mollel ambaye mwaka 2017 alifungua shauri mahakamani alidai eneo hilo.

Alisema baada ya kutoka hukumu na wao kushindwa waliamua kukata rufaa kupinga hukumu hiyo na ameshangaa kuona Taitas akivamia kutuo cha Mafuta na kusitisha shughuli zote za biashara yake.

Mollel amelalamika kutopata msaada wowote kutoka Jeshi la polisi kutokana na kitendo Cha uvamizi kilichofanywa na William Taitas Mollel kwa kufungia biashara zake.

Ends.....

View attachment 1787384
labda alitaka kusema mita 700
 
mrangi

JF-Expert Member
Feb 19, 2014
56,151
2,000
Monaban kutwa ana visanga
Hivi ile issue ya NMC iliishia wapi

Ova
 
Uzalendo Wa Kitanzania

JF-Expert Member
Mar 8, 2020
1,010
2,000
Monaban ni kada wa CCM aliyekosa sifa ya Uadilifu kabisa

Kwa ujumla maisha yake yamejaa ulaghai, dhuluma & usanii mkubwa

Yanayomtokea sasa ni matunda ya dhuluma alizofawafanyia watu mbalimbali siku za nyuma
 
sajo

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
1,115
2,000
Mahakama haiwezi kuamuru mtu kunyang'anywa ardhi bali Inaamuru mtu mvamizi kuondoka katika ardhi aliyovamia na aliyevamiwa kurudishiwa ardhi yake. Kichwa cha habari kilivyoandikwa ni kama Mahakama imehalalisha unyang'anyanyi (uporaji) wa ardhi. Maana ya kunyang'anya ni kuwa, mmiliki halali wa eneo anaporwa eneo lake na kupewa mtu mwingine asiyestahili.
 
tweenty4seven

JF-Expert Member
Sep 21, 2013
12,704
2,000
Hilo eneo liko barabarani thamani yake kwa sasa linaweza kufika 3bn au zaidi mana eka moja pembeni ya hiyo barabara inazidi 500m...jamaa alikua ananunua kwa kaka mtu hiyo ardhi wakati ni mali ya familia na yote ina title
 
Bu'yaka

JF-Expert Member
Jul 29, 2010
1,470
2,000
Mambo hayo yalishamiri sana wakati wa utawala wa JK, wafanyabiashara majizi, matapeli, wanyang'anyi, zulumati, madawa ya ....
Ni kweli

huyo JK mwenyewe alitamka kwenye hotuba yake ya kumzika JPM kwamba watu wa Ardhi (wizara) huwawezi hata ungefanya vipi... Rais mstaafu anamkatisha tamaa rais mwingine kwa sababu yeye alishindwa..
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom