Francis12
JF-Expert Member
- Sep 30, 2016
- 7,533
- 22,276
Mahakama Kuu Kanda ya Arusha leo Ijumaa tarehe 16.12.2016 majira saa 4 asubuhi itatoa uamuzi dhidi ya Pingamizi la awali lililowekwa na Mawakili wa upande wa serikali kwenye rufaa mpya ya dhamana yaliyowasilishwa mawakili upande wa Mbunge Godbless Lema.
Pia kutasikilizwa kwa maombi upande wa mawakili wa mbunge Lema. Wananchi wote mnakaribishwa kujitokeza kwa wingi mahakamani ili kumtia moyo Mbunge wenu Godbless Jonathan Lema.
[HASHTAG]#Justice[/HASHTAG] For Lema
[HASHTAG]#Bring[/HASHTAG] Back Ben Saanane
[HASHTAG]#Justice For [/HASHTAG]Maxence Melo
============
Wakili anayemtetea Mbunge Godbless Jonathan Lema Sheck Mfinanga ameshawasili
Jeshi la Polisi wamezuia wananchi kuingia mahakamani kusikiliza kesi ya mbunge Godbless Lema.
Tulipewa taarifa kesi itaanza kusikilizwa kuanzia saa 10.00 mpaka sasa bado hajaanza.
Kesi ya kwanza inaendelea mahakamani muda huu tumezuia kuingia ndani.
Waandishi wa habari tumezuia kuingia mahakamani kusikiliza kesi ya mbunge Godbless Jonathan Lema kwa kisingizio kuwa ndani nafasi ni ndogo sana.
Geti la kwanza tumekaguliwa tukaruhusiwa kuingia ndani tena kukawa na ukaguzi mwingine wakutoa kitambulisho tofauti na geti la kwanza,licha ya kuonyesha vitambulisho kisingizio kikaja hamna nafasi ndani.
Pingamizi la upande wa mawakili wa serikali la kwanza limetupiliwa nje.
Mapingamizi mawili juu ya rufaa ya dhamana ya kesi inayomkabili Lema zilizowekwa na Serikali yametupiliwa mbali na mahakama mchana huu.
Shauri upande wa mawakili wa mbunge Godbless Lema limeshaanza kusikilizwa
Kesi ya rufaa ya dhamana inaendelea mahakamani muda huu.
Majibizano ya kisheria yanaendelea muda huu mahakamani.
Kesi bado inaendelea mahakamani maamuzi yakitolewa tutawaletea taarifa muwe na subira kuna mabishano makubwa sana ya kisheria kati pande zote mbili
Uamuzi umetolewa kesi ya Mbunge Godbless Jonathan Lema imearishwa mpaka tarehe 20.12.2016
Tarehe 20.12.2016 ndo maamuzi kuhusu dhamana ya Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini Godbless Lema yatatolewa.
========
Pingamizi la serikali latupwa kesi ya Lema
Mahakama Kuu Kanda ya Arusha imetupilia mbali pingamizi la mawakili wa serikali ilizoweka dhidi ya taarifa ya dharura ya kusudio la kukataa rufaa ya mawakili wa Mbunge wa Arusha Mjini, Godblees Lema.
Mbunge Godbless Lema akirudishwa gerezani
Jaji Modesta Opiyo wa mahakama kuu kanda ya Arusha alisema katika maamuzi yake kuwa pingamizi zilizowekwa hazina msingi kwani waleta maombi walifuata taratibu zote za katika kiapo na hati ya dharua ya kuitwa mahakamani.
Baada ya uamuzi huo Jaji Opiyo aliwataka mawakili wa Lema ,Shedrack Mfinanga na Faraji Mangula kuwasilisha hoja zao katika kiapo na hati ya dharura.
Akizungumza baada ya kukubaliwa na Jaji ,wakili Mfinanga alimtaka Jaji huyo kusikiliza rufaa hiyo kwani kuchelewa siyo sababu ya msingi sana kwa mujibu wa sheria na kunukuu kesi mbalimbali zilizochelewa kukatiwa rufaa kwa siku nyingi na kudai kuwa mahakama ya rufaa ilizikubali na kuzitolea maamuzi.
Mfinanga amesema na kumwomba Jaji kusikiliza rufaa yao kwa sababu ni ya msingi na kamwe haiwezi kuvunja sheria ya makosa ya jinai iliyowekwa kwa mujibu wa sheria.
Mawakili wa serikali wakiongozwa na Wakili Mfawidhi Materius Marandu, Hashim Ngole na Elizabert Swai walipinga vikali kukubaliwa kwa rufaa hiyo kwa madai kuwa Jaji Msengi alitupilia mbali na kurudia kuikubali ni ukiukwaji mkubwa wa sheria za makosa ya Jinai.
Baada ya malumbano hayo yaliyochukuwa zaidi ya masaa 5 Jaji Opiyo alisema kuwa uamuzi wa kuikubali ama kuikataa rufaa hiyo atautoa Desemba 20 mwaka huu majira ya saa 6 mchana katika mahakama hiyo.
Godbless Lema
Lema anakabiliwa na kesi hiyo ya uchochezi aliyosomewa katika mahakama ya wilaya ya Arusha mbele ya hakimu mkazi Deusdedit Kamugisha Novemba 8 mwaka huu na aliwekewa pingamizi na mawakili wa serikali ya kutopata dhamana baada ya hakimu kusema kuwa dhamana iko wazi.
Mbunge huyo wa Arusha Mjini alikamatwa Novemba 2 mwaka huu Mkoani Dodoama kwa kosa hilo baada ya kuhutubia katika mikutano ya hadhara katika kata mbalimbali za Jiji la Arusha kuwa ameoteshwa kuwa Rais Magufuli atakufa kabla ya mwaka 2020 hali inayodaiwa kuleta uchochezi kwa wananchi waliomchagua kuwa Rais wa nchi.
Chanzo: IPP Media