Arusha - Mahakama Afrika yaibua ukandamizaji Tanzania kesi ya mgombea binafsi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Arusha - Mahakama Afrika yaibua ukandamizaji Tanzania kesi ya mgombea binafsi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Candid Scope, Jun 16, 2012.

 1. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #1
  Jun 16, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  [​IMG]
  Mwanaharakati na Mwanasiasa
  Mchungaji Mtikila

  Kesi inayounguruma Arusha ambayo ilifunguliwa na Mchungaji Mtikila dhidi ya serikali ya Tanzania ukiukwaji wa haki za binafsi kuhusu mgombea binafsi inaelekea Ukingoni huku Majaji wakiwabamiza ukutani mawakili wanaoitetea serikali dhidi ya usawa na haki za binadamu juu ya uhuru wa mtu binafsi kugombea nafasi za uongozi wa kisiasa Tanzania.

  • Majaji wa haki za binadamu Afrika katika kesi iliyofunguliwa na Mchungaji Mtikila waliuliza kama kuna usawa kwenye siasa Tanzania kwa wagombea wa vyama vyote kwa nyakati za chaguzi mbalimbali.
  • Majaji walidadisi kama Tanzania kuna haki ya raia wa kawaida ana fulsa ya kwenda bungeni kudai ya marekebisho ya sheria inayokiuka haki yao.
  • Majaji walitaka ufafanuzi wa hoja za watetezi wa serikali kwamba uamuzi wa kuzuia mgombea binafsi ni mahitaji ya umma.
  • Majaji waliwakaba watetezi wa serikali waliposema hoja hiyo imepitwa na wakati kwa vile serikali ipo kwenye mchakacho wa kufanya marekebisho ya sheria, majaji waliwauliza kwa nini tangu hukumu hiyo ilipotolewa na mahakama ya rufaa hadi leo bunge halijafanyia marekebisho ya sheria hiyo kama ilivyoamuliwa na mahakama ya rufaa.
  • Majaji hao waliwauliza mawakili wa serikali kama bunge linaweza kutunga sheria inayofuta nyingine wakati uzoefu unaonyesha wabunge huunga mkono yaliyomo kwenye katiba hata kama wananchi wanalalamikia kukiukwa haki zao.
  • Mtikila kwa upande wake aliulizwa kwa nini ana anadai haki za mgombea binafsi wakati yeye ana chama chake cha siasa.
  Hukumu itatolewa ndani ya miezi mitatu baada ya kupitia hoja za mawakili wa pande zote katika kesi hiyo.

  Source: Habari Leo
   
 2. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #2
  Jun 16, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Mmoja kati ya wanasiasa machachari na ambaye ni mwanaharakati asiyechoka kudai haki za watanzania na kujitoa kwa kila njia kutetea haki za msingi ni huyu Mchungaji Mtikila. Itafika wakati tutamkumbuka katika historia ingawa kwa sasa haionyeshi wazi juhudi zake. Hii inatokana na yeye wakati mwingine kutokuwa na ushirikiana na wanasiasa wengine wa vyama vya upinzani.
   
 3. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #3
  Jun 16, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Mtikila bwana anapambana kweli. Tungepata wanaharakati watatu tu kama hawa Tanzania tungekuwa mbali!
   
 4. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #4
  Jun 16, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Mh sina hakika kama harakati zake ni kwaajili ya taifa ama maslahi binafsi yetu macho!
   
 5. OSOKONI

  OSOKONI JF-Expert Member

  #5
  Jun 16, 2012
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 10,809
  Likes Received: 3,892
  Trophy Points: 280
  tunahitaji mmoja zaidi maana wewe na yeye tayari ni wawili!!
   
 6. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #6
  Jun 16, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,199
  Likes Received: 1,978
  Trophy Points: 280
  Ni kweli mkuu Kimbunga si unakumbuka kule kwa chacha wangwe alipambana na mawe jukwaani kwi! Kwi! Kwi!
   
 7. mpinga shetani

  mpinga shetani JF-Expert Member

  #7
  Jun 16, 2012
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 3,268
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 145
  Ni kweli. Mtikila mmoja ni sawa na Chadema 5000
   
 8. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #8
  Jun 16, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Mkuu Precise pangolin unajua wanasiasa karibu wote ni wachumia tumbo hivyo naye kuna wakati huchumia tumbo. Lakini tofauti yake na wanasiasa wengine yeye huwa na misimamo ya kuikomboa jamii kwa ujumla wake. Kama unakumbuka aliipigania Tanganyika kwa muda mrefu. Kwa kulisimamia hili na kwa kuamimi katika Tanganyika chama chake kilichelewa kupata usajili wa kudumu kama Chama cha siasa. Akaja akapigania mgombea binafsi na bado anaendeleza mapambano. Siamini kuwa ugombea binafsi ni wa ajili yake tu.

  Yeye anapigania sheria kubadilishwa ili kuwe na uwanja sawa wa mchezo siyo unaingia kwenye uchaguzi huku ukijua kwamba sheria ni pendelezi baadaye unaanza kupiga mayowe ati umeonewa!
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 9. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #9
  Jun 16, 2012
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,634
  Trophy Points: 280
  Duh Mtikila lazima atakuwa na damu ya kipare anavyopenda kesi kama Mkurya na Ugali.
   
 10. Bilionea Asigwa

  Bilionea Asigwa JF-Expert Member

  #10
  Jun 16, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 12,628
  Likes Received: 9,841
  Trophy Points: 280
  safi sanaa..
  mtikila jembe sana
  mpaka kitaeleweka tuu
   
 11. idawa

  idawa JF-Expert Member

  #11
  Jun 16, 2012
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 18,539
  Likes Received: 10,462
  Trophy Points: 280
  umejichanganya hujaeleweka.!
   
 12. wagaba

  wagaba JF-Expert Member

  #12
  Jun 16, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 829
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  Mgombea binafsi imepata baraka zote kwa sasa, lazima hukumu itakuwa in his favour.
  Hakuna jipya hapa.
   
 13. Baba V

  Baba V JF-Expert Member

  #13
  Jun 16, 2012
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 19,507
  Likes Received: 170
  Trophy Points: 160
  na CCM yote na ndo maana anaikimbiza serikali yao vibaya
   
 14. Joseph

  Joseph JF-Expert Member

  #14
  Jun 16, 2012
  Joined: Aug 3, 2007
  Messages: 3,527
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Huyu jamaa ananikosha sana maana yeye ni mtu pekee ambaye amekuwa mstariwa mbele katika kutetea haki za umma wa watanzia kwa ujumla wao.
   
 15. m

  muchetz JF-Expert Member

  #15
  Jun 16, 2012
  Joined: Aug 16, 2010
  Messages: 495
  Likes Received: 97
  Trophy Points: 45
  Hii kitu ni muhimu sana kuliko tunavyofikiria. Ikitokea Mtikila akashinda inaweza kuleta mabadiliko makubwa sana kwenye siasa za Tanzania, kwani si siri wengi wetu tu waoga sana linapokuja suala la ushiriki wa siasa sababu ya namna tuanavyo jihusisha na vyama vya siasa. Bado kuna dhana kwa kiasi kikubwa kwamba ushiriki wa kisiasa maana yake ni kujiunga na chama.

  Ukisema ubunge kwa mfano mtu anauangalia zaidi kama CCM, CDM, CUF e.t.c vivyo hivyo kwa udiwani na vyeo vingine vya kisiasa. Pili sio siri vyama vikuu vya kisiasa (na hasa CCM ambayo iko madarakani inanufaika zaidi na hili) vinatumia rungu la sheria inayolazimisha wagombea wa kisiasa kuwa wanachama wa kisiasa kutishia uhuru wa wanasiasa kuendeleza ukuu wao.

  Hivyo basi utaona uwepo wa mgombea binafsi unavyo hatarisha ukuu wa vyama hivi.

  Naamini uwepo mwa mgombe binafsi utapanua kwa kiwango kikubwa uwajibikaji wa viongozi wa kisiasa kwa wananchi badala ya chama, au serikali(ambayo inaundwa na chama) hivyo pia kufanya uwajibikaji wa serikali kuwa mkubwa zaidi (checks and balances). Kwa mfano mbuge aliyegombea kupitia jimbo X kama mgombea binafsi hawezi kutishwa kufukuzwa ubunge wake na katibu wa chama(ukifukuwa uanachama uanpoteza uwaziri, ubunge nk) kwasababu hana bosi wa aina hiyo.

  Mwisho kabisa naamini pia mgombea binafsi anaweza kuleta mabadiliko makubwa kwenye uundwaji na malengo ya vyama vya siasa na hatimaye bunge letu na hata serikali zetu siku za mbele. Tunaweza kuwa tumepata moja ya machujio muhimu yanayo tuletea siasa uchwara za vyama.!!!
   
 16. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #16
  Jun 16, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Kadiri ya kumbukumbu zangu Mtikila ndiye anayethubutu kuibamiza serikali mahakamani, wengine wanaishia tu maandamano. Huyu jamaa ni jabali.
   
 17. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #17
  Jun 16, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Good point. Uthubutu wa mgombea binafsi kisiasa kutaleta mwamko wa wananchi kujua zaidi hazi zao za msingi kuzidai bungeni kama Jaji alivyouliza kuhusu uwezekano wa raia wa chini kuweza kwenda bungeni kudai mabadiliko ya sheria ambayo inamkandamiza. Jambo hilo kwa sasa halipo na hakuna dalili ya kuruhusu uwepo wa dirisha kama hilo.
   
 18. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #18
  Jun 16, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Nisingekubaliana na hoja yako kwa sababu Mtikila alipoanza muda mrefu kupigania Utanganyika si dalili ya masilahi binafsi vinginevyo ni msukumo wa kuona mbali machungu tuliyonayo ya Muungano.

  Hili la mgombea binafsi Mtikila binafsi hana shida nalo kwa vile anacho chama cha siasa ambacho anaweza kupigia kugombea.

  Kwa vyo vyote anachohangaikia Mtikila ni haki za binadamu. Jua yeye ni Mchungaji na kujitolea kwa ajili ya kondoo ni jambo la kawaida katika itikadi za uchungaji.
   
 19. m

  mchaichai JF-Expert Member

  #19
  Jun 16, 2012
  Joined: Nov 5, 2011
  Messages: 650
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mchungaji Mtikila mungu akubariki sana na tunakuombea kuna cku mungu atakulipa...sala zangu na za wapenda mageuzi watakuombea maisha marefu wewe na familia yako na tunakuomba uwaandae watoto wako kuwa kama wewe kwani nchi hii bado tunahitaji wapiganaji vingnevyo watoto na wajuu zetu hasa cc vijana watakuwa manamba
   
 20. M

  Mjenda Chilo JF-Expert Member

  #20
  Jun 16, 2012
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 1,425
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 145
  Na ipitishwe nikachukue jimbo nami nipate title ya uheshimiwa b4 my name, hii Phd naona imegoma kuisha inipe cheo cha u Dr. Wananchi msininyime kura coz mabomba lzm yatoe maziwa nchi nzima.
   
Loading...