Return Of Undertaker
JF-Expert Member
- Jun 12, 2012
- 4,572
- 26,885
The wonders of the world.
Ambulace zilizonunuliwa awamu ya 4 na wabunge wawili wa mkoa wa Arusha kwa pesa zao za mfukoni Joshua Nasari na Godbless Lema zimeanza kufanya kazi tangu awamu iliyopita na juzi zimeshiriki kikamilifu kubeba maiti za watoto wetu wa shule waliopata ajari kule Arusha,Lakini leo wakati wa kuaga miili ya watoto hao ambulace hizo zimeamuliwa ziondolewe mara moja uwanjani hapo kwa kuwa zilinunuliwa na wabunge wa upinzani na zina majina ya wabunge wa upinzani waliozinunua.
Yani hawakuishia kumbagua mhe.lema kutoa salam za rambirambi kwa wananchi wake bali wamebagua hadi gari alilonunua kwa pesa zake kwa ajili ya kuwasaidia wananchi kwenye jimbo lake.Gari hizi zimekuwa zikiwahudumia wananchi wa mkoa wa arusha bila kubagua itikadi za vyama pamoja na kuwa zilinunuliwa na wabunge wa upinzani,,LAKINI Leo gari hizi zimebaguliwa kwa kuwa tu zilinunuliwa na wabunge ambao sio wa chama chao.
Ninalaani vikali ubaguzi huu,,,na kila mwananchi apige kelele kupinga ubaguzi huu nchi ,hii ilijengwa kwa misingi ya umoja,Viongozi wanapaswa kujua kuwa adui wa taifa hili ni UMASKINI,UJINGA NA MARADHI lakini viongozi wetu wameacha kupambana na maadui hao wao wanapambana na wapinzani wao kisiasa Il est de la folie à grande échelle viongozi wa namna hii wanapatikana hapa kwetu na sudani kusini pekee dunia nzima.
Lakini nawaonya ipo siku mbegu hii ya kibaguzi mnayoipanda zidi ya wapinzani itakuja kuwaletea matatizo makubwa na mtaliingiza taifa kwenye matatizo makubwa sana na mwisho wa siku mtatoka kwenye viyoyozi na kwenda kuishi kwa lazima segerea na keko,nawashauri acheni mara moja ubaguzi huu.
R.I.P watoto wetu
mdude nyagali
sumu ya nyigu