Arusha: Maduka yote ya kubadilishia fedha za kigeni(Forex) yasimamiwa na JWTZ, wananchi watakiwa kwenda Benki Kuu

Benki Kuu itoe actual market rate hakutakuwa na shida na pia wakumbuke kufungua matawi mengi kila mahali.
 
Maduka ya kubadilisha fedha za kigeni Arusha karibu yote yako chini ya ulinzi wa wanajeshi wakiwa na mitutu kwa kile kinachoitwa operation.

Its truly happening in Arusha.

--------
Ulinzi mkali umeimarishwa kwenye maduka karibu yote yanayohusika na biashara ya kubadilisha fedha(Forex)

Yadaiwa kuna oparesheni maalum inayoendelea ambayo hadi sasa haijafahamika inahusu nini

Aidha, wanaotaka kubadili fedha watakiwa kwenda kupata huduma hiyo Benki Kuu
Ina maana kuna watu wameshukiwa kutakatisha fedha!
Na huenda wengine wanaendesha biashara bila utimilifu!
Hawaja comply na sheria ya fedha.
Tuvumiliane tu nchi inyooshwe tukumbuke ilipinda kuanzia kwenye ramani.

HM
 
Anaandika Malisa huko FB
Nasikia huko Jamhuri ya watu wa kusadikika wamekagua benki kuu yao wakaona hakuna pesa za kigeni. Yani reserve ya pesa za kigeni ni ndogo sana kiasi kwamba haitoshi kufanya purchase nje kwa miezi kadhaa ijayo. Kwahiyo wameamua kwenda kuzitafuta kwenye maduka ya kubadili fedha. Wanaamini zimefichwa huko. Kwamba wenye maduka wamezibana na hawataki kuziachia. Kwahiyo wameamua kwenda kuzisaka kwa mitutu ya bunduki. Songombingo za Kaboka mchizi.!

Ngoja niwape shule kidogo. Sababu za msingi za kupotea kwa 'dola' katika nchi hiyo ni hizi hapa.

#Mosi; nchi huwa inapata pesa za kigeni kwa kuuza bidhaa na huduma nje. Lakini nchi ya kusadikika imezuia kuuza mazao nje. Nasikia huko mahindi yanaozea ndani, mbaazi ndo kwisha habari yake, tangawizi hata ukitupa watu hawaokoti. Hivyo vyote vilikuwa vina soko kubwa nje ya nchi na vinaingizia nchi hiyo pesa nyingi za kigeni. Lakini mfalme wao akapiga marufuku wasiuze nje. Leo wanamtafuta mchawi. Maajabu.!

Koro-show nasikia nayo imezuiwa kuuzwa nje. Serikali ktk nchi ya kusadikika imesema itanunua yote. That means hakuna pesa zozote za kigeni nchi hiyo itaingiza. Kama makampuni binafsi kutoka nje yangeruhusiwa kununua yangekuja na 'dola'. Wangechange na kupata madafu ya kulipa wakulima. Hayo 'madola' yaliyochenchiwa yangeingia kwenye mabenki na hatimaye benki kuu. Kwahiyo serikali ingeongeza reserve yake ya pesa za kigeni. Lakini wameamua kununua koro-show zote wenyewe, leo wanatafuta dola kwa mitutu?

Na mfalme wao amesema akikosa soko atamwambia kila mtu kwenye nchi hiyo ale ratili mbili za koro-show. Hizo ratili mbili kwa kila raia zinanunuliwa kwa pesa ya madafu na zitaliwa na raia wa humohumo ndani. Kwahiyo koro-show zote zinaweza zikaisha bila kuingiza hata dola moja kwenye nchi hiyo. Hii ni biashara kichaa ktk historia ya biashara duniani.!

#Pili; nchi inapata pesa za kigeni kupitia mikopo na misaada mbalimbali ya kimataifa kama vile kutoka Benki ya dunia, IMF, na mataifa wahisani kama Marekani, Umoja wa Ulaya etc. Sasa nasikia Benki ya dunia imesitisha mikopo na misaada kwenye nchi hiyo. Baadhi ya mashirika ya kimataifa nayo yamesitisha shughuli zake huko. Umoja wa Ulaya nao unafikiria kusitisha misaada yote kwa nchi hiyo, na tayari balozi wao ameshafurushwa. Kwahiyo hakuna 'foreign grant wala loan' ambayo inaingiza pesa za kigeni kwenye nchi hiyo kwa sasa. Lakini wanaenda kutafuta pesa za kigeni kwa AK47 kwenye maduka ya kubadili fedha. Hekaya za Abunuasi.!

#Tatu; Nchi inapata pesa za kigeni kwa kukaribisha wawekezaji wa kigeni kwa wingi (Foreign investors). Mwekezaji akienda kujenga kiwanda katika nchi fulani haendi na pesa za madafu, anaenda na dola. Akifika huko hizo dola anazibadili na kupewa madafu. Dola zinaingia kwenye system na kuongeza reserve ya pesa za kigeni.

Lakini kwenye nchi ya kusadikika foreign investors wanafokewa na kunyang'anywa passport. Kiongozi akishashiba 'ugali tembele' anaropoka tu 'mnyang'anyeni passport'. Matokeo yake wawekezaji wanahamisha mitaji na kwenda kuwekeza kwenye nchi nyingine. Leo nchi ya kusadikika iko busy kutafuta nani kaficha pesa za kigeni kwenye sandarusi. Harakati za pimbi.!

#Nne; nchi inaingiza pesa za kigeni kutokana na jinsi inavyouza utaalamu wake nje ya nchi. Lakini kwenye nchi ya kusadikika wataalamu wamezuiwa kwenda kufanya kazi nje. Serikali yao imesema mtu yeyote anayepata kazi nje ya nchi inabidi aombe kibali kwanza akiambatanisha mkataba wa ajira. Na serikali inaweza kumruhusu au kumkatalia. Leo serikali hiyohiyo ipo 'busy' kutafuta dola kwenye maduka ya wahindi. Futuhi.!

#Tano; Njia nyingine ya kumaintain pesa za kigeni ni kuregulate kiwango cha kununua na kuuza bidhaa na huduma nje ya nchi. Unatakiwa kuuza zaidi kuliko unavyonunua. Hakikisha unanunua nje vitu vya muhimu tu. Vingine vitengeneze mwenyewe. Hii ni kwa sababu kila unapoagiza bidhaa yoyote nje ya nchi unapunguza reserve yako ya pesa za kigeni. Lakini kanchi ka kusadikika kanatumia reserve yake ya pesa za kigeni kununulia hadi toilet paper, halafu leo kanatafuta pesa zilikofichwa. Inna Lillahi wa inna ilayhi raji'un.!

Malisa GJ
 
Mbona wajeda ndo wanalinda kaogpa raia wakakamavu watalamba rushwa na kuziweka kwenye kofia zao
 
Yes credible intel inaweza kuwa chochote kile. Na si tu uhalifu.
Ukiona askar mahali kama hapo haimaanish ni waalifu. Otherwise wangebebwa na kupelekwa ndani jion hii na maduka kufungwa.

Wahalifu pia si wajinga. Its a game of cat and mouse

Jeshi hapo linafanya kazi yake vizuri tu
 
Sielewi kesho kutakuwa na operesheni gani tena humu nchini, kila siku lazima litaibuka jambo jipya la kushangaza.
 
Anaandika Malisa huko FB
Nasikia huko Jamhuri ya watu wa kusadikika wamekagua benki kuu yao wakaona hakuna pesa za kigeni. Yani reserve ya pesa za kigeni ni ndogo sana kiasi kwamba haitoshi kufanya purchase nje kwa miezi kadhaa ijayo. Kwahiyo wameamua kwenda kuzitafuta kwenye maduka ya kubadili fedha. Wanaamini zimefichwa huko. Kwamba wenye maduka wamezibana na hawataki kuziachia. Kwahiyo wameamua kwenda kuzisaka kwa mitutu ya bunduki. Songombingo za Kaboka mchizi.!

Ngoja niwape shule kidogo. Sababu za msingi za kupotea kwa 'dola' katika nchi hiyo ni hizi hapa.

#Mosi; nchi huwa inapata pesa za kigeni kwa kuuza bidhaa na huduma nje. Lakini nchi ya kusadikika imezuia kuuza mazao nje. Nasikia huko mahindi yanaozea ndani, mbaazi ndo kwisha habari yake, tangawizi hata ukitupa watu hawaokoti. Hivyo vyote vilikuwa vina soko kubwa nje ya nchi na vinaingizia nchi hiyo pesa nyingi za kigeni. Lakini mfalme wao akapiga marufuku wasiuze nje. Leo wanamtafuta mchawi. Maajabu.!

Koro-show nasikia nayo imezuiwa kuuzwa nje. Serikali ktk nchi ya kusadikika imesema itanunua yote. That means hakuna pesa zozote za kigeni nchi hiyo itaingiza. Kama makampuni binafsi kutoka nje yangeruhusiwa kununua yangekuja na 'dola'. Wangechange na kupata madafu ya kulipa wakulima. Hayo 'madola' yaliyochenchiwa yangeingia kwenye mabenki na hatimaye benki kuu. Kwahiyo serikali ingeongeza reserve yake ya pesa za kigeni. Lakini wameamua kununua koro-show zote wenyewe, leo wanatafuta dola kwa mitutu?

Na mfalme wao amesema akikosa soko atamwambia kila mtu kwenye nchi hiyo ale ratili mbili za koro-show. Hizo ratili mbili kwa kila raia zinanunuliwa kwa pesa ya madafu na zitaliwa na raia wa humohumo ndani. Kwahiyo koro-show zote zinaweza zikaisha bila kuingiza hata dola moja kwenye nchi hiyo. Hii ni biashara kichaa ktk historia ya biashara duniani.!

#Pili; nchi inapata pesa za kigeni kupitia mikopo na misaada mbalimbali ya kimataifa kama vile kutoka Benki ya dunia, IMF, na mataifa wahisani kama Marekani, Umoja wa Ulaya etc. Sasa nasikia Benki ya dunia imesitisha mikopo na misaada kwenye nchi hiyo. Baadhi ya mashirika ya kimataifa nayo yamesitisha shughuli zake huko. Umoja wa Ulaya nao unafikiria kusitisha misaada yote kwa nchi hiyo, na tayari balozi wao ameshafurushwa. Kwahiyo hakuna 'foreign grant wala loan' ambayo inaingiza pesa za kigeni kwenye nchi hiyo kwa sasa. Lakini wanaenda kutafuta pesa za kigeni kwa AK47 kwenye maduka ya kubadili fedha. Hekaya za Abunuasi.!

#Tatu; Nchi inapata pesa za kigeni kwa kukaribisha wawekezaji wa kigeni kwa wingi (Foreign investors). Mwekezaji akienda kujenga kiwanda katika nchi fulani haendi na pesa za madafu, anaenda na dola. Akifika huko hizo dola anazibadili na kupewa madafu. Dola zinaingia kwenye system na kuongeza reserve ya pesa za kigeni.

Lakini kwenye nchi ya kusadikika foreign investors wanafokewa na kunyang'anywa passport. Kiongozi akishashiba 'ugali tembele' anaropoka tu 'mnyang'anyeni passport'. Matokeo yake wawekezaji wanahamisha mitaji na kwenda kuwekeza kwenye nchi nyingine. Leo nchi ya kusadikika iko busy kutafuta nani kaficha pesa za kigeni kwenye sandarusi. Harakati za pimbi.!

#Nne; nchi inaingiza pesa za kigeni kutokana na jinsi inavyouza utaalamu wake nje ya nchi. Lakini kwenye nchi ya kusadikika wataalamu wamezuiwa kwenda kufanya kazi nje. Serikali yao imesema mtu yeyote anayepata kazi nje ya nchi inabidi aombe kibali kwanza akiambatanisha mkataba wa ajira. Na serikali inaweza kumruhusu au kumkatalia. Leo serikali hiyohiyo ipo 'busy' kutafuta dola kwenye maduka ya wahindi. Futuhi.!

#Tano; Njia nyingine ya kumaintain pesa za kigeni ni kuregulate kiwango cha kununua na kuuza bidhaa na huduma nje ya nchi. Unatakiwa kuuza zaidi kuliko unavyonunua. Hakikisha unanunua nje vitu vya muhimu tu. Vingine vitengeneze mwenyewe. Hii ni kwa sababu kila unapoagiza bidhaa yoyote nje ya nchi unapunguza reserve yako ya pesa za kigeni. Lakini kanchi ka kusadikika kanatumia reserve yake ya pesa za kigeni kununulia hadi toilet paper, halafu leo kanatafuta pesa zilikofichwa. Inna Lillahi wa inna ilayhi raji'un.!

Malisa GJ
Dereva wa basi kanywa gongo Lita 5, Abiria wanajua ila basi lipo kwenye mwendokasi. Matumaini pekee ni Muumba
 
Pesa zote walikomba kwa ajili ya kurudia chaguzi kuwanunua madiwani, wabunge, Akiba yote BOT wameikomba kienyeji kwa kuchukua pesa bila idhini ya Bunge, CCM wakitaka pesa wanaenda kuchukua na Bashite akitaka pesa anaenda kuchukua, ujenzi wa Reli na ununuzi wa ndege kwa cash ndiyo ulimaliza akiba ya Dola huko BOT hata oparation nyingi za hovyo hovyo zimechangia Dola kukombwa BOT .
 
Anaandika Malisa huko FB
Nasikia huko Jamhuri ya watu wa kusadikika wamekagua benki kuu yao wakaona hakuna pesa za kigeni. Yani reserve ya pesa za kigeni ni ndogo sana kiasi kwamba haitoshi kufanya purchase nje kwa miezi kadhaa ijayo. Kwahiyo wameamua kwenda kuzitafuta kwenye maduka ya kubadili fedha. Wanaamini zimefichwa huko. Kwamba wenye maduka wamezibana na hawataki kuziachia. Kwahiyo wameamua kwenda kuzisaka kwa mitutu ya bunduki. Songombingo za Kaboka mchizi.!

Ngoja niwape shule kidogo. Sababu za msingi za kupotea kwa 'dola' katika nchi hiyo ni hizi hapa.

#Mosi; nchi huwa inapata pesa za kigeni kwa kuuza bidhaa na huduma nje. Lakini nchi ya kusadikika imezuia kuuza mazao nje. Nasikia huko mahindi yanaozea ndani, mbaazi ndo kwisha habari yake, tangawizi hata ukitupa watu hawaokoti. Hivyo vyote vilikuwa vina soko kubwa nje ya nchi na vinaingizia nchi hiyo pesa nyingi za kigeni. Lakini mfalme wao akapiga marufuku wasiuze nje. Leo wanamtafuta mchawi. Maajabu.!

Koro-show nasikia nayo imezuiwa kuuzwa nje. Serikali ktk nchi ya kusadikika imesema itanunua yote. That means hakuna pesa zozote za kigeni nchi hiyo itaingiza. Kama makampuni binafsi kutoka nje yangeruhusiwa kununua yangekuja na 'dola'. Wangechange na kupata madafu ya kulipa wakulima. Hayo 'madola' yaliyochenchiwa yangeingia kwenye mabenki na hatimaye benki kuu. Kwahiyo serikali ingeongeza reserve yake ya pesa za kigeni. Lakini wameamua kununua koro-show zote wenyewe, leo wanatafuta dola kwa mitutu?

Na mfalme wao amesema akikosa soko atamwambia kila mtu kwenye nchi hiyo ale ratili mbili za koro-show. Hizo ratili mbili kwa kila raia zinanunuliwa kwa pesa ya madafu na zitaliwa na raia wa humohumo ndani. Kwahiyo koro-show zote zinaweza zikaisha bila kuingiza hata dola moja kwenye nchi hiyo. Hii ni biashara kichaa ktk historia ya biashara duniani.!

#Pili; nchi inapata pesa za kigeni kupitia mikopo na misaada mbalimbali ya kimataifa kama vile kutoka Benki ya dunia, IMF, na mataifa wahisani kama Marekani, Umoja wa Ulaya etc. Sasa nasikia Benki ya dunia imesitisha mikopo na misaada kwenye nchi hiyo. Baadhi ya mashirika ya kimataifa nayo yamesitisha shughuli zake huko. Umoja wa Ulaya nao unafikiria kusitisha misaada yote kwa nchi hiyo, na tayari balozi wao ameshafurushwa. Kwahiyo hakuna 'foreign grant wala loan' ambayo inaingiza pesa za kigeni kwenye nchi hiyo kwa sasa. Lakini wanaenda kutafuta pesa za kigeni kwa AK47 kwenye maduka ya kubadili fedha. Hekaya za Abunuasi.!

#Tatu; Nchi inapata pesa za kigeni kwa kukaribisha wawekezaji wa kigeni kwa wingi (Foreign investors). Mwekezaji akienda kujenga kiwanda katika nchi fulani haendi na pesa za madafu, anaenda na dola. Akifika huko hizo dola anazibadili na kupewa madafu. Dola zinaingia kwenye system na kuongeza reserve ya pesa za kigeni.

Lakini kwenye nchi ya kusadikika foreign investors wanafokewa na kunyang'anywa passport. Kiongozi akishashiba 'ugali tembele' anaropoka tu 'mnyang'anyeni passport'. Matokeo yake wawekezaji wanahamisha mitaji na kwenda kuwekeza kwenye nchi nyingine. Leo nchi ya kusadikika iko busy kutafuta nani kaficha pesa za kigeni kwenye sandarusi. Harakati za pimbi.!

#Nne; nchi inaingiza pesa za kigeni kutokana na jinsi inavyouza utaalamu wake nje ya nchi. Lakini kwenye nchi ya kusadikika wataalamu wamezuiwa kwenda kufanya kazi nje. Serikali yao imesema mtu yeyote anayepata kazi nje ya nchi inabidi aombe kibali kwanza akiambatanisha mkataba wa ajira. Na serikali inaweza kumruhusu au kumkatalia. Leo serikali hiyohiyo ipo 'busy' kutafuta dola kwenye maduka ya wahindi. Futuhi.!

#Tano; Njia nyingine ya kumaintain pesa za kigeni ni kuregulate kiwango cha kununua na kuuza bidhaa na huduma nje ya nchi. Unatakiwa kuuza zaidi kuliko unavyonunua. Hakikisha unanunua nje vitu vya muhimu tu. Vingine vitengeneze mwenyewe. Hii ni kwa sababu kila unapoagiza bidhaa yoyote nje ya nchi unapunguza reserve yako ya pesa za kigeni. Lakini kanchi ka kusadikika kanatumia reserve yake ya pesa za kigeni kununulia hadi toilet paper, halafu leo kanatafuta pesa zilikofichwa. Inna Lillahi wa inna ilayhi raji'un.!

Malisa GJ
Hizi dollar 500 nilizoficha kwenye kibubu changu, asije akawatuma JWTZ kuzichukua, ngoja nipeleke kwa wazungu kuliko nimpe huyu mhuni tu.
 
Back
Top Bottom