Arusha: Madiwani waliotimuliwa na CHADEMA wabwagwa mahakamani!

Kama habari hii ni ya kweli basi si Mkuchika pekee aliyeumbuka bali muumbukaji mkuu ni PM.
Pinda ndio wakwanza kutoa ushauri kuwa waende Mahakamani wakati anajua fika kufukuzwa Chamani kuna vyombo ndani ya chama vya kusikiliza rufani na sio mahakama.
Na hasa huyu PM kilaza, yeye alishauri waende mahakamani, hajui alichokuwa anakiongea. AIBU YAO MAGAMBA.
 
Hongera Mahakama ya Arusha, mmeonyesha kuwa manaifahamu kazi yenu licha ya pressure kubwa mliyokuwa nayo. Kwa maana hiyo, historia yenu imeandikwa na mtaheshimika na vizazi vyote vya Tanzania vitakavyokuja.
 
Good news. Hapa makongoro mahanga tumbo moto, kwani hata alipojaribu kufanya njama mahakama itupilie mbali kesi ya fred ameangukia pua.
Sasa atapopata taarifa hii ya arusha, kamasi zitammwagika huyo, balaa.
Hebu tupewe jimbo letu segerea hapa.
Viva chadema, viva TANZANIA
 
Wapi zitto igunga ili mwendeleze ushindi? Au yeye ni mgeni rasmi wa kwenda kufunga mkutano kwa kuwa yeye ni mkubwa kuliko Mbowe na Slaa? Kwa sasa yuko Busy?
 
Sasa hivi hapa kwenye jiji la Arusha ni cherekochereko kwenye mzunguko wa clock Tower wafuasi wa chama cha Chadema wanasherehekea.

kweli we ni ndallo.

unapost thread halafu unakuwa wa kwanza kuipa uhai? Ungetulia ukasubiri wadau waseme, halafu wewe ungejibu hoja zao.
sio lazima ukubaliane na mimi, ni mtazamo wangu tu
 
Aibu yake Mkuchika!


Sio aibu yake tu, kama Mh. Waziri hajui majukumu yake, wala haifahamu Katiba ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania aliyo apa kuilinda na kuitetea, Ni wakati muaafaka akajiuzuru, na kupisha watu wenye nia thabiti ya kuilinda Katiba na kusimamia utawala wa sheria.
 
Sasa hivi hapa kwenye jiji la Arusha ni cherekochereko kwenye mzunguko wa clock Tower wafuasi wa chama cha Chadema wanasherehekea.

Ndallo,
Si usubiri wachangiaje waanze kuchangia na wewe utakuwa unaongezea kulingamna na michango yao?
 
Ile kesi iliyokua inawakabili wale madiwani watano Arusha hatimaye hukumu imeshatekelezwa na wameshindwa na sasa uchaguzi wa madiwani Arusha utarudiwa tena! Souce Mahakama kuu Arusha.

Ndallo! Tunashukuru sana kwa hili kwani nilitamani sana ningekuwepo lakini kutokana na sababu iliyokuwa nje ya uwezo wangu nimeshindwa kufika. Na ndiyo maana naikubali uwepo wa WanaJF ya kwmb kila kinachojiri unapata.
 
Nasubiri comments kutoka kwa Radhia, Mwita25, Rejao, Malariasugu, na kigazeti cha Uhuru.
 
Aibu kwa waziri mkuchika, Hii ni kuonesha kwamba Chadema sasa haitazuilika kwa mtindo huo. Wale jamaa itabidi wahame jiji la Arusha. Nahisi huko ndiko alikokuwepo Lema. Kazi kweli.

Jamani Mallah na zile pick up zake za Peugeot 404 simwoni tena mitaa ya Kijenge na Kimandolu. Kwani kama na hukumu ndo hiyo hata ile baa ya pentagon itakufa. Naamini hata familia itasononeka sana. HAYA NDIO MADHARA YA KUTAMANI UBUNGE UKIWA DIWANI!!!!!!
 
Back
Top Bottom