Arusha: Madiwani waliotimuliwa na CHADEMA wabwagwa mahakamani!

Ndallo

JF-Expert Member
Oct 1, 2010
7,623
4,281
Ile kesi iliyokua inawakabili wale madiwani watano Arusha hatimaye hukumu imeshatekelezwa na wameshindwa na sasa uchaguzi wa madiwani Arusha utarudiwa tena!

Souce Mahakama kuu Arusha.

MAHAKAMA ya hakimu mkazi Arusha imetupilia mbali kesi iliyofunguliwa na madiwani watano waliofukuzwa kwenye Chama Cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA) ambapo imedaiwa kuwa madiwani hao wanatakiwa kulipa garama mbalimbali ambazo zimetumika katika kesi hiyo.

Hapo awali Madiwani hao waliwasilisha pingamizi ambapo pingamizi hilo lilidai kuwa madiwani hao hawakutendewa haki na chama hicho ambapo chama hicho kiliwafukuza.

Hayo yamedhibitika leo katika mahakama ya hakimu mkazi ya jiji la arusha ambapo kesi hiyo ilikuwa ikisikilizwa na Hakimu Hawa Mguruta ambapo alisema kuwa alifikia uamuzi huo baada ya kupitia hoja nne za pingamizi zilizowasilishwa mahakamani hapo na mawakili wadaiwa, Method Kimomogoro na Albert Msando na majibu ya wakili wa wadai,, Severine Lawena.

Katika shauri hilo la madai namba 17 la mwaka 2011 washitakiwa walikuwa ni Chama Cha Demokrasia na Mendeleo (CHADEMA) na Freeman Mbowe huku wadai wakiwa ni madiwani waliofukuzwa kwenye chama hicho na kata zao kwenye mabano ni Naibu Meya , Estomii Mallah ( Kimandolu) , John Bayo (Elerai), Ruben Ngowi ( Themi), Rehema Mohamed (Viti Maalum) na Charles Mpanda (Kaloleni).

Aidha Hakimu Mguruta alisema kuwa anakubaliana na hoja za mawakili wa wadai kuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kuchunguza maamuzi ya chombo binafsi kama ilivyo kamati kuu ya Chadema ambapo walibainisha kuwa chombo chenye mamlaka hayo ni mahakama kuu .

"ni kwamba nakubaliana na hoja kuwa Chadema haiwezi kushitakiwa kwa jina lake kwani jina hilo halina uhai kisheria hivyo haiwezi kushitaki wala kushitakiwa kwa mujibu wa sheria'alieleza Hakimu Mguruta.

Hakimu Mguruta alisema kuwa anakubaliana na hoja ya mawakili hao kuwa Mwenyekiti wa Taifa wa Chama hicho (Mbowe) hawezi kushitakiwa binafsi alipaswa kushitakiwa kwa nafasi yake ua Uenyekiti wa Taifa vinginevyo hataweza kutekeleza maelekezo ya mahakama hiyo ndani ya Chadema

"Mbowe alipaswa kushtakiwa kwa nafasi yake ya uenyekiti wa Taifa kwani endapo ataondolewa kwenye nafasi hiyo au kujiuzulu hataweza kutekeleza maamuzi ya mahakama kwani hataweza kuendesha na kusimamia maamuzi ya vikao ndani ya chadema" alisema hakimu mguruta .

Katika hatua nyingine Hakimu huyo alikubaliana na hoja kuwa kesi hiyo imefika mahakamani hapo ikiwa imepitwa na wakati kwani tayari madiwani hao walishakata rufaa kwenye baraza kuu la Chadema hivyo kesi hiyo imepoteza maana huku akiongeza kuwa mahakama kuu ndiyo yenye uwezo wa kupitia maamuzi yaliyofanywa na na vikao ndani ya taasisi lakini haiwezi kuhoji au kuamua juu ya taratibu za ndani za chama husika.

Wakati maamuzi hayo yakitolewa madiwani watatu kati ya watano waliofungua kesi hiyo walikuwa mahakamani hapo ambao ni Diwani wa kata ya Elerai Bw John Bayo , Naibu Meya wa jiji la Arusha ambaye pia ni diwani wa a kata ya Kimandolu, Bw Estomih Mallah ambapo walipotakiwa kutoa maoni yao mara baada ya kikao cha mahakama kumalizika walisema kuwa hawana maoni ya kuongea na vyombo vya habari.

Aidha iliwabidi madiwani hao waliofungua kesi hiyo kusubiri ndani ya chumba cha mahakama mpaka mashabiki hao wa Chadema walipotoka nje ndipo nao wakatoka ingawa waliendelea kukaa kwenye maeneo hayo ya mahakama mpaka wanachama hao walipoondoka kwa maandamano na mbunge wa Arusha Mjini, Godbless lema.

Hata hivyo katika hatua nyingine polisi wenye silaha na mabomu ya machozi wakiwa kwenye magari mawili ya Polisi yenye namba za usajili PT 1844 na PT 0746 walifika na kuwaamuru wanachama hao kutawanyika mbele ya jengo la ofisi za mkuu wa wilaya ya Arusha zilipo ofisi za mbunge huyo ambapo walitii na kuondoka.
 

lukindo

JF-Expert Member
Mar 20, 2010
8,470
9,015
ukweli unaweza kukaa hata miaka 100,000++ (zaidi ya laki moja) lakini huwa haubadiliki kuwa uongo! Kwa umri wake sidhani kama atakuwa na la kujifunza lakini vizazi vijavyo vitajifunza kitu hapa.
Aibu yake Mkuchika!
Huwa napenda sana wimbo huu kila ninapousikia, hizi ni baadhi ya haya chache.
Wind of Change
….
…..
The world is closing in
Did you ever think
That we could be so close, like brothers
The future's in the air
Can feel it everywhere
Blowing with the wind of change

Take me to the magic of the moment
On a glory night
Where the children of tomorrow dream away
In the wind of change
…
…
The wind of change
Blows straight into the face of time
Like a storm wind that will ring the freedom bell
For peace of mind
Let your balalaika sing
What my guitar wants to say
…….
……
 

Mzee wa Rula

JF-Expert Member
Oct 6, 2010
8,173
3,330
Ni kweli wale madiwani kama uamuzi ulikuwa na shinikizo basi watalia sana, maana mahakama imepigilia msumari kuwa kama wanataka wakate rufaa kwenye CC ya chama na si mahakamanio tena. Mimi nitoe pongezi kwa hakimu kupractice weledi wake badala ya kuburuzwa! Hiyo ni changamoto kwa hao madiwani kuwa hakuna aliye maarufu kuliko chama. Chama ndiyo kimewafikisha hapo, hivyo hawakutakiwa kubweteka na kuitunishia misuli CC.
Ngoja tuone Mkuchika naye atasemjae baada ya hukumu hiyo.
 

Chakaza

JF-Expert Member
Mar 10, 2007
37,936
66,155
Kama habari hii ni ya kweli basi si Mkuchika pekee aliyeumbuka bali muumbukaji mkuu ni PM.
Pinda ndio wakwanza kutoa ushauri kuwa waende Mahakamani wakati anajua fika kufukuzwa Chamani kuna vyombo ndani ya chama vya kusikiliza rufani na sio mahakama.
 

POMPO

JF-Expert Member
Mar 12, 2011
6,690
2,397
Aibu ya Pinda aliewashauri waende huko! Bado Shibuda. Naanza kuwa na iman na mahakama safi kawa wazee! Chama cha magamba kisiwaendesh endeshe!
 

Gurti

JF-Expert Member
Nov 19, 2010
211
59
Chadema Arusha wakiongozwa na Godbless Lema wana mikakati ya kuweka mawakili wazuri na kushinda Kesi. ccm Igunga akina Machemba mwagalu wanafanya mapenzi na wake za watu. kazi kweli.
 

Gurti

JF-Expert Member
Nov 19, 2010
211
59
Wapi zitto igunga? Au yeye ni mgeni rasmi wa kwenda kufunga mkutano kwa kuwa yeye ni mkubwa kuliko Mbowe na Slaa? Kwa sasa yuko Busy?
 
20 Reactions
Reply
Top Bottom