Arusha: MADIWANI WALIOTIMULIWA CDM KUGOMBEA KUPITIA NCCR

Mzito Kabwela

JF-Expert Member
Nov 28, 2009
18,857
7,615
Nipo Arusha hivi sasa kikazi lakini kwakuwa Jiji hili ni ngome ya makamanda wa CHADEMA sikusita kufanya kautafiti kangu kadogo na huu ndio UWELI.

Kwa mujibu wa Bwana Bayo ambaye alikuwa Diwani wa kata ya Elerai anasema mbali na kukata rufaa juu ya maamuzi ya mahakama yaliyotolewa hivi karibuni dhidi yao lakini madiwani wote waliotimuliwa na CHADEMA wanategemea kugombea tena kupitia chama cha NCCR-MAGEUZI. Na kwa mujibu wake huyo Bayo, mkakati madhubuti unaandaliwa kuhakikisha wanashinda uchaguzi huo.

Nimejiuliza maswali mengi, mojawapo ni hili, wataamuaje kugombea kwa tiketi ya NCCR wakati wanakata rufaa? Je rufaa yao ikikubaliwa na mahakama ikawapa haki ya kuendelea kuwa madiwani wa Chadema mpango wao wa kuhamia NCCR utayeyuka au washajua mbali na kukata rufaa lakini watachemsha tena?
 
Lengo ni kupunguza kura za upinzani, viti viende CCM. Wanajua wakiendea wao CCM, viti vitarudi CDM
 
Wazee wa kugoma....tuwape mkono wa buriani ktk kifo cha kisiasa!!
 
madiwani njaaa hao..waende kwa Pinda na Mkuchika wakapewe kazi ya kusafisha ofisi
 
Hao kwish_nei! Tatizo walidhani wao ni Bora kuliko chama kilichowadhamini. Na waende NCCR halafu wasubiri waone cha moto!
 
Kwani nccr hawakuwa na wanachama kabla? Au taratibu za kugombea nafasi kwao zikoje? Mtu anateuliwa na chama baada ya mchujo au mtu anaweza kutoka hata ccm akaenda tume
akawaambia kwamba nimekuja kugombea kwa tiketi ya nccr wakamruhusu tu!
 
Kama vipi waungane na Mpendazoe, hawa wote ni wahanga wa kisiasa.
 
Mnataka kuwanyang'anya na haki zao za KIKATIBA na KIRAIA za NCHI hii? Acheni wagombee wanakotaka. Binafsi naichukia sana ile sheria iliyowavua UDIWANI kwani naamini kwa siasa za nchi hii anachaguliwa MTU sio CHAMA.
 
Back
Top Bottom