Waliojiuzulu udiwani Meru wabwagwa kura za maoni CCM, wamwangukia Magufuli

Duniahadaa

JF-Expert Member
Oct 16, 2017
336
677
Katika kata zote ni Emmanuel Mollel peke yake wa kata ya MAKIBA aliyeibuka kidedea, wengine wote katika kata zao wameangukia pua maskini!

Kituko kikubwa ni kata ya Ambureni Japhet Jackson ambaye NAYE alijiuzulu udiwani kupitia CHADEMA kwa ahadi ya kupewa nafasi ya kugombea ndani ya CCM, yeye alipata kura 4 (kati ya hizo 2 alizawadiwa na mwenyekiti wa kikao ili kuficha aibu).

Ndugu huyu sasa anahaha kufanya mazungumzo na viongozi wa wilaya akiwakumbusha ahadi aliyotoa Mwenyekiti wa CCM John Magufuli, stadium kuwa "tutawarudisha hawa hawa" Kura zilipigwa jana lakini leo ameamkia wilayani na kufanya mazungumzo na kamati ya siasa apate tiketi ya kugombea udiwani aliouachia.

Wajumbe wa kamati ya siasa wana mkejeli kuwa atajiju, lakini wengine wapo bega kwa bega na yeye.

Pia PCCB walifika katika shule yake kuulizia kama kuna nafasi ya kuleta watoto (walijifanya wazazi wahamiaji), jamaa akawaambia shule ilifungwa. Itakumbukwa kuwa moja ya ahadi alizopewa ili kuachia udiwani ni kufunguliwa kwa shule yake ambayo ameijenga kwenye tindiga ambayo serikali waliifungu.

Lakini baada issue ya Nassary kubumburuka, wakaifunga haraka, hivyo PCCB walipokuja kwake aligundua mtego akategua. Balaa hii!!! udiwani hana, shule bado imefungwa.

Nitaendela kuwajuza.
 
CCM hawana rafiki wa kudumu ni pale wanapotaka wakutumie ndipo wanapokufanya rafiki yao,wakishamaliza kukutumia hawana habari na wao tena.
 
Back
Top Bottom