Arusha: Madiwani wa jiji la Arusha walia na Mkurugenzi wa jiji

Jim007 2

JF-Expert Member
Dec 28, 2012
395
247
Katika kikao maalum cha baraza la madiwani cha tarehe 23 Desemba 2016 kilichokuwa kujadili agenda ya ukodishwaji vibanda zaidi ya 1000 vya stendi na Soko kuu .

Kikao hicho kilichohuhudhuriwa na katibu tawala mkoa RAS na katibu tawala wilaya DAS kilianza kwa Tafrani kubwa baada ya baadhi ya madiwani hao kugoma kikao kisiendelee hadi waelezwe kwanini mkurugenzi huyo aliyefyeka posho za madiwani walizokuwa wanajilipa kuwa mamlaka hiyo kaitoa wapi wakati ametukuta na posho zetu walihoji.

Awali walisema mkuu wa mkoa, wilaya na mkurugenzi maarufu kama GDK( yaani Gambo, Daqarro na Kihamia )wanaingilia mamlaka yao ambapo mkurugenzi huyo mwenye misimamo mikali alifyeka posho mbalimbali za madiwani na watumishi na hata za kazi zingine alizodai hazina tija na kuamua kuwalipa walimu madeni ya nyuma huku akiyazibia masikio maoni ya madiwani hao.

Hali hiyo imezua Uadui mkubwa ambao umesababisha madiwani hao kujifungia kwa nyakati tofauti mara kwa mara kupanga namna ya kumdhibiti mkurugenzi huyo pamoja na GDK kwa ujumla ambapo mara kadhaa walimtengenezea tuhuma feki kupitia mitandao ya kijamii hasa jamii forums.

Madiwani hao hata hivyo wamepata pigo la mwaka baada ya leo kulazimishwa kupitisha azimio la kutoa notisi ya miezi 3 kwa wapangaji hao wa vibanda kuondoka ili vitangazwe upya kwa mujibu wa sheria ya manunuzi ya umma tofauti na mazoea ya kuwapangisha watu kinyemela bila mikataba kwa maslahi yao ya kisiasa na rushwa ambapo baadhi ya wapangaji walitoa hongo hadi million 3 ili wapatiwe upendeleo.

Baadhi ya madiwani wanahusika na uchafu huo ni wale wa kata za Ngarenaro, Unga limited, Levolosi, Moivaro,Moshono,na Sokoni wani nm ambaye pia ni Meya na wengineo.

Hata hivyo leo wamekiri kwamba mkurugenzi huyo wa jiji la Arusha Athumani Kihamia ni Mjanja sana ambaye hakuwepo ktk kikao hicho cha leo lakini alimuachia ofisi mhandisi wa ujenzi kitu ambacho madiwani hawakukitegemea hivyo kubaki wamepigwa butwaa baada ya kugundua listi ya uongozi iliyokuwepo ni mpya kwao tofauti na matarajio ambapo RAS aliwabana vilivyo Mkurugenzi huyo yupo safarini kikazi.

Baadhi ya madiwani walisema 'tuwe wa kweli huyu mkurugenzi uwezo wake upo juu sana kiutendaji na kiuelewa kwani kila pembe tumemkosa hatabiriki kabisa ingawa kiukweli ni muadilifu lakini anabana matumizi kupita kiasi hii ni hatari kwetu na baadhi ya watumishi.

Kukosa kazi maalum za kufanya ni baadhi ya mambo ya nayo chang'a vurugu kati ya madiwani na serikali mkoani Arusha. WANANCHI wanapaswa kuwa makini na wanasiasa wajanja wajanja wanaotegemea tenda za halmashauri ili kujikimu kimaisha .
 
Ukiandika habari ya tuuma kwa Simba halafu ukaseka mbwembwe za kuisifia Yanga na kuweka sentensi za kuonyesha kua Simba wanakiri Yanga ni wajanja na hawawezi kila idara itatosha tu kukujua upande wako na habari yako haiwezi kuaminika sio kwa Simba tu hata Yanga wenzio
 
Mbona Bavichaaa mnatoa povu....ama mmeshikwa pabaya huko Arusha??
 
Ukiandika habari ya tuuma kwa Simba halafu ukaseka mbwembwe za kuisifia Yanga na kuweka sentensi za kuonyesha kua Simba wanakiri Yanga ni wajanja na hawawezi kila idara itatosha tu kukujua upande wako na habari yako haiwezi kuaminika sio kwa Simba tu hata Yanga wenzio
Tuuma ni nini wewe kilaza??
 
Mleta mada ni teja.

Vibanda tulijenga sisi wenye hayo maduka. Na bado tunalipa kodi. Mnachotaka kufanya fanyeni si mageni. Hakuna atayewapigia magoti
 
Chadema Arusha wanatafutana sasa wamepoteana....GDK kanyaga twende
 
0ff6f63b692432d5d6090dfa71ee2d4c.jpg

Hii ndiyo kiboko yenu Arusha
 
Huyu mkurugenzi hana akili kabisa hivi inamaana kakataliwa kuongoza vikao halafu anakuja na ujinga hajui hata kuandika wewe Kihamia inaelekea ni kichwa maji
 
Huyu mkurugenzi hana akili kabisa hivi inamaana kakataa iwapo kuongoza vikao halafu anakuja na ujinga hajui hata kuandika wewe Kihamia inaelekea ni kichwa maji
Hebu kamuulize Lema anamtambua sawa sawa huyu jamaa ni nani.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom