Arusha: Lengai Ole Sabaya afikishwa Mahakamani kwa Uhujumu Uchumi, Utakatishaji Fedha

KeyserSoze

JF-Expert Member
Feb 26, 2014
4,922
2,000
Rugemalila na Habinder Sing Seth na wengine ambao hupelekwa mahakamani, huchuchumaa hivyo baada tu ya kutelemka kwenye gari na wakati wa kurudishwa rumande kabla ya kupanda gari. Mtuhumiwa ukiwa hauko kwenye motion (hutembei) unachuchumaa, hiyo ni kuimarisha ulinzi watuhumiwa wasikimbie. Watu wakiwa wamechuchuma hawawezi kukimbia. Mtu utakaye anza kusimama wakati uko kwenye amri ya kuchuchumaa utaonekana kwamba kuna jambo unataka kulifanya kuliko mkiwa mmesimama siyo rahisi kumgundua mtu mwenye nia ya kukimbia.
Kwahio ni ka-utaratibu fulani Je kautaratibu hako ni kazuri..., au ni kushushiana hadhi kwa mtuhumiwa kufanywa kama mharifu ? Samahani hata ilivyotokea kwa kina Rugemalila na yule kibaka wa kuku na simu sikusema ila sio kwamba nilifurahishwa..., Hii yote ni kujitayarisha na sisi potential watuhumiwa (mimi, wewe na yule) siku yakitukuta tupelekane kistaarabu mpaka pale makosa yetu yakithibitishwa ndio tunyooshwe..., ofcourse legally yaliyomkuta Rugemalila sio ubinadamu (hata kama ni fisadi, angekuwa proven guilty haraka kistaarabu then aadhibiwe ipasavyo)...
 

Matanga

JF-Expert Member
Nov 13, 2019
2,124
2,000
#29October2020; nilimkosoa Sabaya kuhusu kutumia magari yenye namba "feki" za UN kuteka na kuumiza wananchi wa Hai.

#30October2020; Sabaya akanipigia simu mara 3 sikupokea. Akaniandikia sms ya matusi na kutishia kuniua.

#1November2020; Nikascreenshot ujumbe huo na kumtumia rafiki yangu aliyekua kiongozi serikalini, just in case lolote likinitokea.

#26December2020; tukiwa eneo moja Moshi mimi na Don Mbowe, baada ya kuondoka Sabaya alivamia eneo hilo na kudai aoneshwe tulipo. Alipoambiwa tumeondoka alikataa kukubali. Akapiga risasi hewani na kuvuruga biashara eneo hilo.

#28December2020; Akakutana na binamu yangu Moshi (wanafahamiana). Akamwambia mpigie Malisa mwambie aje hapa, lakini usimwambie tupo wote. Jamaa akakataa. Akampiga na kumlaza rumande. Akamnyang'anya simu na hajamrudishia hadi leo.

#13May2021; Mama Samia akamsimamisha kazi kwa tuhuma mbalimbali.

#04June2021; akapandishwa mahakamani kwa makosa mbalimbali ikiwemo matumizi mabaya ya madaraka.

Nimwambie nini Mungu?

Malisa GJ
 

Chaliifrancisco

JF-Expert Member
Jan 17, 2015
15,706
2,000
20210605_140638.png
 

mbarika

JF-Expert Member
Apr 1, 2015
2,716
2,000
Leo serikali imeruhusu rasimi Chanjo kuanza kutumika Tanzania lkn kwa akili kubwa watawala wakaona isiwe nongwa kutukanwa mitandaoni na kuhojiwa hojiwa ikabidi liingizwe hili suala la SABAYA kiukweli hakuna aliyethubutu tena kulipa kipaumbele suala la Kuruhusu Chanjo leo wengi wao wamejikita kufuatilia suala la SABAYA

Kingine ambacho kina mlengo wa SABAYA ambacho wapinzani uchwara hawajakijua ni kwamba SABAYA ni mkakati wa kisiasa kuiangamiza CHADEMA na kuibua upinzani na muda si mrefu Tundu Lisu wakishirikiana kwa karibu kabisa na NYALANDU atakuwa mtetezi wa SABAYA na hapo Tundu Lisu atatangaza kuhamia ACT WAZALENDO ya Zito kabwe itakayombeba SABAYA na wanasiasa wengine wenye msimamo wa kijamaa kutoka CCM haya Mambo hayaji kwa bahati Mbaya ni mojawapo ya mbinu 100 ya CCM
Ndiyo unajidanganya hivo?
Jamaa amepakwa mafuta tayar

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 

jaji mfawidhi

JF-Expert Member
Feb 20, 2016
10,571
2,000
Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya na wenzake wanne, leo Ijumaa, wako mahabusu ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha akiwa chini ya ulinzi mkali wa jeshi la polisi.

Bado haijafahamika mashitaka yanayomkabili

=====

UPDATES:

=====

Arusha. Aliyekuwa mkuu wa Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro, Lengai Ole Sabaya (34) na walinzi wake watano wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Arusha wakikabiliwa na makosa mbalimbali likiwemo la uhujumu uchumi, utakatishaji fedha na kupokea rushwa.

Sabaya ambaye alisimamishwa na Rais Samia Suluhu Hassan Mei 13, 2021 kupisha uchunguzi alifikishwa mahakamani hapo akiwa amefungwa pingu na baada ya wote kushuka kwenye magari ya polisi, walitakiwa kuchuchumaa na kisha kupelekwa katika chumba maalum na baadaye kuingizwa mahakamani.

Waendesha mashtaka wa Serikali, Tumaini Kweka, Abdallah Chaula na Tresla Garvas mbele ya Hakimu Mfawidhi, Martha Mahumbuga na Hakimu Mkazi Mkuu, Salome Mshasha wamesema Sabaya na wenzake walitenda makosa hayo Januari 20 na Februari 9, 2021.

Kweka amesema Sabaya na wenzake watano anatuhumiwa kwa makosa ya kuunda genge la uhalifu, uhujumu uchumi, kujipatia fedha kwa njia ya rushwa na utakatishaji fedha ambapo Sabaya alijipatia Sh90 milioni kutoka kwa mfanyabiashara, Francis Mroso mkazi wa kwa Mromboo ambaye alikuwa anatuhumiwa kwa makosa ya ukwepaji kodi ili amsaidie jambo ambalo ni makosa.

Pia, Sabaya na walinzi wake wawili, Sylivester Nyengu (26) maarufu kicheche na Daniel Mbura (38) wanakabiliwa na makosa mawili ya ujambazi wa kutumia silaha wakidaiwa kuyatenda Februari 9, 2021.

Wanadaiwa walimfunga pingu na kumpiga Bakari Msangi ambaye ni diwani wa CCM kata ya Sombetin na kumuibia Sh390,000 na pia katika eneo la Bondeni jijini Arusha wakitumia silaha, Sabaya na walinzi hao wanatuhumiwa kumpiga, kumtishia silaha na kumpora Ramadhani Ayoub simu na Sh35,000.

Kwa kuwa makosa hayo hayana dhamana watuhumiwa hao walipelekwa mahabusu Gereza Kuu la Kisongo na kesi hiyo kuahirishwa hadi Juni 18, 2021.

CREDIT: Mwananchi

Zaidi, soma: Thread 'Ole Sabaya asomewa Mashtaka Sita (6) kwa Uovu aliotenda Hai. Aenda Rumande hadi Juni 18' Ole Sabaya asomewa Mashtaka Sita (6) kwa Uovu aliotenda Hai. Aenda Rumande hadi Juni 18

Pia soma
1) Rais Samia amsimamisha kazi Ole Sabaya, Mkuu wa Wilaya ya Hai ili kupisha uchunguzi wa tuhuma dhidi yake

2) Ole Sabaya akamatwa pamoja na mabaunsa wake. Ahojiwa na Vyombo vya Dola

View attachment 1807936
Ole Sabaya akitoka kwenye gari la Polisi akiwa kafungwa PINGU

View attachment 1807996
Ole Sabaya akiwa amechuchumaa mbele ya Mahakama
kikosi kazi, kiwa-hasi, pili wapatiwe mashababi wa kuwanyorosha huko nyuma, ndio wasubirie kesi zao.
 

Idugunde

JF-Expert Member
May 21, 2020
3,928
2,000
Mahakama ni chombo huru, na hakitakiwi kuingiliwa na kutumika kisiasa.

Mtuhuliwa Sabaya ameshatinga kizimbani. Ushahidi upo tayari na victims wanaodai kutendewa hayo makosa wapo kama mashahidi wakuu sasa habari za kuahirisha wiki mbili za nini?

Wananchi tuna kiu kikubwa ili tupate ukweli hivyo fanyeni haraka ndani ya mwezi kesi ziwe zimeisha. Sikilizeni mashahidi watatu kila wiki mfululizo na kisha tupate majibu.

Dpp anadai amekamilisha ushahidi na akampandisha mtuhumiwa Sabaya mahakamani kwa nini kesi ichelewe?

Acheni kupokea presha za wanasiasa.
 

Jozi 1

JF-Expert Member
Aug 16, 2015
6,559
2,000
Mahakama ni chombo huru, na hakitakiwi kuingiliwa na kutumika kisiasa.

Mtuhuliwa Sabaya ameshatinga kizimbani. Ushahidi upo tayari na victims wanaodai kutendewa hayo makosa wapo kama mashahidi wakuu sasa habari za kuahirisha wiki mbili za nini?

Wananchi tuna kiu kikubwa ili tupate ukweli hivyo fanyeni haraka ndani ya mwezi kesi ziwe zimeisha. Sikilizeni mashahidi watatu kila wiki mfululizo na kisha tupate majibu.

Dpp anadai amekamilisha ushahidi na akampandisha mtuhumiwa Sabaya mahakamani kwa nini kesi ichelewe?

Acheni kupokea presha za wanasiasa.
Kesi kuahirishwa kwa wiki mbili ni kawaida. Ndio utaratibu wenyewe kwenye kesi za jinai.
Wewe ndiye unyetaka kuingilia kesi kisiasa na kuzivuruga mahakama. Shwaini
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom