Arusha: Lengai Ole Sabaya afikishwa Mahakamani kwa Uhujumu Uchumi, Utakatishaji Fedha

Naipendatz

JF-Expert Member
Jul 27, 2011
5,079
8,219
Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya na wenzake wanne, leo Ijumaa, wako mahabusu ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha akiwa chini ya ulinzi mkali wa jeshi la polisi.

Bado haijafahamika mashitaka yanayomkabili

=====

UPDATES:

=====

Arusha. Aliyekuwa mkuu wa Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro, Lengai Ole Sabaya (34) na walinzi wake watano wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Arusha wakikabiliwa na makosa mbalimbali likiwemo la uhujumu uchumi, utakatishaji fedha na kupokea rushwa.

Sabaya ambaye alisimamishwa na Rais Samia Suluhu Hassan Mei 13, 2021 kupisha uchunguzi alifikishwa mahakamani hapo akiwa amefungwa pingu na baada ya wote kushuka kwenye magari ya polisi, walitakiwa kuchuchumaa na kisha kupelekwa katika chumba maalum na baadaye kuingizwa mahakamani.

Waendesha mashtaka wa Serikali, Tumaini Kweka, Abdallah Chaula na Tresla Garvas mbele ya Hakimu Mfawidhi, Martha Mahumbuga na Hakimu Mkazi Mkuu, Salome Mshasha wamesema Sabaya na wenzake walitenda makosa hayo Januari 20 na Februari 9, 2021.

Kweka amesema Sabaya na wenzake watano anatuhumiwa kwa makosa ya kuunda genge la uhalifu, uhujumu uchumi, kujipatia fedha kwa njia ya rushwa na utakatishaji fedha ambapo Sabaya alijipatia Sh90 milioni kutoka kwa mfanyabiashara, Francis Mroso mkazi wa kwa Mromboo ambaye alikuwa anatuhumiwa kwa makosa ya ukwepaji kodi ili amsaidie jambo ambalo ni makosa.

Pia, Sabaya na walinzi wake wawili, Sylivester Nyengu (26) maarufu kicheche na Daniel Mbura (38) wanakabiliwa na makosa mawili ya ujambazi wa kutumia silaha wakidaiwa kuyatenda Februari 9, 2021.

Wanadaiwa walimfunga pingu na kumpiga Bakari Msangi ambaye ni diwani wa CCM kata ya Sombetin na kumuibia Sh390,000 na pia katika eneo la Bondeni jijini Arusha wakitumia silaha, Sabaya na walinzi hao wanatuhumiwa kumpiga, kumtishia silaha na kumpora Ramadhani Ayoub simu na Sh35,000.

Kwa kuwa makosa hayo hayana dhamana watuhumiwa hao walipelekwa mahabusu Gereza Kuu la Kisongo na kesi hiyo kuahirishwa hadi Juni 18, 2021.

CREDIT: Mwananchi

Zaidi, soma: Thread 'Ole Sabaya asomewa Mashtaka Sita (6) kwa Uovu aliotenda Hai. Aenda Rumande hadi Juni 18' Ole Sabaya asomewa Mashtaka Sita (6) kwa Uovu aliotenda Hai. Aenda Rumande hadi Juni 18

Pia soma
1) Rais Samia amsimamisha kazi Ole Sabaya, Mkuu wa Wilaya ya Hai ili kupisha uchunguzi wa tuhuma dhidi yake

2) Ole Sabaya akamatwa pamoja na mabaunsa wake. Ahojiwa na Vyombo vya Dola

Sabaya1.jpg

Ole Sabaya akitoka kwenye gari la Polisi akiwa kafungwa PINGU

Social(2).png

Ole Sabaya akiwa amechuchumaa mbele ya Mahakama
 
Picha hiyo ikutafakarishe mtu yeyote utakayeiona.

Tambua ya kuwa nafasi uliyonayo ni ya muda tu. Hata kama utaishikilia mpaka mwisho wa uhai wako, ipo mahali utalipwa kutokana na matendo yako.

Busara zikuongoze utende haki na muombe Mungu akusimamie.

Majivuni na ukatili hayana lolote bora la kulipalilia.

Jana ulikuwa ukiwaamuru polisi na kukupigia salute, leo wanakupigisha magoti na pingu mkononi.
 
Back
Top Bottom