VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,136
- 17,871
Waraka wa Mbunge wa Arusha Mjini (CHADEMA), Godbless Lema kuachiwa juma lijalo. Waraka huo, niliopata bahati ya kuuchungulia, unabeba mambo muhimu yahusuyo hasa haki za binaadamu. Mambo hayo yalionwa na kusikiwa na Lema alipokuwa Mahabusu Kisongo kwa takribani miezi minne.
Waraka huo maalum kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na viongozi wengine,unaibua pia njama mbalimbali zinazofanywa na wakandamizaji wa haki za binaadamu. Lema pia anaanika simulizi zenye kuliza za mahabusu wanaopigwa danadana kwenye kesi zao na kuwafanya wasitendewe haki.
Lema ameandika. Lema anataka Rais ajue. Anataka ujumbe umfikie Rais na marekebisho yafanyike. Lema ameapa kuendelea kusema ukweli na kuusimamia kwa namna yoyote iwezekanayo. Lema hatanii, anasema na kufanya kweli. Kaeni mkao wa kula kwa Waraka huo wa Mbunge Lema kwenda kwa Rais.
Mwafaaaaa!
Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Arusha kumchagua Lissu Urais wa TLS)