Arusha kitovu cha umahiri wa tehama EAC

elivina shambuni

JF-Expert Member
May 31, 2018
461
295
1566968805118.png


TANZANIA imepewa hadhi ya kimataifa ya kuwa mwenyeji wa Kituo cha umahiri cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano Afrika Mashariki (CENIT@EA), kilichozinduliwa katika Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela (NM-AIST) jijini Arusha.

Arusha ndiko yalipo makao makuu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na taasisi mbalimbali za kimataifa, ikiwa ni pamoja na Mahakama ya Afrika. Akizindua kituo hicho, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia wa Tanzania, Profesa Joyce Ndalichako alisema kituo hicho kilichofadhiliwa na Serikali ya Ujerumani kinalenga kuwajengea uwezo Watanzania na wanachama wa EAC katika masuala ya Tehama katika kuleta maendeleo ikiwa ni pamoja na kutoa ufadhili wa masomo ya shahada za uzamili.

Alisema Mwongozo wa Sayansi, Teknolojia na Ubunifu unatambua nafasi ya Tehama kama nyenzo muhimu katika kuimarisha maendeleo ya kiuchumi na kijamii katika nyanja mbalimbali yakiwemo masuala ya viwanda, uchumi na maeneo mengine akitolea mfano mifumo ya fedha inayotumia TEHAMA inavyotumika Afrika Mashariki.

Amewashukuru wafadhili wa kituo hicho serikali ya Ujemani ambao tayari wametoa kiasi cha Euro Milioni 1.384 ambayo ni takribani Shilingi Bilioni 3.5 za Kitanzania kati ya Euro Milioni 4 thamani ya mradi mzima utakaotekelezwa kwa miaka minne hadi 2021.

Mapema, akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Jerry Muro aliishukuru Taasisi ya NM- AIST kwa kuendelea kushirikiana na Wilaya ya Arumeru katika kutekeleza miradi ya maendeleo na kwa kuanzisha Kituo cha Umahiri cha TEHAMA na kuitaka taasisi hiyo ya Nelson Mandela kuhakikisha kituo hicho hakiwi cha wanataaluma pekee, bali pia huduma zake zisaidie wananchi hasa wakulima katika kuongeza tija katika kilimo na mazao na kusaidia kutoa mbinu bora za kilimo kupitia tati zitakazokuwa zikifanyika.

Naye Kaimu Mwenyekiti wa Baraza wa taasisi hiyo, Profesa Lughano Kusiluka amesema kituo hicho ni cha Jumuiya ya Afrika Mashariki ambacho kitakuwa kikifundisha wanafunzi katika ngazi za shahada ya umahiri katika teknolojia ya mambo simu , hasa masuala ya usalama wa matumizi ya simu na mawasiliano
 
Back
Top Bottom