Arusha: Kijana matatani kwa kujiteka na kuwaomba nduguze hela ili alipe madeni

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,005
9,872
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha ACP JUSTINE MASEJO Akiongea na waandishi wahabari leo ofisi kwake amesema kuwa Mnamo 25.07.2021 muda wa saa 15:20 Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha lilipokea taarifa kutoka kwa mtu mmoja (jina limehifadhiwa) kuwa ndugu yake aitwaye DICKSON S/O PETER MUNGULU ametekwa ambapo taarifa hizo walizipata kupitia ujumbe mfupi wa simu (SMS) uliotumwa kutoka kwa simu ya mhanga ukieleza kwamba ametekwa na ili aachiwe zinahitajika kiasi cha fedha Shilingi Milioni Tatu (Tsh.3,000,000) vinginevyo atauawa.

Amesema kuwa Baada ya kupokea taarifa hizo Jeshi la Polisi Mkoani hapa lilifanya uchunguzi wa kina na tarehe 28.07.2021 muda wa jioni Jeshi la Polisi Mkoani hapa lilifanikiwa kumpata Kijana huyo aliyesadikika kuwa ametekwa huko maeneo ya MOROMBO katika nyumba ya kulala wageni (Jina limehifadhiwa)

Kamanda wa Polisi ameendelea kuwaambia waandishi kuwa Baada ya kumhoji DICKSON S/O PETER MUNGULU ambaye mwaka 2020 alimaliza Shahada ya Elimu katika Chuo kikuu cha Makumira kilichopo Arusha, ilibainika kuwa alitoa taarifa za uongo kwa ndugu zake ili pate kiasi hicho cha fedha ziweze kumsaidia kulipa madeni yake mbalimbali yanayomkabili.

ACP MASEJO amesema kuwa Sambamba na hilo baada ya kumchunguza zaidi katika mwili wake ilibainika kuwepo na majeraha sehemu ya Shingo na Mguu alikiri kujichoma na kitu chenye ncha kali yeye mwenyewe kwa nia ya kuuaminisha wazazi wake pamoja na ndugu zake wengine kwamba alitekwa.

Jeshi la Polisi Mkoani hapa linaendelea na upelelezi wa tukio hilo na pindi utakapokamilika jalada litapelekwa Ofisi ya Mwendesha Mashtaka wa Serikali kwa hatua zaidi za kisheria.

Kamanda Masejo ametoa wito kwa wananchi,vijana wenye tabia kama hii ilionyeshwa na kijina uyu kuwa Jeshi la Polisi halita wafumbia macho wale wote watakao husika na litawachukuliwa hatua kali za kisheria kwa wataobainika kupotosha umma na kutoa taarifa za uzushi kwa kwa jamii.Pia niwaombe wananchi kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu katika maeneo yao kwa Jeshi la Polisi ili zifanyiwe kazi.
 
Mwamba kakosea alitakiwa atafute watu wenye kazi zao waingie mzigoni pesa mbona ingetoka wangegawana kiroho safi uchoyo tu.
Natania tu wakuu !!
 
Linatuma meseji lipo humo humo gesti.
Kazi nyepesi yaani polisi wanaenda alipo na kuuliza waliingia wangapi hapo guesthouse kasaini peke yake na inaonekana alianza na pombe baadae akaamua kujizuru na hela ya hapo ukute anadaiwa...ametumia mbinu mbovu kupata pesa
 
Back
Top Bottom