ARUSHA: Kijana aliyeandika kwenye ukurusa wake wa Facebook kuwa Tundu Lissu angeuawa akamatwa na Polisi

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,899
Jeshi la polisi mkoani Arusha limemshilikia kijana mmoja afahamikae kwa jina la Abuu aliyesambaza ujumbe kwenye account yake ya Facebook maneno makali kuhusu Mh Tundu lissu akisema ni bora majambazi wangemuuwa ameshikwa ili akawasaidia polisi.

Mpaka sasa yuko kituo cha polisi Kijenge Arusha kwa kuhojiwa zaidi.
 
Buku la bando limesababisha alale korokoroni na apate matatizo

Huu ushabiki huu ,huenda alitaka apate likes na comments nyingi za mapovu ili aridhike ,huenda ni kuwapandisha hasira tu watu haswa chadema

Bora angeyefanyia JF ila kafanyia Facebook ,picha bwerere ,na kitambulisho kakianika

Usipoweza kuzuia mihemuko ,ushabiki matatizo yake ndio haya

Huku JF kuna watu wanafanya sacarsm tukio ya lissu ili kuwakera wapinzani ila kimtindo hawachukuliwi serious sana ila huyo dogo wa fesibuku aliyejianika uchi yamemkuta

Sasa kailetea matatizo familia yake haswa wazazi. ..tutumie bando zetu vzr

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom