Arusha: Kigogo OBC, wafanyakazi waachiwa huru, wakamatwa

Doncy monco

Member
Jul 26, 2019
38
101
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Arusha, jana imewaachia huru raia 10 wa kigeni na Mkurugenzi wa Kampuni ya wawekezaji ya Otterlo Business Cooperation (OBC) kutoka Falme za Kiarabu, Isack Mollel (59), baada ya upande wa Jamhuri kushindwa kuwasomea maelezo ya awali kwa zaidi ya mara nne.

Hata hivyo, baada ya kuachiwa huru na shauri hilo kufutwa, watuhumiwa hao walikamatwa tena na polisi na kupelekwa Kituo Kikuu cha Polisi Arusha.

Mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa mahakama hiyo, Niku Mwakatobe, upande wa Jamhuri uliwakilishwa na Wakili wa Serikali Janeth Sekule na Mwendesha Mashtaka wa Serikali kutoka Idara ya Kazi, Emmanuel Mweta huku Mollel akitetewa na mawakili Method Kimogogoro, Daudi Haraka, Elvaison Maro na Goodluck Peter.

Shauri hilo la jinai namba 74 la mwaka huu, lilipangwa kuwasomea washtakiwa hao maelezo ya awali na kuanza kusikilizwa kwa mashahidi wa Jamhuri.

Wakili Janeth alidai hawako tayari kuwasomea hoja hizo kwa madai kuwa hajajiandaa.

“Kama nilivyoainisha, takribani wiki mbili nilikuwa na matatizo, sikuwepo na leo ndiyo nimeingia ofisini na kukutana ma tarehe hii ya shauri husika, sikuwa nimejiandaa,” alidai.

Baada ya maelezo hayo, Hakimu Niku alisema awali washtakiwa hao walifikishwa mahakamani hapo kwa mara ya kwanza Februari 7, mwaka huu na kuwa ni zaidi ya miezi sita ‘facts’ hazijaendelea.

“Licha ya kila mara mahakama kusema inaahirisha shauri hili kwa sababu ya Jamhuri kushindwa kuendelea na kesi (kuwasomea hoja za awali), mahakama inawaachia huru chini ya kifungu cha 225(5) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai, washitakiwa mko huru, mnaweza kwenda,” alisema.

Awali kabla ya uamuzi huo wa Hakimu Niku, Wakili Maro aliieleza mahakama hiyo kuwa hili lilikuwa ahirisho la mwisho kwa upande wa Jamhuri na kuwa wanaiomba mahakama ipange kesi hiyo tarehe za karibuni, ikiwezekana ipangwe Septemba 9, ili wateja wao waweze kusomewa hoja za awali na kesi kuendelea kusikilizwa.

Baada ya watuhumiwa hao kuachiwa huru, walikamatwa tena na polisi waliokuwa mahakamani hapo na kuondolewa kwa gari lililokuwa na namba za usajili T 125 DFQ saa 4:41 asubuhi.

Mollel anashikiliwa Gereza la Kisongo jijini hapa kwa kuwa anakabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi.

Katika shauri hilo, Mollel anakabiliwa na mashtaka 37 ya kujihusisha na kuajiri raia 37 wa kigeni wasiokuwa na vibali halali vya kufanya kazi nchini wala cheti cha msamaha, kinyume na sheria ya kuratibu ajira na mahusiano ya wageni.

Mollel anaungana na raia 10 wa kigeni waliokuwa wakifanya shughuli mbalimbali, ikiwemo ufundi magari, ufundi matairi, wapishi, madereva na wapaka rangi nyumba, ambao waliajiriwa OBC iliyopo eneo la Loliondo, Wilaya ya Ngorongoro mkoani hapa ikijishughulisha na shughuli za uwindaji wa kitalii.

Washtakiwa wengine ni Darweshi Jumma, Riaz Aziz Khan, Mohammad Tayyab, Ali Bakhsh, Abdul Rehman Muhammad, Martin Crasta, Imtiazd Fiaz, Arshad Muhammad, Hamza Sharif na Zukfiqar Ali.

Awali Agosti 21 mwaka huu mawakili wa utetezi katika shauri hilo waliulalamikia upande wa Jamhuri kukwamisha shauri hilo kuendelea kusikilizwa.

Ilidaiwa mahakamani hapo kuwa mawakili wanaohusika wameenda kwenye mafunzo Dar es Salaam, hivyo kuiomba mahakama hiyo kupanga tarehe nyingine.

Kufuatia maelezo hayo, Wakili Haraka alidai mahakamani hapo kuwa hii ni mara ya nne kwa shauri hilo kuahirishwa kwa madai kuwa mawakili wanaopaswa kuwasomea hoja hizo wana dharura.
 
Wasinge toka mahakamani wangekaa na hakimu akitoka watoke naye

Ova

Ulisha wahi kukaa mahabusu au kufikishwa mahakamani? Naona logic yako ndogo sana kuhusu mambo ya mahakama, hapo watajutia kukamatwa kwa case ya uhujumu uchumi, hizi case ni mbaya sana hazina dhamana na unaweza kaa ndani mahabusu kwa muda wote kusubiria uchunguzi kukamilika..

Case ya uhujumu uchumi au case kama ya treason hatari sana sana..!!
 
Kwa hiyo hakimu kuwaachia ilikuwa ni sanifu tu?

Inavyoonekana ilipangwa waachiwe halafu wadakwe tena!

Maana ni nani aliwaandaa polisi na defender lao?

Wajuzi wa sheria mnasemaje kuhusu hizi sheria za kihuni?

Kwanini wasibadilishiwe tu mashitaka wakaendelea na kesi, mpaka waachiwe bandia?

Hamuelewi sheria hii ni jinsi gani inavyokojolea hisia za watuhumiwa!

Mtu unaachiwa, unajawa na furaha pamija na familia yako inakuja kukukumbatia kukupa pongezi, dk5 nyingi tayari ushadakwa tena!

Ni nani alianzishaga hii sheria kandamizi namna hii?
 
Yaani bora ulivyosema hujui sheria. Na hao ni mamburula tuuu walivyokaa rumande hawajaambiwa tuu kifungu hicho unajiteteaje?
Subiri watakueleza wengine ulivyoanza kikuda hivyo this is the best you get.
 
sio kila économic case haina dhamana kaka, huwa dhamana zake hadi high court na mashart ya kuacha nusu ya pesa inayoendana na gharama ya case , ni
money laundering ndo haina dhamana na zinginezo
 
Kwa hiyo hakimu kuwaachia ilikuwa ni sanifu tu?

Inavyoonekana ilipangwa waachiwe halafu wadakwe tena!

Maana ni nani aliwaandaa polisi na defender lao?

Wajuzi wa sheria mnasemaje kuhusu hizi sheria za kihuni?

Kwanini wasibadilishiwe tu mashitaka wakaendelea na kesi, mpaka waachiwe bandia?

Hamuelewi sheria hii ni jinsi gani inavyokojolea hisia za watuhumiwa!

Mtu unaachiwa, unajawa na furaha pamija na familia yako inakuja kukukumbatia kukupa pongezi, dk5 nyingi tayari ushadakwa tena!

Ni nani alianzishaga hii sheria kandamizi namna hii?
kibaya zaidi hapo case inaenda kuanza upya kabisa, wakati ilishafikia hatua za kuanza kusikiliza mashahidi
 
Ulisha wahi kukaa mahabusu au kufikishwa mahakamani? Naona logic yako ndogo sana kuhusu mambo ya mahakama, hapo watajutia kukamatwa kwa case ya uhujumu uchumi, hizi case ni mbaya sana hazina dhamana na unaweza kaa ndani mahabusu kwa muda wote kusubiria uchunguzi kukamilika..

Case ya uhujumu uchumi au case kama ya treason hatari sana sana..!!
Hivi unajua hukumu ya uhujumu uchumi ikoje?
Mahakamani nishaburuzwa kwa kesi nyingine tu

Ova
 
Yaani bora ulivyosema hujui sheria. Na hao ni mamburula tuuu walivyokaa rumande hawajaambiwa tuu kifungu hicho unajiteteaje?
Subiri watakueleza wengine ulivyoanza kikuda hivyo this is the best you get.
Nineanza kikuda mkuu sindiyo?
Basi wewe upo vizuri. Ninaishia hapa.
 
Ulisha wahi kukaa mahabusu au kufikishwa mahakamani? Naona logic yako ndogo sana kuhusu mambo ya mahakama, hapo watajutia kukamatwa kwa case ya uhujumu uchumi, hizi case ni mbaya sana hazina dhamana na unaweza kaa ndani mahabusu kwa muda wote kusubiria uchunguzi kukamilika..

Case ya uhujumu uchumi au case kama ya treason hatari sana sana..!!
Hiyo sheria inahalalisha uhalifu wa dola dhidi ya raia, ni uonevu na hata wanaoutumia hiyo sheria kuwaumiza raia wajue iko siku watalipa.

Vv
 
Unaijua vizuri OBC au unaongea tu? Unajua wamasai hadi walichomewa nyumba zao na mifugo, na walipigwa vibaya kisa tu OBC huko Loliondo, unadhubutu kusema wanaonewa? Hivi nyie kila case mnaona serikali inaonea raia? Ukute hata hujui hii issue vizuri, sbb tu unajua kusoma na kuandika basi umeamua kujibu usichojua
 
sio kila économic case haina dhamana, usikalili, money laundering ndo haina dhamana na zinginezo

Usikalili? Hiki ni kiswahili au? Na usikute ww ni wakili au mwanasheria wakati lugha inakupiga chenga.. Anyway, hiyo profile ni yako? Can we have private chat nimekupenda, unavutia sana hasa mak.alio na shape, uko vizuri kwa nje, ndani sijui.. 💋😋😊
 
Rais Wa Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania
Ananyoosha Nchi
Wale Ambao Ni Untouchable Go And Touch Them!!
😅😄😃😂😁😀
 
Unaijua vizuri OBC au unaongea tu? Unajua wamasai hadi walichomewa nyumba zao na mifugo, na walipigwa vibaya kisa tu OBC huko Loliondo, unadhubutu kusema wanaonewa? Hivi nyie kila case mnaona serikali inaonea raia? Ukute hata hujui hii issue vizuri, sbb tu unajua kusoma na kuandika basi umeamua kujibu usichojua
hao OBC walivamia kwenye uho uwekezaji au walipitia serikalini na kupewa vibari vyote na serikali ya ccm? Au walikuja from nowhere tu,
 
hao OBC walivamia kwenye uho uwekezaji au walipitia serikalini na kupewa vibari vyote na serikali ya ccm? Au walikuja from nowhere tu, bastard

Wee dada mbona matusi yanakutoka mchana mchana tena mbele za watu? Kitu gani kimekufanya mpaka utoe hilo tusi bila aibu? Kama umesukumwa na hasira, basi siku nyingine hakikisha kwanza hizo hasira zako zimeshuka halafu ndiyo uandike kwenye keyboard ili ulinde staha yako.
 
hao OBC walivamia kwenye uho uwekezaji au walipitia serikalini na kupewa vibari vyote na serikali ya ccm? Au walikuja from nowhere tu,

Vibari 🍌✂❌❌❌❌❌❌❌
Muulize Kinana hayo maswali ndio aliwaleta na sio CCM ukome, CCM inatoka wapi? acha utoto, nitakujia na KY sasa hv utapunguza purukushani
 
Ulisha wahi kukaa mahabusu au kufikishwa mahakamani? Naona logic yako ndogo sana kuhusu mambo ya mahakama, hapo watajutia kukamatwa kwa case ya uhujumu uchumi, hizi case ni mbaya sana hazina dhamana na unaweza kaa ndani mahabusu kwa muda wote kusubiria uchunguzi kukamilika..

Case ya uhujumu uchumi au case kama ya treason hatari sana sana..!!
Je Jiwe anavyoendelea kuhujumu uchumi
 
Back
Top Bottom