Arusha iongozwe na Mameya wawili kama marais wa Ivory Coast.

Luteni

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
2,274
296
Juzi tumeendelea kushuhudia uhaini wa demokrasia ukifanyika ndani ya nchi yetu wakati wa uchaguzi wa meya wa manispaa ya Arusha. Nauita uhaini kwa sababu kitendo kilichofanywa na madiwani wa CCM kumchagua meya toka uchochoroni ni kudhihirisha oroho wa madaraka wa chama hicho.

Kutokana na kanuni za mabaraza ya halmashauri, yaani uchaguzi utafanyika tu endapo kolamu imetimia 2/3 ya wajumbe kitu ambacho hakikuwepo ni dhahiri kuwa kanuni zimekiukwa, na kwa kitendo hicho CCM imebaka demokrasia ni sawa na mapinduzi ya kijeshi.

Nakishauri chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema, pamoja na kukusudia kwenda mahakamani waitishe mapema uchaguzi wao wa meya chini ya Mwenyekiti wa Halmashauri ya Moshi kuchagua meya atakayefanya kazi sambamba na meya wa CCM.

Najua mwanzo CCM watakibeza kitendo hiki kama walivyobeza walkout ya wabunge kususia hotuba ya rais lakini baadaye watakuja kutambua umuhimu wa wake baada ya jamii kuona msuguano utakaokuwepo. Serikali ya Ivory Coast ilibeza vile vile rais kujiapisha lakini leo wanazungumuza lugha nyingine.

Kwa kitendo hicho Chadema watakuwa wanaua ndege wawili kwa jiwe moja.

Hivi Chadema watajifanya wastaarabu hadi lini wakati CCM haionyeshi ustaarabu?
 
Kishongo

JF-Expert Member
May 4, 2010
932
64
Huo si ushauri mzuri. Kama CCM wamechagua bila koramu, na umesema ni makosa, kwa nini unataka Chadema warudie makosa hayo hayo?
Uamuzi mzuri ni kwenda mahakamani.

Pengine ungetoa pia ushauri kwa Mbunge Lema aache kuingia siasa kichwa-kichwa na baadaye kuishia kuilaumu polisi. Mbunge huyu ana tabia ya kufuata mkumbo wa waungaji mkono wake (mob psychology). Akichukuliwa hatua halali za kipolisi anaishia kulalama.

Nahisi kiwango chake cha elimu kinachangia pia kumfanya apatwe na masahibu ya namna hii. Mlio karibu mpeni ushauri.
 
Unadhani haki itatendeka kwenye mahakama zetu za Tanzania?
 
Crashwise

JF-Expert Member
Oct 23, 2007
22,228
8,722
Pengine ungetoa pia ushauri kwa Mbunge Lema aache kuingia siasa kichwa-kichwa na baadaye kuishia kuilaumu polisi. Mbunge huyu ana tabia ya kufuata mkumbo wa waungaji mkono wake (mob psychology). Akichukuliwa hatua halali za kipolisi anaishia kulalama.

Nahisi kiwango chake cha elimu kinachangia pia kumfanya apatwe na masahibu ya namna hii. Mlio karibu mpeni ushauri.
hicho unachokiongea ni ujinga mtupu, maana ya kuingia kwenye siasa kichwa kichwa nini?, amefata mob psychology ulitaka aendele kuwa peti peti, watu kama Lema kwa CCM ni sumu kwao ndiyo maana huishia kutumia nguvu nyingi kuliko ubongo wewe uliona wapi polisi wakaingilia mkutano kama hiyo...wanataka tuwe kama kenya ambapo hufikia wabunge kupigana bungeni, tutakuwa wapole mpaka lini kumbuka haki haipatikani kwa kubembelezana mbeleza na watu kama Lema ndiyo wanotakiwa kwa sasa hapa kwetu kuliko sisi tunaokalia kulalamika kwenye keyboard subiri na utaona..
 
Halisi

JF-Expert Member
Jan 16, 2007
2,802
608
Huo si ushauri mzuri. Kama CCM wamechagua bila koramu, na umesema ni makosa, kwa nini unataka Chadema warudie makosa hayo hayo?
Uamuzi mzuri ni kwenda mahakamani.

Pengine ungetoa pia ushauri kwa Mbunge Lema aache kuingia siasa kichwa-kichwa na baadaye kuishia kuilaumu polisi. Mbunge huyu ana tabia ya kufuata mkumbo wa waungaji mkono wake (mob psychology). Akichukuliwa hatua halali za kipolisi anaishia kulalama.

Nahisi kiwango chake cha elimu kinachangia pia kumfanya apatwe na masahibu ya namna hii. Mlio karibu mpeni ushauri.

Duh!! "Hatua halali" za polisi ni kumpiga mbunge aliyepigiwa kura na watu kibao? Ama kweli maslahi yanapofua watu!!! Mungu ibariki Tanzania yetu
 
samirnasri

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
1,388
213
Dr. Slaa aliamua kutumia busara sana katika kuepusha shari hapa nchini baada matokeo ya uchaguzi mkuu kutangazwa. Angeweza kuwahimiza wafuasi wa chadema kuandamana kupinga mchakato mzima wa uchaguzi na kutangazwa matokeo. Nina hakika wananchi wengi wangeitikia wito huo hasa kutokana na hamasa kubwa waliyoionesha wakati wa kusubiri matokeo katika maeneo mbalimbali hapa nchini. Lakini pamoja na mambo yote hayo nashawishika kusema kwamba busara hizo zimekua ni kazi bure kwa sababu yale ambayo dr slaa na chadema waliyaepuka ndio hayo ambayo CCM wanataka yatokee. Umafia uliofanywa na ccm kwenye uchaguzi wa meya na naibu meya mkoani Arusha unaonesha ni jinsi gani chama hicho tawala kimedhamiria kuipeleka tanzania kwenye machafuko yasiyokua ya lazima. Nimegundua kua ccm kupitia jeshi lake la polisi ndio wamekua waasi wa vurugu zote za uchaguzi. Kwa maana hiyo sitashangaa tena nikiona chadema nao wakaamua kupambana kwa kutumia nguvu ya UMMA kwa kua wao hawana nguvu ya dola.
 
emma 26

Senior Member
Oct 29, 2010
108
2
wenye viburi lazima wapate kisago kama wangekuwa wanaelew
ana tu polis wangepiga mtu?kama unaona vurugu ndo suruhisho huna hakili na kama unazo basi hujui kuzitumia
 
Luteni

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
2,274
296
wenye viburi lazima wapate kisago kama wangekuwa wanaelew
ana tu polis wangepiga mtu?kama unaona vurugu ndo suruhisho huna hakili na kama unazo basi hujui kuzitumia
CCM-Arusha wamewapata na kuwafurahisha watu kama nyie mnaoona ya leo bila kujali ya mbele.
 
Crashwise

JF-Expert Member
Oct 23, 2007
22,228
8,722
wenye viburi lazima wapate kisago kama wangekuwa wanaelew
ana tu polis wangepiga mtu?kama unaona vurugu ndo suruhisho huna hakili na kama unazo basi hujui kuzitumia
Yaani mtu kama wewe nikikutana wewe na kuchinja bila kuhitaji kibali...maana hunatofauti na kunguni
 
msafiri.razaro

JF-Expert Member
Oct 12, 2010
1,227
687
Dr. Slaa aliamua kutumia busara sana katika kuepusha shari hapa nchini baada matokeo ya uchaguzi mkuu kutangazwa. Angeweza kuwahimiza wafuasi wa chadema kuandamana kupinga mchakato mzima wa uchaguzi na kutangazwa matokeo. Nina hakika wananchi wengi wangeitikia wito huo hasa kutokana na hamasa kubwa waliyoionesha wakati wa kusubiri matokeo katika maeneo mbalimbali hapa nchini. Lakini pamoja na mambo yote hayo nashawishika kusema kwamba busara hizo zimekua ni kazi bure kwa sababu yale ambayo dr slaa na chadema waliyaepuka ndio hayo ambayo CCM wanataka yatokee. Umafia uliofanywa na ccm kwenye uchaguzi wa meya na naibu meya mkoani Arusha unaonesha ni jinsi gani chama hicho tawala kimedhamiria kuipeleka tanzania kwenye machafuko yasiyokua ya lazima. Nimegundua kua ccm kupitia jeshi lake la polisi ndio wamekua waasi wa vurugu zote za uchaguzi. Kwa maana hiyo sitashangaa tena nikiona chadema nao wakaamua kupambana kwa kutumia nguvu ya UMMA kwa kua wao hawana nguvu ya dola.

Polisi wamezidi kuingilia demokrasia, sasa inabidi wajue kwamba ikibidi wafanyiwa kama yale ya Pemba.
 
Mungi

JF Gold Member
Sep 23, 2010
16,980
9,547
Mahakama zetu zinatenda haki kabisa, tena bila upendeleo.
Hukumu ya kesi itakayofunguliwa kesho itatolewa bila kumwonea mtu na chadema watashinda kesi.
Hukumu itakuwa mwezi wa saba mwaka 2015
 
Luteni

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
2,274
296

Facts1

JF-Expert Member
Dec 23, 2009
307
28
Arusha yapata meya wawili•

Aliyepewa unaibu Meya awageuka CCM

na Ramadhani Siwayombe, Arusha

SAKATA la uchaguzi wa Meya wa Arusha mjini limeingia katika sura mpya baada ya mkurugenzi wa manispaa ya Arusha Estomii Chang'a kusema uchaguzi uliofanywa na kumshirikisha mbunge wa Viti Maalumu mkoa wa Tanga Mary Chatanda ulikuwa na baraka za Kaimu Katibu wa Bunge Eliakimu P. Mrema.

Chang'a alitoa ufafanuzi huo kwa waandishi wa habari jana wakati akijibu maswali ya waandishi kuhusiana na utata uliojitokeza kuhusu uchaguzi huo ambapo ilipelekea vurugu baada ya kutangazwa meya bila madiwani wa CHADEMA kuwepo.

Katika vurugu hizo mbunge wa jimbo la Arusha mjini, Godbles Lema alikamatwa na polisi kwa kichapo na kuswekwa rumande kwa saa kadhaa kabla ya kuachiwa na kulazimika kukimbizwa hospitali baada ya kuishiwa nguvu.

Akiongelea matukio hayo Mkurugenzi huyo alisema kufuatia utata uliojitokeza wa uhalali wa Mary Chatanda kupiga kura manispaa ya Arusha badala ya Tanga, alilazimika kuwasiliana na ofisi ya bunge kupata ufafanuzi ndipo alipoletewa barua iliyosainiwa na Mrema ikimhalalisha Chatanda kushiriki uchaguzi huo.

Alifafanua licha ya kupata ufafanuzi huo siku ya Ijumaa alilazimika kuahirisha kikao hicho cha baraza na kufanya kikao cha siri cha ndani siku ya Jumamosi ambapo madiwani wa CHADEMA hawakuhudhuria ndipo akalazimika kuendelea na taratibu za uchaguzi na kumtangaza Gaudensi Limo kuwa meya huku Michael Kivuyo akimtangaza kuwa ndie naibu meya.

Wakati mkurugenzi akitoa ufafanuzi huo aliyetangazwa kuwa Naibu Meya Michael Kivuyo (TLP) ameongea na waandishi wa habari jana na kusema uchaguzi uliofanyika haukuwa halali kwa kuwa ulikiuka baadhi ya kanuni za halmashauri.

Kivuyo alisema licha ya yeye kuchaguliwa kuwa naibu meya lakini atashirikiana na madiwani wa CHADEMA kupinga uchaguzi huo kwani ulikiuka taratibu mbalimbali za kikanuni za halmashauri.

Alipoulizwa kuhusu wadhifa wake kama ataendelea kuwa nao wakati anapinga uchaguzi huo alisema anawasiliana na chama chake ili atoe tamko la kujiuzulu nafasi hiyo ya unaibu meya kwa kuwa uchaguzi uliomchagua haukuwa halali.

Wakati hayo yakiendelea, madiwani wa CHADEMA hadi jana jioni walikuwa wanaendelea na kikao cha kumchagua meya wa jiji la Arusha ambapo nafasi hiyo ilikuwa ikiwaniwa na diwani wa kata ya Kimandolu Estomii Mala.

Akiongea na Tanzania Daima msemaji wa madiwani wa CHADEMA John Bayo alisema kuwa wao wanachagua meya wao na leo watamsindikiza katika ofisi za manispaa ya Arusha kuanza kazi za umeya.

Hali hiyo inamaanisha kuwa kutakuwa na mameya wawili katika ofisi moja hali ambayo si ya kawaida kutokea katika historia ya siasa za nchi hii.

Kwa hali hiyo, kinachotokea Arusha katika ngazi ya umeya kinafafana kabisa na kile kilichojitokeza nchini Ivory Coast ambapo nchi hiyo sasa inaongozwa na marais wawili baada ya kila moja kujitangaza rais.

Uchaguzi huo wa kumpata Meya wa jiji la Arusha uliingia tafrani kutokana na vyama vya CCM na CHADEMA kulumbana katika masuala ya kanuni, CHADEMA wakipinga mbunge wa viti maalum Mary Chatanda (CCM) kuwa mjumbe wa mkutano huo huku CCM nao wakipinga mbunge wa viti maalumu wa Rebecca Mgondo (CHADEMA) kuwa hajaapishwa kuwa mbunge hivyo hastahili kuwa mjumbe wa kikao hicho.

Wakati yote hayo yakiendelea, aliyetangazwa kuwa meya wa jiji la Arusha Gaudensi Lyimo (CCM), jana aliitisha kikao na waandishi wa habari chini ya ulinzi wa maofisa kadhaa wa polisi waliovalia kiraia, kuzungumzia yaliyojitokeza katika uchaguzi.

Kitendo hicho kiliwakera waandishi wa habari na kulazimika kumhoji Lyimo kwa kumtaka aeleze sababu za kuwaita askari kanzu hao katika kikao chake hicho kinyume na taratibu za kawaida za vikao kama hivyo vya wanahabari.

Katika majibu yake, Lyimo alijitetea kuwa wana usalama hao wamelazimika kuwepo kwa ajili ya kuangalia usalama wa eneo hilo kutokana na hali inayoendelea hivi sasa tangu kuvurugika kwa mkutano wa baraza la madiwani ambao yeye alitangazwa kuwa meya wa Arusha.

Majibu hayo hayakuweza kukidhi haja ya waandishi wa habari na kufikia hatua ya kulaumu halmashauri hiyo ya manispaa ya Arusha kuanza kutumia vyombo vya dola vibaya kitendo ambacho hata siku ya kikao cha baraza vilitumika kuwasambaza wananchi waliofika kutaka kusikiliza kikao hicho cha kwanza na kurushiwa mabomu ya machozi.

"Tunaomba tukwambie wazi kuwa kama ndio staili hii umeingia nayo, ofisini hii tutakuwa hatuji katika mikutano yako hata kama umetualika. Kutuletea askari ni kuingilia uhuru wa habari kwani tutakuwa tunashindwa hata kuuliza baadhi ya maswali kutokana na kukaa kwa hofu," alisema Moses Mshala mwandishi wa habari wa gazeti la Mwananchi.

Aidha, akizungumzia suala hilo mwandishi wa habari wa gazeti la Raia Mwema, Paulo Sarwat, alisema kitendo cha polisi kuwafukuza waandishi katika kikao hicho cha baraza la madiwani ni cha udhalilishaji mkubwa kwa wanahabari na hali hiyo ikiendelea kuna hatari ya haki nyingi za wananchi kuhodhiwa bila maelezo ya msingi.

Baada ya malalamiko hayo ya waandishi dhidi ya udhalilishaji huo, ofisi ya mkurugenzi ililazimika kuomba radhi kwa kilichotokea na kuahidi hakitajirudia tena katika siku zijazo.
 
Lenana

JF-Expert Member
Oct 10, 2010
421
78
Diwani wa tlp kata ya sokoni aache ubabaishaji nani kamloga kiumbe huyu msimamo hana na sidhani kama kweli yu na chadema kama anavyojinasibu?
 
Mwita Maranya

JF-Expert Member
Jul 1, 2008
10,565
7,938

Hii style ya Allassane Dramane Ouattarra Mr. ADO imetulia sana.

Vinginevyo sisiem wataendelea kujifanyia mambo kiholela tu wakiwahadaa wadanganyika kwamba wanalinda amani na utulivu.

Chadema Arusha hakuna kurudi nyuma, kitaeleweka tu hata kama wakiamua kulindwa na polisi saa 24,kwakuwa hiyo ni ofisi ya umma watalazimika kuelewa tu na kuachia ngazi. Halafu afande mwema si alisema hana polisi wa kutosha kulinda usalama wetu. Sasa ngoja wawahamishie hao wachache waliopo hapo ofisi za manispaa halafu uone vijana wa kazi wanavyorudi kutikisa mitaa.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom