ARUSHA: Hiace (Daladala) Ya Usa-River to Mjini Yatekwa Usiku Kuamkia Leo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

ARUSHA: Hiace (Daladala) Ya Usa-River to Mjini Yatekwa Usiku Kuamkia Leo

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Puppy, Jan 29, 2012.

 1. Puppy

  Puppy JF-Expert Member

  #1
  Jan 29, 2012
  Joined: Oct 6, 2011
  Messages: 2,267
  Likes Received: 653
  Trophy Points: 280
  Habari Zenu Wanajamvi.


  Jana majira ya saa mbili na nusu usiku, nilimsindikiza shangazi kupanda daladala kutoka Usa-River kurudi kwake mjini. Daladala walopanda ni ya kawaida sana yenye kupiga routes za kikatiti kila siku, nimeitambua kwa kuiona ila kwa bahati mbaya sikukariri jina.
  Ilipofika mida ya saa tano usiku nikaona missed call ya namba mpya, nikaipiga hiyo namba kila naeongea nae analia simwelewi, nikakata kwanza nijipange. Nikapiga tena akapokea mwanaume akasema yuko Tengeru chini walitekwa.
  Nikatafuta washkaji kama watano hivi tukaenda na mapanga, kufika tukakuta Abiria wote wako chini. Dereva gari na majambazi hawako. Hakuna aliepigwa wala kuumia. Wamenyanganywa kila kitu wameachwa na nguo tu.
  Wanasema majambazi yalimshikia dereva bastola wakamuamuru ashushie gari Tengeru sokoni kama unaelekea CDTI au LITI, walipofika mbele kahawani ndio wakaamriwa watoe kila walichonacho, mpaka fungu la mchicha walinyanganywa.
   
 2. ntamaholo

  ntamaholo JF-Expert Member

  #2
  Jan 29, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 10,142
  Likes Received: 2,104
  Trophy Points: 280
  mradi wa mabasi makubwa usambae hadi mikoani. Halafu arusha nyie bangi sana, ndo matokeo yake hayo. Kila mtu muuza banghi, mirungi na madawa mengine, kuepuka dhahama kama hizo, saidieni kupambana na watumia mihadarati
   
 3. Dr.Chichi

  Dr.Chichi JF-Expert Member

  #3
  Jan 29, 2012
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 2,336
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 145
  du wamshukuru Mungu wapo salama hiyo siyo style ya majambazi waarusha,kawaida wangechezea kichapo kwanza
   
 4. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #4
  Jan 29, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  na huyo dreva apepona?
   
 5. Puppy

  Puppy JF-Expert Member

  #5
  Jan 29, 2012
  Joined: Oct 6, 2011
  Messages: 2,267
  Likes Received: 653
  Trophy Points: 280


  Dereva, majambazi pia gari hawajulikani waliko
   
 6. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #6
  Jan 29, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,506
  Likes Received: 2,246
  Trophy Points: 280
  Aisee! Poleni sana! Kwa arusha saa mbili usiku mbona ni mapema tu jamani? Hiyo barabara ya cdti inapaswa kuwekwa taa za barabarani manake hakuna movements hapo kati.
   
 7. Puppy

  Puppy JF-Expert Member

  #7
  Jan 29, 2012
  Joined: Oct 6, 2011
  Messages: 2,267
  Likes Received: 653
  Trophy Points: 280


  Dr. Chichi hii style ipo siku hizi maana hata raia hawataki longolongo, jambazzi akitokea anaulizwa anataka nini anapewa anasepa vitatafutwa tena.
  Sasa ubishane nao wakukate mapanga wakati madaktari wa pale West Meru wako mgomoni nani atakaekupiga stiches??
   
 8. Puppy

  Puppy JF-Expert Member

  #8
  Jan 29, 2012
  Joined: Oct 6, 2011
  Messages: 2,267
  Likes Received: 653
  Trophy Points: 280


  Meku sio kila mwizi ni mtumia mihadarati. Unataka kusema hata yule alepiga MIL90 za bodi ya mkopo ni mtu wa mihadarati??
   
 9. Puppy

  Puppy JF-Expert Member

  #9
  Jan 29, 2012
  Joined: Oct 6, 2011
  Messages: 2,267
  Likes Received: 653
  Trophy Points: 280


  Na ile kahawa pale inaleta giza mbaya kabisa
   
 10. Jumakidogo

  Jumakidogo R I P

  #10
  Jan 29, 2012
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 1,859
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Apepona au amepona?
   
 11. Shinto

  Shinto JF-Expert Member

  #11
  Jan 29, 2012
  Joined: Dec 6, 2010
  Messages: 1,781
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Huko si kwa Lema? Pipooooooooz pwaaaaaaaa!
   
 12. Captain22

  Captain22 JF-Expert Member

  #12
  Jan 29, 2012
  Joined: Aug 25, 2011
  Messages: 618
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 45
  Pole sana mkuu. Ila mashangaa highway patrol walikuwa wapi?
   
 13. Captain22

  Captain22 JF-Expert Member

  #13
  Jan 29, 2012
  Joined: Aug 25, 2011
  Messages: 618
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 45
  Kama hujui uliza kwanza. Nani alikwambia Usa river na Tengeru ni jimbo la Mh. Lema? Jifunze Jiografia ya nchi yako.
   
 14. n

  ndomyana JF-Expert Member

  #14
  Jan 29, 2012
  Joined: Jan 24, 2012
  Messages: 4,731
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  Kwa marehemu sumari uko, kwa lema kupo safi skuizi aman tupu. Magamba hayajachafua hali ya hewa
   
 15. bht

  bht JF-Expert Member

  #15
  Jan 29, 2012
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 10,341
  Likes Received: 209
  Trophy Points: 160
  Shule alosoma haikua na ramani ya karatasi wala lile tufe, vitabu vya kiada Au ziada. Sasa angejuaje!!
   
 16. Filipo

  Filipo JF-Expert Member

  #16
  Jan 29, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 9,330
  Likes Received: 210
  Trophy Points: 160
  Pole shangazi yake Puppy na abiria wengine! Tuombe dereva awe mzima! Hili tukio lilimtokea bro wangu kama miezi mitatu iliyopita maeneo ya Ngulelo. Andengenye yupo bize na cdm!
   
Loading...