ARUSHA hawana MBUNGE, wamebaki na CHADEMA...

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
6,135
17,802
Mwishoni mwa juma nilikuwa jijini Arusha.Kwenye safari zangu za kimapato.Nikajifunza jambo moja.Kwamba CCM,kiwe kimehusika na hukumu iliyomsimamishia ubunge Lema ama la,haina mvuto Arusha.Ingawa Jaji Rwakibalira alimsimamisha Lema kuwa Mbunge,bado wana-Arusha wameishikilia CHADEMA mioyoni mwao.Wanaoongozwa na Lema kama kocha aliye nje ya 'pitch'-kwenye 'touch line'.

Hakuna mradi unaopitishwa Arusha bila idhini ya CHADEMA.Hata sisi wasomi wa Sheria tunahakikishiwa ulinzi pale Arusha na CHADEMA.Siioni dalili ya CCM kupata Ubunge pale hata kama uchaguzi utarudiwa baada ya Rufaa ya Lema Mahakama ya Rufani kukataliwa(?).CHADEMA inaliwaza,inaokoa,inaongoza na itashika nchi muda si mrefu.Natamani Kibaha kwangu kuwe kama Arusha....
 
Vuta Nkuvute CDM Kibaha ipo ila sema nguvu ya uchakachuaji ilozi nguvu ya umma 2010.

Kwa mbali naona tumaini jipya hata kama halipo ila limejengwa kama ule mji mpya chini ya imani ya Kikristo.
 
Hata Kibaha yako itakuwa hv hv katika chaguzi ingine inayokuja!
Leo hii hakuna kijana wa rika langu atakayesimama na kuipa kura ccm.

Tukienda mbele kidogo hii chama cha mafisadi itakuwa historia ya kwmb tulikuwa na chama chenye rangi ya kijani.
 
Kwa aibu ya kuongozwa na CCM, nimeamua kuhamisha kambi yangu na kutuma makombora kutokea Kawe kwa Halima.Nitashiriki ipasavyo kuikomboa Kibaha yangu.Promise...
 
karibu tena chuga kwa Hon/mh/kamanda/kipenzi cha Arusha/asiye ogapa kutishiwa kifo/..... GODBLESS ARUSHA MJINI LEMA mbunge ambaye ikulu inatamani arudishiwe haki yake ya ubunge apunguze speed ya KUKIJENGA CHAMA TANZANIA NZIMA...
 
arusha ipo kivyake kaka.. Mkoa wa tofauti.. Hawana wa wakilish. Mbunge hawana, madiwan hawana[except maeneo machache], sa jiulize wanasonga vipi..
 
tangu kuondolewa aliyekua mbunge wa arusha mjini mh lema mazingira ya mji wa arusha yamezidi kua machafu kupitiliza.leo asubuh nimepitia maeneo ya sokoine rod wakati naenda kazini barabara imejaa taka nying sana maganda ya machungwa ndiz nk.najiuliza mbona kabla hawajamtoa mbunge hali ilikua nzuri?vipi leo mji uwe hivi?halimashauri inafanya nini?au wako bize kutafuta kitu kidogo kwenye miradi ya barabara za ndani ya mji
 
Wengi watadhani unampigia Mb Lema kampeni ila ni ukweli mji wa Arusha umepoteza hadhi ni mchafu na umekuwa ovyo ovyo.
 
mitaro michafu,chember zimeziba,taka zimejaa kila kona ya mji halmashauri manispaa wamejisahau hakuna wanachofanya zaidi ya kufikiria matumbo yao
 
Inasikitisha sana kwa kweli na ccm wanajidanganya kwamba wanawakomoa wana Arusha
 
Tatizo kubwa la wana Arusha ni kuwa walishaaikataa CCM katika maisha yao na hata kama Lema asiwepo kisha aurhusiwe kugombea ubunge na Lowasa Lema atashinda na Lowasa atashindwa vibaya sana pamoja na hela zake.

Hukumu yao haipo mbali.
 
hii inatisha sana hasa eti huu ndio mji wa kitalii?nakumbuka lema alivyoingia 2 mitaro ikaanza kujengwa jiji likawa safi mpaka iliweka sheria ukivuta sigara mjini ukatupa kichung huna bahati.leo hata ukivutia office ya mkoa pouw2.tena ndipo panchafu kupita maelezo
 
Uchafu wa mji wa arusha hausiani na mbunge bali mkuu wa mkoa ambae katokea ccm. Zaidi ya kua na propaganda sioni cha maana anachofanya... Arusha ndio mji mkuu na wa maendeleo ukiachia dar sasa sijui kwanini serikali haiangalii vizuri.. Ningekua mi ni rais ungekuta mkuu wa mkoa wa arusha nishampiga chini siku nyingi
 
Hata wakazi wa Ubungo wanalalamika Ubungo imejaa taka maji hakuna barabara mbovu.
 
hii inatisha sana hasa eti huu ndio mji wa kitalii?nakumbuka lema alivyoingia 2 mitaro ikaanza kujengwa jiji likawa safi mpaka iliweka sheria ukivuta sigara mjini ukatupa kichung huna bahati.leo hata ukivutia office ya mkoa pouw2.tena ndipo panchafu kupita maelezo

Sijui Mimi naishi Arusha ipi, namjua Lema vizuri na kimsingi sikuwa anaona anachokifanya Kmart Mbunge tofauti na kukukutana na wale vijana wake wa unga limited na kutafuta fujo
 
Uchafu wa mji wa arusha hausiani na mbunge bali mkuu wa mkoa ambae katokea ccm. Zaidi ya kua na propaganda sioni cha maana anachofanya... Arusha ndio mji mkuu na wa maendeleo ukiachia dar sasa sijui kwanini serikali haiangalii vizuri.. Ningekua mi ni rais ungekuta mkuu wa mkoa wa arusha nishampiga chini siku nyingi

Mkuu JF kuna Great Thinkers...

Umeipata wapi hii kuwa "Arusha ndio mji mkuu wa maendeleo ukiachia Dar"

Tufahamishe mkuu.
 
Back
Top Bottom