Arusha: Familia ya Watu 12 yakosa makazi baada ya kuvamiwa na kutolewa vitu nje

Jembe Jembe

JF-Expert Member
Jun 9, 2016
749
1,797
Familia moja yenye watu 12 iliyoko mtaa wa Simanjiro kata ya Sombetini jijini Arusha imekosa mahali pa kuishi baada ya Watu wanaodaiwa kuwa madalali wa mahakama kuvamia nyumba Yao na kuwaondoa Kwa nguvu na Kisha kutupa nje vitu vyao.

Familia hiyo imejikuta kwenye wakati mgumu baada ya kutolewa vitu nje kwa madai kuwa nyumba wanayoishi imeuzwa na benki ya Akiba Commercial Bank miaka Saba iliyopita Kwa thamani ya sh, milioni 120.

Hatahivyo,familia hiyo imeeleza ya kwamba wametolewa nje ya nyumba hiyo kibabe bila kuzingatia haki ya msingi ikiwemo kutopewa notisi ya kusudio la kuondolewa katika Nyumba Yao inayotolewa na mahakama.

Akihojiwa na waandishi wa habari Eliasa Mkilya ambaye alijitambulisha kama mmiliki wa nyumba hiyo alisema kwamba leo majira ya saa nne asubuhi kundi la zaidi ya watu 12 walifika katika makazi yake na kujitambulisha kama madalali wa mahakama kutoka kampuni ya KBM-SONS & COMPANY LTD ya jijini Dar es salaam ambapo wakiongozana na mtendaji wa mtaa wa kata ya Sombetini Robert Naftari ambapo waliwataka watoke nje na ghafla wakaanza kutoa vitu nje ya nyumba yao.

Aidha Mkillya ameituhumu kampuni hiyo ya udalali Kwa kufanya uharibifu mkubwa wa vyombo vya ndani pamoja na upotevu wa sh, milioni 1.6 fedha alizodai kuibiwa na Dalali huyo wakati wakiondoa vitu ndani .

Hata hivyo,meneja wa kampuni ya udalali ,Mbaraka Olotu alipinga vikali madai hayo huku akifafanua kwamba kampuni yao imefuata taratibu zote za kumuondoa mkazi huyo.

“Tarehe 23 Agosti mwaka huu tulimpatia notisi ya kuondoka na tukamwambia aondoe vitu vyake lakini hakutimiza masharti lakini tulipeleka nakala ofisi ya mkuu wa wilaya,mwenyekiti wa mtaa na polisi “alifafanua Olotu

Mkillya,alidai kwamba hajawahi kupewa notisi ya kuhama katika nyumba yake cha ajabu alielezwa kwamba notisi hiyo alikabidhiwa mtendaji wa kata hiyo jambo ambalo hakukubaliana nalo.

“Walipojitambulisha niliwaomba notisi ya kuniondoa wakadai walishampa mtendaji wa kata na waliibandika kwenye mlango jambo ambalo sio kweli “alisema Mkillya

Alieleza ya kwamba anachofahamu yeye alikopa fedha mwaka 2012 kiasi cha sh, milioni 120 kupitia benki ya Akiba Commercial Bank tawi la Arusha na amejitahidi kulilipa deni hilo mpaka sasa amebakiza jumla ya kiasi cha sh,61 milioni.

Mkillya amepinga vikali nyumba yake kuuzwa kiasi cha sh,120 milioni kwa kuwa thamani yake halisi ni zaidi ya sh,300 milioni.

“Kitu cha ajabu zaidi ninachoshangaa nyumba yangu ina thamani ya kiasi cha sh,300 milioni lakini wameuza sh,120 milioni huu ni uhuni “alieleza Mkillya

Naye Latifa Mkillya ambaye alijitambulisha kama mtoto wa Mkillya alisema kwamba wanapinga kuondolewa kibabe kwa kuwa hawajapewa notisi yoyote ya kuondolewa kwenye nyumba yao japo anakiti kuwwpo mgogoro Kati ya baba yake na benki hiyo.

Alimuomba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Samia Suluhu Hassan kuingilia kati ili haki iweze kutendeka.

Alipotafutwa afisa mtendaji wa kata ya Sombetini jijini Arusha,Naftari Robert kwa njia ya simu alijibu kwa kifupi kwamba hayuko katika mazingira mazuri ya kuzungumzia suala hilo na kisha kukata simu ghafla.

Mwisho.

IMG_20211021_153908_766.jpg
IMG_20211021_160743_705.jpg
IMG_20211021_153938_923.jpg
IMG_20211021_153943_441.jpg
IMG_20211021_160723_388.jpg
 
Kwa uzoefu wangu Hakuna mtu anayeuziwa nyumba akakubali kwamba taratibu zimefuatwa.
Milioni 120 Kwa miaka tisa nyumba imeenda kihalali tuache kulea ujinga.
Tukumbuke hizo ni amana za wateja wa bank, ikifilisika Kwa mikopo chechefu (isiyolipika) wenye amana hizo watapata hasara.

Kabla ya kukopa ujue kabisa unabet, ukiliwa usianze kutupigia kelele maana ungetusua usingetupigia kelele.
 
Mikopo haijawahi kumuacha mtu salama na mbaya zaidi mkopo haunaga fundi. Mungu awape wepesi ktk maisha yao mapya waathirika hao.
 
Alafu utakuta Kigagula fulani wa ufipa anaponda utawala wa Magufuli.

R.I.P JPM

Huyo mzee muhuni tu; nyumba imeuzwa miaka 7 iliyopita analalamika nini? Ina maana miaka 7 yote hakulipa mkopo wowote wala kodi
 
Familia moja yenye watu 12 iliyoko mtaa wa Simanjiro kata ya Sombetini jijini Arusha imekosa mahali pa kuishi baada ya Watu wanaodaiwa kuwa madalali wa mahakama kuvamia nyumba Yao na kuwaondoa Kwa nguvu na Kisha kutupa nje vitu vyao.

Familia hiyo imejikuta kwenye wakati mgumu baada ya kutolewa vitu nje kwa madai kuwa nyumba wanayoishi imeuzwa na benki ya Akiba Commercial Bank miaka Saba iliyopita Kwa thamani ya sh, milioni 120.

Hatahivyo,familia hiyo imeeleza ya kwamba wametolewa nje ya nyumba hiyo kibabe bila kuzingatia haki ya msingi ikiwemo kutopewa notisi ya kusudio la kuondolewa katika Nyumba Yao inayotolewa na mahakama.

Akihojiwa na waandishi wa habari Eliasa Mkilya ambaye alijitambulisha kama mmiliki wa nyumba hiyo alisema kwamba leo majira ya saa nne asubuhi kundi la zaidi ya watu 12 walifika katika makazi yake na kujitambulisha kama madalali wa mahakama kutoka kampuni ya KBM-SONS & COMPANY LTD ya jijini Dar es salaam ambapo wakiongozana na mtendaji wa mtaa wa kata ya Sombetini Robert Naftari ambapo waliwataka watoke nje na ghafla wakaanza kutoa vitu nje ya nyumba yao.

Aidha Mkillya ameituhumu kampuni hiyo ya udalali Kwa kufanya uharibifu mkubwa wa vyombo vya ndani pamoja na upotevu wa sh, milioni 1.6 fedha alizodai kuibiwa na Dalali huyo wakati wakiondoa vitu ndani .

Hata hivyo,meneja wa kampuni ya udalali ,Mbaraka Olotu alipinga vikali madai hayo huku akifafanua kwamba kampuni yao imefuata taratibu zote za kumuondoa mkazi huyo.

“Tarehe 23 Agosti mwaka huu tulimpatia notisi ya kuondoka na tukamwambia aondoe vitu vyake lakini hakutimiza masharti lakini tulipeleka nakala ofisi ya mkuu wa wilaya,mwenyekiti wa mtaa na polisi “alifafanua Olotu

Mkillya,alidai kwamba hajawahi kupewa notisi ya kuhama katika nyumba yake cha ajabu alielezwa kwamba notisi hiyo alikabidhiwa mtendaji wa kata hiyo jambo ambalo hakukubaliana nalo.

“Walipojitambulisha niliwaomba notisi ya kuniondoa wakadai walishampa mtendaji wa kata na waliibandika kwenye mlango jambo ambalo sio kweli “alisema Mkillya

Alieleza ya kwamba anachofahamu yeye alikopa fedha mwaka 2012 kiasi cha sh, milioni 120 kupitia benki ya Akiba Commercial Bank tawi la Arusha na amejitahidi kulilipa deni hilo mpaka sasa amebakiza jumla ya kiasi cha sh,61 milioni.

Mkillya amepinga vikali nyumba yake kuuzwa kiasi cha sh,120 milioni kwa kuwa thamani yake halisi ni zaidi ya sh,300 milioni.

“Kitu cha ajabu zaidi ninachoshangaa nyumba yangu ina thamani ya kiasi cha sh,300 milioni lakini wameuza sh,120 milioni huu ni uhuni “alieleza Mkillya

Naye Latifa Mkillya ambaye alijitambulisha kama mtoto wa Mkillya alisema kwamba wanapinga kuondolewa kibabe kwa kuwa hawajapewa notisi yoyote ya kuondolewa kwenye nyumba yao japo anakiti kuwwpo mgogoro Kati ya baba yake na benki hiyo.

Alimuomba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Samia Suluhu Hassan kuingilia kati ili haki iweze kutendeka.

Alipotafutwa afisa mtendaji wa kata ya Sombetini jijini Arusha,Naftari Robert kwa njia ya simu alijibu kwa kifupi kwamba hayuko katika mazingira mazuri ya kuzungumzia suala hilo na kisha kukata simu ghafla.

Mwisho.

View attachment 1983354View attachment 1983355View attachment 1983356View attachment 1983357View attachment 1983358
Huyo mzee tapeli. Ana uwezo wa kukopa mil 120 lakini akafanya uzembe.

Benk hawawezi kukukopesha pesa nyingi hivyo kama hawana uhakika unaweza kulipa
 
Back
Top Bottom