ARUSHA: Diwani mwingine wa CHADEMA kata ya Moita jimbo la Monduli amejiuzulu

Good riddac
Ni diwani wa kata ya Moita ambapo ni mojawapo ya kata zilizo katika jimbo aliyekuwa mbunge wa Monduli na waziri mkuu mstaafu Mh Edward Ngoyai Lowassa.

Akizungumza na shirika la utangazaji la TBC, diwani huyo amesema amefikia hatua hiyo baada ya kuona anakosa ushirikiano toka kwa Mwenyekiti wa halmashauri na mbunge wake. Hata hivyo madiwani wengine wamekuwa wakimpa ushirikiano.

Mkurugenzi wa halmashauri ya Monduli Steven Ulaya amethibitisha kwa njia ya simu kupokea barua ya kujiuzulu kwa diwani huyo. Na amezitaka mamlaka zinazohusika kuandaa utaratibu wa uchaguzi katika kata hiyo.

Wananchi wa kata yake wamefurahiwa na maamuzi hayo na kumtaka kuachana na siasa za malumbano.

Good riddance! Uzuri ni kwamba kajiuzulu peke yake lakini wapiga kura wake wako pale pale. Tusubiri uchaguzi
 
Siku hizi hawataki kusingizia kujiuzulu kwa ajili ya kuunga mkono utendaji wa Magufuli,Kama kajiuzulu kwa kukosa ushirikiano na Mwenyekiti wa halmashauri,kwani na wananchi waliomchagua hawampi ushirikiano?wenye akili wameshaelewa kilichopo ndani ya kapeti ndiomaana taarifa yenyewe imetangazwa na TBC CCM.
 
sijaelewa kabisa hawa madiwani wananunuliwa tsh ngapi?
Nawaza ningekuwa mimi diwani dau langu lingekuwa tsh ngapi.

Hii sasa sio mchezo pamoja na kuwaonya wasiondoke bado wanasepa.

Hii imetokea hadi Monduli tunakodhani ni eneo makini km sio ngome ya mtu makini.

Najiuliza mwisho wake upi?

IMG_20170726_115848_383.JPG

sweeper
 
Mbowe akili yake imegota.
Chama amwachie Tundu Lisu.
Katibu mkuu awe Juma Mwalimu.

Mbowe hana sifa tena za kuwa kiongozi kwa sababu amethitika kuwa alikwepa kodi kwa muda mrefu.
Alitumia siasa kama kichaka cha kuhujumu uchumi wa nchi.

Mbowe kaa pembeni kwa maslahi mapana ya chama chako.
Tafadhali Mbowe ridhika tu na ubunge wako na ujenge maendeleo ya jimbo lako.
Itisha kikao ili upate maoni ya wajumbe wako.
Kuna tatizo kubwa sana.
Mpaka madiwani wanajiuzulu au hata kununuliwa basi kuna shida.
Hakuna mtu mjinga wa kuacha maslahi ya udiwani kama hakuna tatizo.

Mbowe kumbuka 2020 sio mbali mtabaki na kauli mbiu ya Magufuli ni dikteta lakini mkumbuke wananchi hawajui hata maana ya udikteta ni nini?
Wananchi na hao madiwani wenu wa huko vijijini wote uelewa wao umeushia kwenye kata zao na hawana shida na mambo ya kitaifa kama udikteta na ukabila sijui udini. Hayo hayana tija kwa mwananchi wa kijijini.

Kuna mambo mengi ya kufanya kama chama na sio kupambana mkuu wa nchi kwa lugha za kejeli.

Chadema kimekosa mbinu ndio maana kinapinga hata maendeleo ya wanyonge.
Kuna mahali nilishauri kuwa kama pesa za mikutano zipo kwa nini wasizitumie kujenga shule za wasichana waliobakwa na kuzaa bila hiyari yao?

Hivi mtu kama Lowasa au Sumaye au Mbowe anashindwa kufanya harambee za kujenga shule au kuwalipia wanafunzi waliozalishwa nyumbani badala ya kutoa matamko ya kuwaudhi watanzania wengi ambao kwa imani yao au kwa ushabiki wao au kwa maoni yao wanaona kuwa hao wanafunzi hawana haki ya kupata elimu tena maishani mwao?

Kuna wanafunzi wengi wa vyuo vikuu walikosa mikopo lakini sikusikia Lowasa wala Mbowe wala Sumaye wakiitisha waandishi wa habari na kuwataka watanzania hasa wanachadema na wapenda haki kutoa michango yao ili wanafunzi maskini wasome chuo kikuu?
Badala yake wanatoa matamko ya kutatanisha ambayo hayana tija kwa taifa letu hasa kwa watu wa vijijini maaskini?

Nadhani Polepole alisikia ushauri wangu akauchukua na kuahidi kuwa CCM itawalipia baadhi ya wanafunafunzi watakaokosa mikopo.
CCM kitazidi kutawala mana waliotegemewa kuwa wana wa Nuru wamekosa maarifa,hekima na busara.

Hivi ni kipi cha msingi kati ya kutumia ruzuku kwa kuwasomesha watoto wa maskini au kuandaa maandamano ambayo yataishia kwa kupigwa mabomu?

Kwa mtizamo wangu naamini kuwa Mbowe ameshafikia ukomo wa kuvuta watu kujiunga na Chama chake cha Chadema japo ni ukweli kuwa amekijenga mpaka hapo kilipo.

Sababu za msingi za kumtathimini Mbowe kuwa hana uwezo tena ni kila mtu atambue kuwa Tanzania ni nchi ya kijamaa. Hivyo ili upate uungwaji mkono ni lazima uwe mjamaa na uwe unazijua shida za watanzania kwa kuziishi sio kuzisoma kwenye magazeti kama alivyo Mbowe.

Ama uwe mjamaa wa kuzaliwa na uishi kama wananchi wa kawaida au ufanye mambo yanayoonyesha ujamaa wetu. Hapa ndipo palipokuwa panampa sifa Lowasa kwa kuchangia michango kwenye shughuli za kijamii.

Mbowe ni mtoto aliyezaliwa na kukulia kwenye familia ya kitajiri sana.
Hana hata chembe ya kuujua umaskini kwa kuuishi. Na ninavyojua tangu shuleni huwa hakuna urafiki na upendo wa dhati kati ya maskini na tajiri.
Maskini atampenda tajiri pale tu atakapo muona anajitoa na kusaidia hasa kwenye masuala yanayohitaji gharama na michango. Ndio maana leo hii mh. Rais anapofika mahali anajitolea kutoa michango kuchangia shughuli za kijamii. Anaijua vyema hulka ya watu maskini.

Mbowe hajawahi kuishi maisha ya kijijini kama kijijini. Amekua ni mtu wa kukaa katikati ya jiji na kuishi maisha ya juu sana tofauti na alivyo mtu kama Tundu Lisu na wengine.

CCM inavipaji vingi ambavyo chimbuko lake ni watoto wa maskini wanaoishi vijijini.
Chadema wengi wao ni mazao ya watoto wa mjini waliosoma kwa raha na maisha yenye ahueni kubwa.

Mbowe kwa kweli ameshagota hakuna ubishi na hana mpango wa kutafuta vipaji zaidi kama alivyokuwa amewapata wakina Zito na Kafulila ambao ni watu waliotokea mikoa maskini.
Viongozi waluopo ni wakina Halima Mdee ambao ni watoto wa Maprofesa. Hawajui shida za kina mama wa kijijini.

Tundu Lisu anafaa sana kuongoza chama.
Professa Safari na Baregu wanafaa sana kuendelea kujenga Sera za kukosoa sera za CCM lakini sio kuwaacha vijana kumkejeli rais bila kutoa sera.
Mfano Magufuli anaposema hata somesha wale watakaozalia shuleni. Tulitaka kuona Chadema wakisema wao wakiingia madarakani watafanyaje na sio kuanza kutusomea vifungu vya sheria vilivyowekwa na hao hao CCM ambao wameamua kuachana navyo.

Rais ambaye ni mwenyekiti wa CCM amezuia Makinikia ambayo wao wenye waliyaruhusu yaende sasa badala ya wapinzani kutuambia wao wangefanyaje ili kuzuia tusiibiwe kupitia mikataba wanabaki kutusomea mikataba hiyo mibovu ambayo walioiweka wameamua kuilosoa na kuipiga vita. Hata kama ni usanii lakini wananchi wanataka kusikia kuwa makinikia hayaendi nje ya nchi kirahisi tu bila kulipa kodi.

Mbowe kaa na madiwa wote nchi nzima pamoja na wajumbe wa mkutano mkuu. Muwashauri madiwani wenu na mutoe ufafanuzi wa yale mnayoyaamini kama chama juu ya kile kinachoitwa kupinga pinga tu kila kitu kinachofanywa na serikali kwa nia njema.
Viongozi wengi wa Chadema huko vijijini hawajaelewa nini mwelekeo na msimamo wa chama chenu kuhusu vita dhidi ya majipu na utumbuaji wake.
Kule vijijini wanaangalia TBC na kusikiliza TBC Taifa wanachosikia ndicho wanachoamini.
Wanaamini kuwa Chadema wanatetea wezi. Wanaishia hapo mana hakuna ufafanuzi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimesoma mpaka mwisho sijaelewa ulichoandika kabda baadae ndio ntaelewa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kumbe habari ipo TBC, ngoja tusubiri na uhuru kesho waitoe kama walivyofanya na tisheti ya UKUTA.
 
Sizonje anahangaika sana...,kiwanda cha 6 hiki

Sent from my Siemens A-35 using JamiiForums mobile app
Nchi inajengwa na watu ...LAKINI; sharti watu hawa wawe huru na wasilaghaiwe! Hizi mbinu haziwezi kuleta viwanda.
 
Back
Top Bottom