Arusha: Chadema wacharuka Walivaa Jeshi la Polisi wawambia wache Kutumika

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,249
2,000
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wilaya ya Arusha,kimelalamika kuhujumiwa na Chama cha Mapinduzi(CCM) kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi Mkoani hapa ili kukihujumu chama hicho katika maandalizi ya kushiriki uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika hivi karibuni.

Akiongea na vyombo vya habari Katibu wa chadema wilayani humo,Innosent Kisanyage,amesema kuwa kwa sasa chama hicho kipo kwenye zoezi la uhakiki wa wanachama wake katika kata zote za jiji la Arusha,hivyo chama cha mapinduzi kinalitumia jeshi la polisi kuwakamata viongozi wake wa mitaa kwa madai ya kufanya mkusanyiko usio halali.

Amefafanua kuwa wiki iliyopita katika kata ya Elerai viongozi wa chadema walivamiwa na polisi waliokuwa wameambatana na baadhi ya viongozi wa ccm,wakati viongozi hao wa chadema wakiendelea na zoezi la kuhakiki wa wanachama katika kata hiyo ili kujiandaa na uchaguzi ujazo.

"Chadema ni chama cha kisiasa chenye usajili halali lakini viongozi wake wamekuwa wakifanyiwa hujuma kwa lengo la kukidhoofisha kwa kuwakamata viongozi wake wakiwemo wanachama wakati wakitekeleza majukumu yao,"alisema Kisanyage.

Amelitaka Jeshi la Polisi kushughulika na masuala ya ulinzi wa raia na mali zao na kuacha kutumika kukibeba chama cha mapinduzi kwani kwa kufanya hivyo ni kuendelea kuminya demokrasia na uhuru wa wananchi kujieleza na kuchagua chama wakitakacho.

Naye Diwani wa chadema katika kata ya Eleray ,Jofrey Kalumuna alisema chama cha mapinduzi kinafanya hujuma za wazi kwa kulishirikisha jeshi la polisi jijini hapa kuhakikisha kuwa chadema inashindwa kufanya shughuli zake .

Alilitaka Jeshi la Polisi kufanya kazi yake na kujiweka kando na masuala ya kisiasa kwani zoezi linaloendelea kwa sasa ni kujipanga kwa uchaguzi wa serikali za mitalii ,alisema kinachofanywa na ccm ni uoga wa kushiriki uchaguzi huo ndio maana wanatumia mabavu kukidhoofisha chama cha chadema.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom