Arusha: CHADEMA kuwaburuza CCM Mahakamani. Chamlaani DC Daqaro,Polisi na Mount Meru Hospital kuwabeba CCM

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,898
CHAMA cha demokrasia na Maendeleo CHADEMA wilaya ya Arusha,kimejipanga kwenda mahakamani kupinga matokeo ya uchaguzi mdogo wa marudio uliofanyika katika kata tatu zilizofanya uchaguzi katika jimbo la Arusha mjini ambapo chama cha mapinduzi kilishinda.

Aidha katika shauri hilo washtakiwa ni pamoja na mkuu wa wilaya ya Arusha ,Gabriel Dagaro,wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi,jeshi la polisi na waliokuwa wagombea wa ccm katika kata hizo

Akiongea na waandishi wa habari mapema leo agosti 17, katibu wa chadema wilaya hiyo, Inosenti Kisanyage amesema uamuzi huo umetokana na dosari nyingi zilizojitokeza katika uchaguzi huo wa marudio,ikiwemo kughubikwa na na matukio ya uvunjifu wa amani , ukiukwaji wa sheria ,kanuni na taratibu za uchaguzi.

Aidha amesema kuwa uchaguzi huo ulitawaliwa na ubabe kwa wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi kwenye vituo kwa kushindwa kusikiliza malalamiko ya mawakala ,kukataa kutoa fomu za malalamiko na wakati mwingine kuzichana hadharani pindi wakala anapokuwa amepatiwa.

Kwa mujibu wa Kisanyage kata zilizofanya uchaguzi wa marudio katika jimbo la Arusha ni pamoja na kata ya Kaloleni,Daraja mbili na Osunyai JR ambapo chama hicho kilishinda ila matokeo yalibadilishwa kwa hila na kupatiwa ushindi wagombea wa CCM.

‘’Chama kimejipanga kwenda mahakamani kufungua mashtaka kwani jambo hilo la kupoka ushindi wa chadema limekuwa na mazoea kila uchaguzi unaporejewa, awamu hii hatukubali lazima tuwaburuze mahakamani,wasimamizi wa uchaguzi na waliokuwa wagombea wa ccm’’amesema Kisanyage

Katika hatua nyingine chadema wamelalamikia uongozi wa hospitali ya mkoa Mount Meru kwa kushindwa kuwapatia matibabu stahiki baadhi ya majeruhi wa chadema walioumizwa kwa kipigo siku ya uchaguzi katika kata ya kaloleni ,jambo ambalo walisisitiza halistahili na lililenga kupoteza ukweli wa matukio yaliyojitokeza siku hiyo .

Wakati huohuo chama hicho kimelaani jeshi la polisi jijini hapa kwa kushindwa kusimamia kikamilifu zoezi hilo la uchaguzi badala yake walishiriki matukio ya uhalifu ikiwemo kushuhudia aliyekuwa mgombea wa chadema,Bonface Kimaro na mbunge wa Arusha Mjini wakivamiwa na kupigwa na kundi linalodhaniwa ni wafuasi wa ccm huku polisi hao wakitazama kwa macho na kushindwa kuchukua hatua.

Kwa upande wake aliyekuwa mgombea wa chadema kata ya kaloleni,Boniface Kimaro amesimulia alivyovamiwa na kupigwa mbele ya polisi,ambapo alisema watu hao wakitumia gari aina ya IST na Toyota Randcruser walivamia msafara wake wakati akitoka kutembelea vituo na kuzuia kwa mbele gari lake aina ya Noar na kuanza kumshambulia kwa mateke ,nguni na kitu chenye nchakali.

‘wakati naelekea kituo kingine barabara ya tanki la maji kundi hilo walizuia gari yangu kwa mbele na nilipoteremka waliniambia kwamba ..si ulisema usiposhinda utafia kwenye kata hiyo sasa tumekuja kutekeleza’’alisema Kimarao ambaye bado anamaumivu wa makali shingoni yaliyotokana na kipigo.
 
Mahakama watakachofanya ni rahisi tu.Kesi itakuja kuamuliwa 2024 hiyo kama ya kina Maalim inayosubiri uamuzi 2023
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom