ARUSHA:Brigedia Mbungo akabidhi bilioni 1.3 kwa wahanga waliopogwa

Jembe Jembe

JF-Expert Member
Jun 9, 2016
749
1,797
TAASISI ya Kuzuia na kupamba na Rushwa Mkoa wa Arusha TAKUKURU,imefanikiwa kurejesha na kuzikabidhi kwa wahanga kiasi cha shilingi bilioni 1.3 fedha za Umma ambazo ni kodi mbalimbali za serikali na dhuluma zilizochepushwa kwa njia ya rushwa na kufanyiwa ubadhilifu na watuhumiwa mbalimbali Mkoani Arusha.



Akiwa jijini Arusha , mkurugenzi mkuu waTAKUKURU Brigedia Jenerali John Mbungo alikabidhi fedha hizo la wahanga zaidi ya 90 na kuwasihi wananchi kuitumia taasisi hiyo kupinga vitendo vya rushwa, na moja ya fedha zilizorejeshwa ni pamoja na fedha za Umma za Mashirika ya Hifadhi ya PSSSF na NSSF shilingi milioni 293 .



Alisema TAKUKURU imeziokoa fedha hizo kufuatia uchunguzi uliofanywa na taasisi hiyo baada ya kugundua vitendo vya rushwa vilivyopelekea uingiaji mikataba mibovu pamoja na udanganyifu wa dhamana,watumishi walichepusha kwa njia ya rushwa na waajiri mbalimbali wasio kuwa waaminifu



Alisema pia TAKUKURU imefanikiwa ulipwaji wa shilingi milioni 7.6 ambazo ni za Mfuko wa Taifa Shirika la Hifadhi za Jamii{NSSF},fedha hizo ni makato ya michango ya watumishi yaliyopaswa kuwasilishwa katika mfuko huo tawi la Mkoani Arusha kama sheria inavyoelekeza lakini zilichepushwa kwa njia ya rushwa ma waajiri kinyume na sheria.



Alisema katika hatua nyingine TAKUKURU imakabidhi shilingi milioni 11 ambazo ni sehemu ya zaidi ya shilingi milioni 112 ambazo ni fedha za umma za matrekta zilizotolewa na Mfuko wa Pembejeo wa Taifa{ Agricultural Inputs Trust Fund-AGITF} zilizostahili kurejeshwa serikali,kati ya fedha hizo shilingi milioni 101.5 tayari zimeshawekwa katika akaunti ya serikali.



Brigedia Mbungo alisema kuwa fedha hizo zilitolewa na serikali kwa wakulima toka mwaka 2018 kw alengo la kuwasaidia wakulima kuondokana na kilimo cha utumiaji wa jembe la mkono lakini hawakulipa kwa wakati hadi kusakwa na taasisi hiyo na kurejesha kwa nguvu.



Akizungumzia kodi,tozo na faini za serikali katika uchunguzi uliofanywa na TAKUKURU Jijini Arusha kwa kushirikiana na Mamlaka ya mapato Tanzania{TRA} Mkoani Arusha wamebaini makosa ya rushwa ya ubadhilifu pamoja na uhujumu uchumi yaliyosababisha upotevu wa fedha za kodi ya serikali zaidi zaidi ya shilingi milioni 519.



Brigedia Mbungo Alisema fedha hizo ni kodi ya serikali,ambayo kwa njia za rushwa zilikwepwa kulipwa TRA Arusha kutoka kwa makampuni mbalimbali ya utalii,makampuni ya ujenzi pamoja na makampuni ya kilimo yaliyopo hapa Jijini Arusha.



Mkurugenzi huyo pia alisema wamekabidhi zaidi ya shilingi milioni 227 .8 ambazo ni fedha za wananchi kutokana na dhuluma zilizokuwa zimefanywa kwa njia ya rushwa na waajiri wao,waendeshaji huduma za kifedha pamoja na wabia katika biashara walizokuwa wakifanya.



Vile vile Mkurugenzi huyo amekabidhi kwa wananchi kadi za ATM 100 za mabenki ya NMB na CRDB zilizokuwa zimechukuliwa na wanufaikaji hao kinyume na matakwa ya taratibu za kibenki.



Alisema fedha shilingi bilioni 1.8 zilitolewa kinyume cha sheria na taratibu zinazosimamia vyama vya Ushirika zikiwemo SACCOS ambapo SACCOS za AUWSA na AICC za Jijini Arusha zilipokea fedha hizo na kushindwa kuzirejesha fedha hizo serikalini kwa wakati.



Mwisho



IMG-20210424-WA0107.jpg
IMG-20210424-WA0104.jpg
 
Back
Top Bottom