Arusha bila ushirikiano wa CHADEMA na TLP halmashauri ya jiji itaogozwa na CCM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Arusha bila ushirikiano wa CHADEMA na TLP halmashauri ya jiji itaogozwa na CCM

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ngongo, Nov 8, 2010.

 1. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #1
  Nov 8, 2010
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,635
  Trophy Points: 280
  Heshima kwenu wanajamvi,

  Wakuu halmashauri ya jiji la Arusha itaongozwa na upinzani iwapo vyama vya CHADEMA na TLP vitaunganisha nguvu dhidi ya CCM yenye viti vingi.CCM ilipata viti kumi [10]vya udiwani,CHADEMA ilipata viti nane[8] vya udiwani na TLP iliambulia kiti kimoja[1] cha udiwani.Vitakuwepo viti tisa [9] maalumu kwaajili ya wanawake.CCM itapata viti vinne [4],CHADEMA viti vinne [4] na TLP itapata kiti kimoja.

  Ukiviweka pamoja viti vya CHADEMA na TLP jumla itakuwa viti kumi na nne [14] pamoja na mbunge watakuwa na viti kumi na tano [15] dhidi ya viti kumi na nne [14] vya CCM.Kwa mara ya kwanza katika historia ya Tanzania halmashauri ya jiji la Arusha itaweza kuongozwa na upinzani.

  Nimesoma mabandiko kibao hapa jamvini kwamba CHADEMA iache mara moja ushirikiano na TLP na wengine wameenda mbali zaidi wakitaka NCCR Mageuzi iwekwe kando.

  Naomba michango yenu wanajamvi zipo sababu za msingi kushikilia misimamo ya kichama zaidi utaifa.Nijuavyo mimi kwenye siasa hakuna adui wa kudumu wala rafiki wa kudumu.

  Naomba kuwasilisha.
   
 2. Avanti

  Avanti JF-Expert Member

  #2
  Nov 8, 2010
  Joined: Aug 24, 2010
  Messages: 1,209
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Uwezekano mkubwa ni TLP kuwa na CCM
   
Loading...