ARUSHA: Basi la kiwanda Cha A to Z laua, familia ya Marehemu yamlilia Rais Samia

nyamadoke75

Member
Apr 1, 2020
66
239
Familia ya Marehemu Mzee Jacob Menya (54) ambaye alifariki dunia kwa kugongwa na gari la wafanyakazi ( Staff Bus) la kampuni ya kiwanda Cha kutengeneza chandarua Cha A to Z,imeiomba serikali kuingilia Kati uchunguzi wa kifo Cha ndugu yao baada ya kampuni hiyo kuhusishwa kurubuni polisi na kupindisha ukweli.

Tukio Hilo lilitokea Juni 7 Mwaka huu Katika soko la Samunge jijini Arusha, majira ya saa 11 alfajiri wakati dereva wa Gari Hilo aliyetambulika kwa jina moja la mzee John alipomparamia Marehemu na kukatiza uhai wake wakati akikusanya wafanyakazi kwa ajili ya kuwapeleka kiwandani hapo.

Mtoto wa Marehemu John Jacob alisema hadi sasa hawajui haki yao wataipata vipi kwani hata polisi wanawapiga danadana ndio maana wanaiomba Serikali kupitia Rais Samia kuwasaidia kupata haki ya Marehemu baba yake na kuwachukulia hatua kali wahusika ambao wamekuwa wakiwajibu ovyo.
 

mwanawao

JF-Expert Member
Aug 18, 2010
2,855
4,899
Haya mabasi madereva wake wapo Rafu sana, kuna haja ya kuwafukuza na kuajiri madereva wanaojielewa na wanaozingatia sheria barabarani,

Uendeshaji wao sio wa staha hata kidogo!! Askari wa barabarani watupie jicho kwenye hili, la sivyo kuna siku kilio kikubwa kitasikiwa Arusha kumbe ni jambo lingeweza kuzuiliwa mapema kabisa!
 

Isanga family

JF-Expert Member
Feb 25, 2015
10,114
14,601
Hiyo bus ni hatari sana wanaendesha hovyo sijapata kuona wao hawana ishu ya kusubiri gari ingine ipite au mwenda kwa miguu...
 

Ngongo

JF-Expert Member
Sep 20, 2008
16,576
23,284
Ni kweli mabus ya A to Z yaendeshwa hovyo hovyo.

Mbaya zaidi body za mabus ni pana sana yanamaliza upana wa barabara inabidi ujiweke kando sana wakati wa kupishana nao.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

1 Reactions
Reply
Top Bottom