ARUSHA: Baada ya kuingia aibu ya kuzomewa Karatu, Mkuu wa Mkoa aamuru madiwani wakamatwe

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,903
Habari iliyotufikia hivi punde kutokea Mkoani Arusha zinatanabaisha kuwa Baada ya Ziara ya mkuu wa Mkoa wa Arusha Kuingia doa kwa wananchi kumzomea wakati akizungumza kwa kutoa kauli iliyokuwa inapingana na maelezo yaliyotolewa awali na Waziri mkuu Kasim Majaliwa, Kwaaibu hiyo ya kuzomewa na wananchi hao kumuacha peke yake uwanajani Mkuu huyo wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo aamuru madiwani na wananchi 11 wakamatwe.

Tunapotoa taarifa hii madiwani hao na wananchi 11 wanaletwa Arusha mjini kwenye ofisi ya RCO.

Chakujiuliza kama wananchi wanaona utendaji wako si wakuridhisha kuna ubaya gani kutoa maoni yao?

=======

JESHI la Polisi Mkoa wa Arusha linawashikilia watu 12, wakiwemo viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Mkoa wa Arusha.

Viongozi hao walikamatwa kwa amri ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo wakituhumiwa kuhusika kuchoma moto mashine za kuvuta maji kutoka kwenye chanzo cha Kangdet wilayani Karatu kwa madai kwamba wanatekeleza agizo la Serikali, hatua ambayo imeelezwa kuwa haikufuata utaratibu.

Akizungumza na waandishi wa habari jana mjini Arusha, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo, aliwataja waliokamatwa kuwa ni pamoja na Mwenyekiti wa Chadema Wilaya ya Karatu, Moshi Darabe ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Barai, anayedaiwa kuhamasisha wananchi kuchoma moto mashine hizo zenye thamani ya zaidi ya Sh milioni 16.

Wengine waliokamatwa ni Diwani wa Kata ya Mang’ola, Lazaro Emanuel, viongozi wa vijiji vya kata hizo pamoja na baadhi ya wananchi.

Kamanda Mkumbo alisema kuwa msako wa kuwakamata watuhumiwa wengine waliohusika na tukio hilo bado unaendelea na uchunguzi utakapokamilika watafikishwa mahakamani kwa hatua za kisheria.

Desemba 27, mwaka huu, kundi la wananchi wa vijiji vinne vya kata hizo waliandamana, wakang’oa na kuchoma moto mashine za kuvuta maji katika chanzo cha maji cha Kangdet, kinachotegemewa na vijiji vingine vya Kata ya Barai.

Kutokana na tukio hilo, Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa ikiongozwa na mwenyekiti wake ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Gambo, walitembelea eneo la tukio na baada ya viongozi kueleza kilichotokea, aliagiza kukamatwa kwa watu wote waliohusika na uharibifu huo.

“Sheria lazima ichukue mkondo wake kwani agizo la Waziri Mkuu Kassim Majaliwa lilikuwa wazi na halikusema wananchi wachukue sheria mkononi, jambo hili ni kinyume cha sheria,” alisema Gambo katika mkutano huo.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Karatu, Jubilate Mnyenye (Chadema), amesema kuwa yeye, mbunge wa jimbo hilo, Willy Qambalo na Mwenyekiti wa Kijiji cha Mang’ola, Jacob Pius, wametakiwa kuripoti Kituo Kikuu cha Polisi jijini Arusha leo asubuhi kwa mahojiano kuhusu tukio hilo.


Chanzo: Mpekuzi
 
John Pombe Magufuli, Rais wa jamuhuri ya muungano wa tanzania, Mrisho Gambo RC wa arusha anakuvua nguo hadharani.

Chukua hatua yenye tija kwa jamii ya wanaarusha.
Liingie sikio hili litoke sikio la upande wa kule.....
 
Hivi huyu kijana aliweza kuhudhuria mazishi ya yule Padri!? Maana kwa kufanya hivyo walau unajifunza jinsi ya kutumia nafasi yako kuwatumikia watu na watu kukuheshimu badala ya kuwaweka mahabusu kila uchao!
 
Heeheee, anadhani Karatu ni Kasulu eeeh?1 Wale watu wanajitambua ndio maana Majaliwa aliongea nao kwa busara, unamfanyia ubabe mtu wa Karatu ?! Kweli Gambo mgeni Arusha acha anyooshwe, leo wamemzomea na kumuachia uwanja akienda tena hata pata wa kumsikiliza ili azomewe, any way acha madiwani waje Arusha kwa garama za serikali maana huu ni msimu wa holiday wacha waje wale mbzu kwa muoromboo.
 
kama habari hizi ni zakweli labda na mimi nitoe kamchango kangu Kadogo kuhusu jambo hili.

Naomba Nitunge Kamethali kangu.

"Liwali Mzuri ni huye Akubaliye kuosolewa Hasa Pale Anapo Kosea,

utumia Makosa Anayokosolewa Kujirekebisha ili Awe Bora Zaidi"

"Udhaifu wa Makosa ni Mtaji Mzuri sana Ukiutumia Kujirekebisha"

" Uthabiti wa Mtu Udhihirika Pale Unapotenda Kwa Busara"
 
Mbona wakati wa Nyerere Ma RC walikuwa vijana kabisa na waliwaheshimu wananchi na wao wakaheshimiwa na mambo yalikwenda vema, kwanini vijana wasasa wanapenda kugombana na wananchi wao, je kunakuwa na tija gani kwakuwepo mifarakano?
 
Chakujiuliza kama wananchi wanaona utendaji wako si wakuridhisha kuna ubaya gani kutoa maoni yao?

Iachie mahakama itasema kama wana hatia au la.

1.Unaweza kuita kuwa walizomea mkuu wa mkoa lakini mbele ya sheria ikaonekana walifanya vurugu kwenye mkutano halali wa mkuu wa mkoa na kusababisha mkutano kuvunjika na watu kuamua kuondoka kwa hofu ya uvunjifu wa amani

2.ulisaema mwenyewe kuwa walijichukulia sheria mikononi na kuanza kuteketeza mashine za pampu za maji za watu popote walipozikuta.Wao wanatakiwa wakathibitishe mahakamani kuwa wana uhalali kisheria kujichukulia sheria mkononi na kuteketeza mali ya mtu mwingine awe mhalifu au la na wakathibitishe hizo mashine walizoteketeza kama hawakuwapora watu majumbani mwao na wathibitishe kama walizikuta mtoni na si majumbani mwa wamiliki
 
Tumeanza kuwaweka jela hata wananchi wenye kutaka kutoa malalamiko yao? Mwambie Gambo hapo ndipo ulopoharibu kabisa. Wairaqw siyo waoga kama watanzania wengine. Kama walimbishia Mwalimu Nyerere ambaye walimpenda sana na kumweka Herman Sarwatt madarakani kwa kuwa tu ndiye waliyekuwa wanamwamini hata akiwa nje ya Chama tawala itakuwa Gambo?
Bahati nzuri Mwalimu aliwaelewa vizuri na kuwahandle with care hata kumpa Herman vyeo mbali mbali kwa mfano mwakilishi wa EA Legislative Assembly.
Angeamua kupambana naye angepoteza.

Same na Dr.Slaa. Ccm ilipomkataa kuwa mgombea nafasi ya ubunge hadi leo wakapoteza Karatu. Chezea kwingine siyo Wairaqw. Wale siyo wabantu. Wana asili ya kuamini kuwa kila moja ana haki hata kama ni mdogo ama maskini.
 
Habari iliyotufikia hivi punde kutokea Mkoani Arusha zinatanabaisha kuwa Baada ya Ziara ya mkuu wa Mkoa wa Arusha Kuingia doa kwa wananchi kumzomea wakati akizungumza kwa kutoa kauli iliyokuwa inapingana na maelezo yaliyotolewa awali na Waziri mkuu Kasim Majaliwa, Kwaaibu hiyo ya kuzomewa na wananchi hao kumuacha peke yake uwanajani Mkuu huyo wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo aamuru madiwani na wananchi 11 wakamatwe.

Tunapotoa taarifa hii madiwani hao na wananchi 11 wanaletwa Arusha mjini kwenye ofisi ya RCO.

Chakujiuliza kama wananchi wanaona utendaji wako si wakuridhisha kuna ubaya gani kutoa maoni yao?
Akili za kitoto sana. Ivi mtabadirika lini
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom