Arusha: Askari SUMA JKT wakamatwa kwa tuhuma za mauaji


Askari watatu Suma JKT wakamatwa kwa tuhuma za kutesa hadi kuua mtuhumiwa​

TUESDAY SEPTEMBER 07 2021​



MAUAJI PC

Summary

  • Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha linawashikilia askari watatu wa Suma JKT kwa tuhuma za kumtesa hadi kumuua mkazi wa eneo la Ngaramtoni wilayani Arumeru, Almasi Mohamed wakimtuhumu kwa wizi wa mahindi.
ADVERTISEMENT

New Content Item (1)

By Mussa Juma
More by this Author

Arusha. Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha linawashikilia askari watatu wa Suma JKT kwa tuhuma za kumtesa hadi kumuua mkazi wa eneo la Ngaramtoni wilayani Arumeru, Almasi Mohamed wakimtuhumu kwa wizi wa mahindi.

Kamanda wa Polisi Mkoa Arusha, Jastine Maseju akizungumza na Mwananchi leo Jumanne Septemba 7, 2021 amesema watuhumiwa hao ni walinzi shamba la Wakala wa Taifa wa Uzalishaji na Uendelezaji wa Mbegu za Kilimo (ASA) lililopo eneo la Ngaramtoni wilayani Arumeru.

"Ni kweli tunawashikilia askari watatu wa Suma JKT na upelelezi unaendelea wa tukio hili la mauaji na tutatoa taarifa rasmi baada uchunguzi kukamilika,"amesema.

Mke wa marehemu, Mwanahamisi Rajabu amesema mume wake kabla ya kufariki juzi alikuwa na majeraha ya kipigo na alilazwa katika hospitali ya Olturumet akiwa anatapika damu.

"Nilipigiwa simu na polisi kuwa mume wangu amelazwa hospitali anaumwa sana kutokana na kipigo nikaenda na kumkuta ana hali mbaya na akanieleza kwa taabu kilichotokea na baadaye akafariki,"amesema.

Mwenyekiti wa Kitongoji cha Seuli, Elias Ndemlya amesema marehemu alikuwa ni mkazi wa eneo lake akijihusisha na kilimo na aliwahi kuwa mfanyakazi katika shamba hilo.

ADVERTISEMENT

"Hili sio tukio la kwanza baadhi ya askari wa Suma JKT wanaolinda shamba kupiga watu na kujeruhi wakiwatuhumu ni wezi tunaomba Serikali ichukuwe hatua kukomesha ukatili huu,"amesema
 
Back
Top Bottom